Marehemu Jane ndiye aliyenunua kiwanja na kujenga, alitaka jina lake liwe kwenye hati

Marehemu Jane ndiye aliyenunua kiwanja na kujenga, alitaka jina lake liwe kwenye hati

Kama yeye ndo alinunua kwanini hakuweka majina yake toka mwanzo?
Kuna ile mkiwa na mahusiano mazuri, unaona huyu ndo baba afu kidogo unamzidi sasampa kuna ile hali unatamani mwanaume abaki kuwa mwanaume ukiamini mnatafuta kwa ajili yenu na watoto, ila shida inakuja pale mwanaume ameanza kukuzoea na kukuchoka kiasi michepuko ndo imepanda cheo ohoo akili inarudi ghafla kutaka sasa kila mtu akae kwenye 70 yake mwanaume naye ni mbinafsi kiujumla hapendi mwanamke amiliki chochote kinachompa jina mjini anajiuliza ntaambia nini watu na wote wanajua hapa ni kwangu?
Ndo unyama umetokea hapo
 
Ambacho nimeshuhudia kwa wanawake wengi waliopenda, huwa hata kama pesa ni yake imetumika kununua kiwanja na kujenga huwa wanaacha umiliki usome kwa mwanaume kwa ajili ya kumpa heshima mwanaume.

Mapenzi yanapoisha ndio hapo mwanamke huanza kusema "kwanza hii nyumba nilijenga mimi"
Swadakta
Mapenzi/mahusiano yakisha expire vituko ndiyo uanza

Ova
 
Mhhhh una mke? Maaana usikute unaongea nadharia.

Wanaume wengi humu ukiuliza taarifa za upatikanaji wa viwanja sehemu fulani huwa zinatolewa na wake zao (utasikia mme wangu kuna kiwanja mama fulani kaniambia kinauzwa seheku fulani), tusikiache kile kiwanja kizuri sana.

kwa vile wanauke waja ubize mwingi, mara nyingi hutukia wake zao hela walipie kiwanja husika. Huwa tunachukulia simple ila siku zinavyozid kwenda ndio unakuja kujua kale kabarua ka mwenyekiti wa mtaa na mashahidi wa pande nne za kiwanja kana impact kubwa sana sio ka kuchukulia poa poa.

hakikisha kiwanja unaandikisha mwanaume na mkewe awe shahidi, lakini pia kama una kampuni yako, nunua viwanja kwa jina la kampuni hiyo.
Achana na wale wanaokaa nyumbani ila pia wana akili ya kujenga familia wanatoa ushauri mzuri kwa waume zao na kweli familia zinasimama...huyo dada alikuwa mtafutaji mjini, alikuwa akifanya kazi usifanye uwezo wa mkeo ndo uwe wa wanawake wote....kuna wanawake wana matusi mjini bana mwanamke anajenga mpaka waja wanasema anahongwa na juhudi za kuzitafuta zionekana
 
Kuna jamaa alisema usioe mwanamke mwenye kipato kikubwa

Kuoa hakuna kanuni, ujuzi wala fundi. Kuna jamaa alioa mwanamke wa kawaida tuu, hana kipato chochote lakini kwao mwanamke, wakaja uza nyumba yao magomeni kwa bilioni, mgao ukafanyika mke wa jamaa akapata hela za kuzidi. Na hakumuacha mshikaji.
Yupo mtu anaolewa ndio anapata hela, yupo mtu anaoa ndio anatajirika.
 
Sasa kaamua yeye, acha amlete...

Nadhani atanipa tu hasira ya kutafuta mali...

Nitaanza moja na nitajenga nyumba nzuri zaidi... na asipokaa vizuri atarudi kuja kuniomba msaada and guess what? Nitamsaidia ili ajione mjinga na kipindi hiko nimeoa mwanamke mzuri zaidi yake...

Siwezi kuua mtu kisa kaamua akapigwe miti kwa starehe zake na anataka nyumba iwe mali yake...
Na huyo mzuri uliyemuoa baadae naye qnakuja kulianzisha tena.......vicious cirlce inqendelea
 
Rebecca amedai Jeni alikuwa akitaka kubadili majina yaliyokuwa kwenye hati ya nyumba ili kubakiza jina lake na la watoto wao, akieleza kuwa yeye ndiye aliyenunua kiwanja na kujenga nyumba hiyo.
Mke wake ametokea Kilimanjaro ( Angemalizia kabisa kwa kusema ni .. Mchaga)

Kwani hakuna watu wa jamii nyingine wanaopiga matukio kama hayo au ni mtazamo wako tu kuhusiana na hiyo jamii
 
Rebecca amedai Jeni alikuwa akitaka kubadili majina yaliyokuwa kwenye hati ya nyumba ili kubakiza jina lake na la watoto wao, akieleza kuwa yeye ndiye aliyenunua kiwanja na kujenga nyumba hiyo.
Mke wake ametokea Kilimanjaro ( Angemalizia kabisa kwa kusema ni .. Mchaga)
😂😂😂
 
Achana na wale wanaokaa nyumbani ila pia wana akili ya kujenga familia wanatoa ushauri mzuri kwa waume zao na kweli familia zinasimama...huyo dada alikuwa mtafutaji mjini, alikuwa akifanya kazi usifanye uwezo wa mkeo ndo uwe wa wanawake wote....kuna wanawake wana matusi mjini bana mwanamke anajenga mpaka waja wanasema anahongwa na juhudi za kuzitafuta zionekana
Point yako ni nini? Kwani mbona wanaume wanatafuta wanawalisha, wanajenga na kujivunia hii ni mali ya familia.

