Sheria ipo lakini mbele ya sheria, mwanamke anapewa uzito zaidi. Hii kesi kwa kuwa mwnamke anadai amenunua uwanja yeye, kajenga yeye kama ingetokea wanatalikiana nibau nyumba iuzwe au abaki nayo mwanamke na watoto wake.
Siku hizi ukienda mahakamani mwanamke mwenye watoto ndio anabaki na nyumba na watoto wake. Mahakama haziuzi nyumba siku hizi. Watu kibao wanatakikiana na nyumba "matrimonial property" anabaki nayo mwanamke na watoto wake.
Utadai iuzwe, mahakama itakuuliza watoto wakakae wapi? Badae haki za watoto zitaangaliwa kwamba wanatakiwa wawe na makao. Badae utaambiwa kisheria watoto wanatakiwa wakae na mama yao hasa wale wadogo chini ya miaka saba. 😊
Hapo mwisho wa siku, itatafutwa mali nyingine utapewa wewe na nyumba atabaki nayo mwanamke na watoto wake. Kama una nyumba mbili lazima uache moja.
Kuna jamaa nyumba yao (yeye n mkewe) ilipigwa mnada na benki. Mwanamke akaenda mahakamani, mahakama ikaamuru jamaa ampe nyumba nyingine mke wake akae na watoto na wakatalikiana. Mpaka leo mwanamke anakaa pale na watoto wake.