Marekani angeivamia Iran halafu asisaidiwe na nchi nyingine, awekewe vikwazo, halafu Urusi, China, nk ziipatie Iran silaha je, angetoboa?

Marekani angeivamia Iran halafu asisaidiwe na nchi nyingine, awekewe vikwazo, halafu Urusi, China, nk ziipatie Iran silaha je, angetoboa?

Mimi nawashangaa sana watu humu ujue! Jamii forum ni kokolo tunatofautiana sana uelewa. HAIPO NCHI DUNIANI YA KUIWEKEA MAREKANI VIKWAZO. Teh teh teh kwamba " kwamba tunawawekea vikwazo hatutumii ndege zenu za Boeing"
Mbona Russia kawekewa vikwazo lakini gas yakd wanatumia? Kwamba kwakuwa USA kawekewa vikwazo basi na sisi hizi boeing zetu tulizonunua cash tutazipaki??
 
Mbona Russia kawekewa vikwazo lakini gas yakd wanatumia? Kwamba kwakuwa USA kawekewa vikwazo basi na sisi hizi boeing zetu tulizonunua cash tutazipaki??
Nilimainisha kwamba,kumuwekea vikwazo M arekani ni ngumu ikiwa ni pamoja na kukataa kununua ndege zake za Boeing pamoja na vipuli vyake. Kuiwekea Marekani vikwazo is an assumption of non existing fact.
 
Hivi Marekani angejichanganya leo akaamua kuivamia Iran kwa kuitumia ardhi ya Iraq lakini asisaidiwe na nchi nyingine, awekewe vikwazo kama alivyowekewa Urusi.

Halafu Iran isaidiwe silaha mfululizo na Urusi, China, India, na nchi zingine za kiarabu, je Marekani angestahimili kwa muda gani? Ujue kupigana ukiwa umewekewa vikwazo ni kama kupigana ukiwa umefungwa pingu!
Hawezi kustahimili, atatumia nuklia.
 
Nilimainisha kwamba,kumuwekea vikwazo M arekani ni ngumu ikiwa ni pamoja na kukataa kununua ndege zake za Boeing pamoja na vipuli vyake. Kuiwekea Marekani vikwazo is an assumption of non existing fact.
Swali langu nafikiri hujajibu, kwani Russia si kawekewa vikwazo? Kwanini Gas yake wananunua? Kwanini unadhani Boeing ndio hawatafanya biashara na nchi au wateja wake?
 
Umuwekee vikwazo USA Basi husitumie, Pepsi, Coca-Cola, Colgate,Google, Facebook, watsapp, Tweeter,

Husitumie Dollars, Master card, visacard, paypall, husitumie Boeing, ARV, chanjo za magonjwa. Ulipie 1/3 za mchango kwa UN. Ulipie 2/3 ya bajeti ya WHO

Hudumia kambi za wakimbizi, asa Africa, fafhiri UNHCR, UNO, WFP.

Baada ya hapo muwekee US vikwazo [emoji2][emoji2]
Bado awajaijua USA vizuri uyo Iran USA akiamua kuipiga siku3 nyingi watu watakuwa wanakunywa kahawa Tehran
 
Hahahahaha if he is all that mbona hathubutu kusogeza pua pale Ukraine?? Yeye si ni kiranja wa dunia??

Sasahivi waandishi wa Habari wa Ukraine wanaanza kuilaumu US wakati wao ndio walikuwa mstari wa mbele kuwavimbisha vichwa..

Vipi si yule Comedian alihutubia senate akaomba apewe "no fly zone" huyo baba wa dunia mbona mpaka leo hajatoa hiyo no fly zone?? Yeye si ndo yeye bana
Ndugu yangu hakuna duniani anayependa vita,Us na Nato Wala hawajaogopa kuweka fly zone kwa sababu hizo unazojua wew. Kuweka fly zone pale Ukraine is an act of war( nikujiingiza moja kwa moja vitani kitu ambacho si sahihi kabsa. Sasa nikuulize Urusi alitamka mwanzoni kabsa kuwa atayeingilia huo mgogoro wa Ukraine atapata athari ambazo hajawahi kuzipata tangu dunia iumbwe,sasa kwa ufahamu wako hizo nchi zinazopeleka silaha huko hazijaingilia huo mzozo? Naje Urusi ameziwajibisha namna gani kama alivyo ahidi?
 