Iweje nyie mnaojiita watafutaji iwe nongwa.?
Pili sijaongelea mwanamke mkaa nyumbani na mfanyakazi, ila kwa ufupi wanawake wengi ndio hufuatiloa mambo ya eneo fulani au shamba fulani linauzwa mahali fulani, kwa sababu katika Maisha kipao mbele cha 99% ya wanawake ni nyumba kwanza na vyombo vya ndani. Ilihali sisi wanaume 90 ni projects/biashara, gari na furnitures.
 
Sasa wewe ndio mnunuzi kwa nini risiti uandike jina la mtu mwingine? Kuna kitu hakipo sawa.
Hapo hata mimi nashangaa ,kwanini uandike jina la mtu mwingine wakati wewe ndo unanunua? Hata wale wanaoandika majina mawili ilihali anayetoa pesa ni mmoja,nao ni ujinga.Niliwahi kufanya hivyo,kimbembe kikaja ,mwanamke hatuelewani na nataka kuuza kiwanja.Mwanamke akamwambia dalali kiwanja kisiuzwe.Ndo nilijifunza kitu.Ukitaka tuandike majina mawili toka pesa nusu basi.
 
Mwanamke akiwa amenunua uwanja na amejenga nyumba kwa pesa yake, ni ya kwake. Huyo jamaa hata kama alichangia lakini nyumba ni ya Mwanamke. Huyo Mangi wa wapi, alitakiwa astuke mapema sana awe na ya kwake pembeni. Haya sasa anaishia jela na nyumba watakaa watu wengine.
Jamaa ana hela kwao pia zipo hizo stories za kuokoteza tu, mbona jamaa anafahamika tu
 
Tukio la kushtua limetokea Mtaa wa Senzele, Kata ya Bunju B, jijini Dar es Salaam, baada ya Laurent Kweka kudaiwa kumuua mkewe, Jeni Urassa, kwa kumpiga risasi kichwani kisha kujisalimisha Polisi.

Tukio hilo linadaiwa kutokea Alhamisi, Oktoba 1, 2026, majira ya saa 11:30 alfajiri ndani ya nyumba ya wanandoa hao. Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Faustine Mafwele, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mtuhumiwa anashikiliwa kwa ajili ya upelelezi.

Kwa mujibu wa Mafwele, Laurent na marehemu walikuwa wanandoa na wote walitoka mkoani Kilimanjaro. Ameongeza kuwa baada ya uchunguzi na taratibu za kisheria kukamilika, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Mfanyakazi wa ndani wa familia hiyo, Rebecca Mbasha, ambaye amefanya kazi nyumbani hapo kwa miaka minane, amesema mauaji hayo yanadaiwa kufuatia mgogoro wa muda mrefu wa kifamilia kuhusu umiliki wa nyumba.

Rebecca amedai Jeni alikuwa akitaka kubadili majina yaliyokuwa kwenye hati ya nyumba ili kubakiza jina lake na la watoto wao, akieleza kuwa yeye ndiye aliyenunua kiwanja na kujenga nyumba hiyo.

Amesema siku ya tukio Laurent aliingia nyumbani na baada ya muda mfupi alimsikia Jeni na baadaye akasikia kishindo. Aliporejea ndani, alimkuta Laurent akitoka chumbani akiwa ameshika bastola na kumwambia, “nimeshamaliza kazi.” Rebecca alipokwenda chumbani alimkuta Jeni akiwa ameanguka chini akiwa na jeraha kichwani.

Kwa upande wake, Jacqueline Nkaya, ambaye ni mama mdogo wa marehemu, amesema wanandoa hao walikuwa na mgogoro wa muda mrefu na wakati mmoja Jeni aliwahi kutishiwa kuuawa kwa bastola na mumewe, jambo aliloliripoti Polisi.

Amesema Laurent aliondoka na kwenda Kilimanjaro ambako alikaa takribani miezi miwili kabla ya kurejea Dar es Salaam siku ya tukio.

Majirani wamesema hawakuwa na taarifa za migogoro hiyo, wakieleza kuwa familia hiyo ilikuwa ikionekana kuishi kwa amani tangu ilipohamia katika nyumba hiyo Desemba 2025.

Marehemu ameacha watoto wanne, watatu wakiwa shuleni na mmoja bado hajaanza shule.
Chanzo : Global

Vijana tuache kulazimisha mambo tufanye kazi tusing'ang'anie mali za wanawake


Kuna wanaume siku hizi, wanaume suruali. Hawajali lolote. Kazi yao ni kutafuta wanawake wa kuwaleoa
 
Sema wanawake bwana mda mwingine wanatuvuruga sana, yaani wamehamia kwenye nyumba mwaka jana tu disemba hata mwaka hawajamaliza ila tayari mwanamke anataka hati ya nyumba na kiwanja majina yabadilishwe yaandikwe yake. So sad

Kweka alikuwa anafanya kazi au biashara gani?

Maana mwanaume asiye na kipato, ana bunduki tu mfukoni, ni hatari na nusu
 
Back
Top Bottom