BK ndoa ipo hivi; wakati mpo kwenye ndoa manakuwa "blindfolded" hamna mawazo kama ipo siku mtatengena au kudhulumiana au kuanza kugombea mali. Utakuta mwanamke amekuta jamaa ana pagara, yeye akainua renta, akapiga bati. Mawazo ya yanakuwa ni chetu/chao. Kunakuwa hamna mawazo hayo ya kuanza kugombania vitu.
Sasa itakapofikia mapenzi yenu yameisha au kukaanza hila (kutoka upande wowote), ndipo kila mtu anaanza kuhesabu alifanya jini na alichangia nini na alitoa nini. 😊
Hapo ndipo kesi inapoanzia. Kisheria mwanaume akikuta una uwanja au hata nyumba na akashiriki kuiendeleza nyumba hiyo, hata kidogo basi nyumba ile inakuwa "matrimonial property".
Hivyo hivyo na mwanaume, mke akikuta una biashara au nyumba na akashiriki kuiendeleza kwa fedha/nguvu kazi basi mali hiyo anakuwa na uhusika nayo.
Kwa mazingira hayo; hiyo nyumba ya Kweka ilikuwa ni "matrimonial property" nyumba ya ndoa. Maana wote wawili wameishi hapo, wameendeleza nyumba. Hata kama mwanamke alikuwa anafagia na kupunguza majani. Hiyo ni nyumba ya ndoa, wote wanaimiriki kwa mazingira hayo.