Umechanganya!! Umoja wa mataifa hauhusiki katika kuiwekea vikwazo Urusi pia hautahuisika kuiwekea vikwazo marekani. Kwa hiyo michango yake UN ataendelea kupeleka! Dola za kazi gani, si makaratasi tu hayo? Akiwekewa vikwazo tunaachana na dola tunakubaliana kutumia kila nchi pesa yake! Wakimbizi wataendelea kuhudumiwa na UN maana yenyewe haitahusika.

Ukweli ni kwamba Marekani atapigwa ka mtoto mdogo!!
nenda kahangalie bajeti ya UN vizuri then ndio uje apa 50% yote anatoa USA kaangalie izo nchi zako wakina china na Russia wanatoa % ngapi
 
Marceneries wangetoka Dunia nzima kuja kuipiga USA ,nchi nyingi sana zingeosaidia Iran kuipiga USA, USA ni dhaifu sana ,
Inachukiwa sana, nakuhakikishia Kuna nchi za NATO zingetoa misaada kwa Siri ili kuiadhibu USA.

Na hii ndio sababu kubwa amabyo inapelekea USA kuingia vitani na wapambe.kuogopa aibu ya kupigwa peke yake.
Ona mifano midogo TU

USA ilipelekea askari wake somalia,ilijikuta inadhalililishwa na wababe wa kivita wa Somalia,akina Mohamed Farah Aidiid.Gen Morgan na wenzao.

Askari wa Marekani walipigwa na wasomali,wakauliwa,wakatekwa na baadhi Yao wakafungwa kwenye magari kwa nyuma wakiwa miguu imefungwa kamba na kufungwa kwenye magari,wakawa wanaburuzwa magari yakipita mitaani.

Kitendo hicho kiliibua chuki ya wananchi wa USA dhidi ya Serikali Yao na hatimae Serikali ikatoa agizo majeshi ya USA yaliyoko somalia yaondoke huko.

Na huo ukawa ni ushindi wa makundi hayo ya kisomali.

USA ilishindwa somalia.
somalia na USA ile ilikuwa ni gorilar war siyo vita rasmi ile vita gani watu wanajichanganya na raia wanavaa nguo za kawaida kama wananchi? ulitaka USA apige raia
 
Ndugu yangu hakuna duniani anayependa vita,Us na Nato Wala hawajaogopa kuweka fly zone kwa sababu hizo unazojua wew. Kuweka fly zone pale Ukraine is an act of war( nikujiingiza moja kwa moja vitani kitu ambacho si sahihi kabsa. Sasa nikuulize Urusi alitamka mwanzoni kabsa kuwa atayeingilia huo mgogoro wa Ukraine atapata athari ambazo hajawahi kuzipata tangu dunia iumbwe,sasa kwa ufahamu wako hizo nchi zinazopeleka silaha huko hazijaingilia huo mzozo? Naje Urusi ameziwajibisha namna gani kama alivyo ahidi?
Nafikiri hakuna nchi iliyopeleka jeshi na hata visilaha vidogo vidogo wanavyopeleka havina athari kubwa. Nafikiri Russia pia alimaanisha nchi itakayothubutu kupeleka jeshi au wanajeshi wa Nato kupelekwa. Hiyo fly zone pia ni kuingilia na ndio maana US na washirika wake wamemgomea Ukraine kuweka no fly zone.
 
Marekani akiwekewa vikwazo na China maana yake China iache kuuza bidhaa zake Marekani, kwa mwaka China inauza zaidi ya dola bilioni 400 kwa Marekani. Kwa hiyo China wawe vilaza waache kupata bilioni 400 kwa mwaka wabaki kwa Russia kupata dola bilioni 50 kwa mwaka, hii ni 1 ya 8.

Wakati huo China ikose patents zote za Marekani. ZTE ilipigwa sanctions na Marekani mpaka leo hatuoni simu zake, Huawei ilipigwa sanctions mpaka ikafungua biashara ya kufuga nguruwe ili kutosheleza profits. Patents za teknolojia ya simu nyingi ni za makampuni ya Marekani. Hata TCMS wataambiwa hakuna kuuza microchips kwa China wala Russia, Samsung Electronics mnayoona hii Marekani ikitaka ipotee sokoni ndani ya miaka minne inaweza potea. Ukipiga marufuku wasitumie foundry tech ya US kutengeneza chips zao za Exynos, au kufanya outsourcing ya chips kutoka kwa Qualcomm ya Marekani. Kwahiyo Samsung nao watachagua upande wa Marekani kuliko China na Russia.

