Nadhani wote ni wazima humu,
Nafurahi sana kwa wote ulionitaja humu ndani,na feeling proud this is much respect to me,may God be with u all.
Wengi wetu humu hatujui maana ya "RASTA",ngoja niwape maana kwanza ilitujue hawa watu wakoje,tuwatofautishe na watu walio na dreadlocks,maana sio kila mwenye dreadlocks ni RASTA....
RASTAFARAI(Wakati mwingine huitwa (URASTAFARAI)..
NI DINI kama ilivyokuwa Dini nyingine kibao(Christian,Muslim and so on)..
Iliyoanzishwa huko Jamaica miaka 1930.
Wakati mwingine dini hii hutambulika pia kuwa mfumo wa maisha na vuguvugu la kitamaduni.
Mfalme wa zamani ETHIOPIA [emoji1098], (HAILE SELASSIE),anapewa umuhimu wa pekee,MARASTA wengi humuona kama mwili wa "JAH" duniani na kama ujio wa pili wa "YESU" KRISTO.wengine humwaona kama nabii wa kibinadamu ambaye alitambua kikamilifu uungu wa ndani ya kila mtu.
MARASTA wengi wanasisitiza waafrica waliopo nchi za magharabi kurudi Africa [emoji288] ,wanaamini kuwa bara la Africa ni nchi ya ahadi ya Sayuni..
MARASTA huita mfumo wao wa maisha UHAI-(LIVITY),ibadan zao huita MSINGI-(GROUNDATIONS).na hujumisha MZIKI,KUIMBA,MAJADILIANO NA BANGI-(ambayo huonekana kama SAKRAMENT)..
MARASTA wengi hula vyakula vya asili bila NYAMA wala CHUMVI(vyakula hivi huitwa itali).wanaacha nywele zao kukua bila kuchanwa au kukatwa(DREARDLOCKS)
RASTAFARI ilitokea miongoni mwa jumuiya za WAJAMAICA WEUSI,maskini katika miaka ya 1930,ITIKADI yake ya UAFRICA Ilikuwa jibu dhidi ya UTAMADUNI wa KIKOLONI wa JAMAICA..
Sio kila mwenye dreadlocks ni Rasta,URASTA NI IMANI kama zilivyo imani tofauti tofauti hapa duniani,Wengi wao husokota nywele ili wapate WAZUNGU kwa kuwa WAZUNGU wanawapenda sana MARASTA maana ni watu wapole,waelewa sana na wanyenyekevu,MARASTA ndo watu wa asili kabisa wa AFRICA,ambapo mkuu wao alitokea ETHIOPIA [emoji1098], NA ndo nchi haikutawaliwa na WAKOLONI,wengi watu hujificha kwenye kivuli cha URASTA ili wapate PESA,NA MAHITAJI YAO YA KIMAISHA,ni kama WACHUNGAJI FAKE NA MASHEHE MCHWARA(WAONGO)..ambao sasa tunasikia kila siku kwenye vyombo vya HABARI matukio mara PADRE KALAWITI WATOTO 10,mara SHEHE kalawiti vitoto n.k.
Hao wote wanaofanya vitendo vya ushoga sio MARASTA wa IMANI bali ni wenye nywele ndefu zilizosokotwa wasio NA IMANI ya ndani,bali wanatumia kigezo cha kusokota nywele iliwaonekane ni MARASTA wa kweli,mimi nachojua ni watu tu wakawaida..
Nadhani nimejibu majibu ya wote humu ndani,nashukuru kwa uzi wenye tija juu ya jamii yetu hii pendwa ya URASTAFARAI..
HOW YO TREAT OTHERS IS HOW YOU REALLY FEEL INSIDE..
"BOONOONOOONOOOS"