China akishindwa kuzalisha zaidi kwa ajili ya kuuza Marekani atapunguza mahitaji ya gesi na mafuta kutoka Russia na kwingineko, hapo Russia anapunguza mapato, soko la mafuta duniani linashuka uchumi wa OPEC wote unaporomoka na dunia kwa ujumla inaingia mdororo wa uchumi. Marekani inaweza zalisha mapipa milioni 15 ya mafuta kwa siku ukijifanya unaikomoa, kwa siku inatumia mapipa milioni 19 hizo nne zinazokosa kwenye mlinganyo inatafuta hata Libya inawahonga wanaiuzia extra.

Kampuni kama Boeing zinaacha kufanya kazi China na Russia. Pia Dell, HP, Apple, Sony, etc. GPS inafungwa wabaki na GLONAS zao na BeiDou ambazo sio reliable na hazina global support. Android system inafungwa na iOS tuone ni Mwafrika gani ataanza kujaribisha systems ambazo hajawahi sikia. Facebook, WhatsApp, Twitter, Instagram zinafungwa kwao na kwa vifaa wanavyotengeneza. Warusi wabaki na VKontakte (ambayo najua 98% ya wabongo hawajawahi hata kuisikia) na Wachina wabaki na kina WeChat, Weibo na TikTok. Ukiachana na TikTok ni nani duniani hapa atataka aache hizo nyingine atumie VKontakte au Weibo na WeChat?

South Korea, Japan, UK, Germany, France, Australia, Italy, Spain, Canada zitasimama na Marekani. Israel na Switzerland wanaweza chagua kuwa neutral, Waarabu vigeugeu kupindukia watasoma upepo ila wengi watakuwa upande wa Marekani. Yani Qatar aache kuwa upande wa Marekani ambako kila giant aliyeko kule anajiweza na gesi hana, aende kushiriki na China ambako Russia anamuuzia gesi kwa fujo?
Bado awajaijua USA vizuri ,kiufupi USA ndio baba wa tech duniani
 
Swali langu nafikiri hujajibu, kwani Russia si kawekewa vikwazo? Kwanini Gas yake wananunua? Kwanini unadhani Boeing ndio hawatafanya biashara na nchi au wateja wake?
Kumuwekea vikwazo ni pamoja na kukataa product zake Kama Boeing na vipuli vyake, the main essence ya kuiwekea vikwazo nchi ni ili kui suffocate kiuchumi, kama ni kiumbe hai kikose pumzi ya ku support life. Ndio maana nikasema nchi inayoiwekea vikwazo Us itakataa kununua Boeing na parts zake? KAKA NIMECHOKA KUELEZA... WEKA PEMBENI CHUKI DHIDI YA MAREKANI URUHUSI FIKRA HURU. Hiyo scenario ya mtoa mada is quite inapplicable ( haitekelezeki) over
 
Hivi Marekani angejichanganya leo akaamua kuivamia Iran kwa kuitumia ardhi ya Iraq lakini asisaidiwe na nchi nyingine, awekewe vikwazo kama alivyowekewa Urusi.

Halafu Iran isaidiwe silaha mfululizo na Urusi, China, India, na nchi zingine za kiarabu, je Marekani angestahimili kwa muda gani? Ujue kupigana ukiwa umewekewa vikwazo ni kama kupigana ukiwa umefungwa pingu!
Una homa sana hiyo itawezekana vipi mkuu? ukiambiwa Marekani ime invest muda mrefu duniani elewa hivyo., ili umuhame Marekani inabidi uanzishe mambo yako kwa miaka mingi sana, China alitaka kujaribu bila ya Marekani ikashindikana unataja Iran wakati Iran wenyewe saiv wanaomba kuondolewa baadhi ya vikwazo walivyoekewa na Marekani
 
Kumuwekea vikwazo ni pamoja na kukataa product zake Kama Boeing na vipuli vyake, the main essence ya kuiwekea vikwazo nchi ni ili kui suffocate kiuchumi, kama ni kiumbe hai kikose pumzi ya ku support life. Ndio maana nikasema nchi inayoiwekea vikwazo Us itakataa kununua Boeing na parts zake? KAKA NIMECHOKA KUELEZA... WEKA PEMBENI CHUKI DHIDI YA MAREKANI URUHUSI FIKRA HURU. Hiyo scenario ya mtoa mada is quite inapplicable ( haitekelezeki) over
Mbona wewe bado hunielezi kwanini Russia anaendelea kuuza gas kwa hao mahasimu wake waliomwekea vikwazo.

Nielekeze hili kwanza nielewe mkuu..
 
Nafikiri hakuna nchi iliyopeleka jeshi na hata visilaha vidogo vidogo wanavyopeleka havina athari kubwa. Nafikiri Russia pia alimaanisha nchi itakayothubutu kupeleka jeshi au wanajeshi wa Nato kupelekwa. Hiyo fly zone pia ni kuingilia na ndio maana US na washirika wake wamemgomea Ukraine kuweka no fly zone.
Mfano Poland asingekuwa member wa Nato angepeleka hata mshale tu wa msaada Ukraine nini kingempata nusu saa tu badae. Hizo silaha unazosema ndogo ndogo ndizo zilizosababisha ile u turn( kugeuza faster) uelekeo kutoka kwenda mji mkuu na kukimbilia Donbas( Eastern side). Na pili hata hiyo misaada ya silaha ndogo ndogo inamchelewesha Urusi ku accomplish operation yake hivyo usizani anafurahia Ukraine kupata msaada,ikumbuke vita ni garama Kuna loss of life na economy pia, HATA URUSI MWENYEWE HAPENDI.
 
Mbona wewe bado hunielezi kwanini Russia anaendelea kuuza gas kwa hao mahasimu wake waliomwekea vikwazo.

Nielekeze hili kwanza nielewe mkuu..
Hilo la boeng ni mfano mmoja tu basi tufanye gesi na Boeing ziwe sawa ,sasa hemu tukae tujadili jamaa yangu. Hemu njoo na package ya aina ya vikwazo na nchi husika zitakazo weka vikwazo na effect ya vikwazo hivyo kwa ujumla upande wa Us na globally kama inawezekana. THE FLOOR IS YOUR STEPHEN CURRY
 
[emoji3538][emoji3538][emoji3538]Any supply of weapons to Ukraine, no matter how Washington argues them, increases the risk of a direct clash between the Russian Federation and the United States, Deputy Foreign Minister Ryabkov told RIA Novosti[emoji3538][emoji3538][emoji3538]
 
Sasa si achukue hatua
 
Mfano Poland asingekuwa member wa Nato angepeleka hata mshale tu wa msaada Ukraine nini kingempata nusu saa tu badae. Hizo silaha unazosema ndogo ndogo ndizo zilizosababisha ile u turn( kugeuza faster) uelekeo kutoka kwenda mji mkuu na kukimbilia Donbas( Eastern side). Na pili hata hiyo misaada ya silaha ndogo ndogo inamchelewesha Urusi ku accomplish operation yake hivyo usizani anafurahia Ukraine kupata msaada,ikumbuke vita ni garama Kuna loss of life na economy pia, HATA URUSI MWENYEWE HAPENDI.
Mbona ziko nchi haziko NATO na zilipeleka silaha na Russia hajazigusa?

Russia alionesha uanamme Syria kwa kupeleka jeshi kamili na mpaka leo Assad yupo na miji imekombolewa. Kwanini US na NATO wasiende kumtetea mwanachama wao wa baadae waliyempa kichwa?
 
Hilo la boeng ni mfano mmoja tu basi tufanye gesi na Boeing ziwe sawa ,sasa hemu tukae tujadili jamaa yangu. Hemu njoo na package ya aina ya vikwazo na nchi husika zitakazo weka vikwazo na effect ya vikwazo hivyo kwa ujumla upande wa Us na globally kama inawezekana. THE FLOOR IS YOUR STEPHEN CURRY
Mantiki ya huu uzi nadhani wengi hamjaelewa. Hata tunaongelea Ceteris Paribus, kwa maana mpaka hao wakubwa wafikie kukuwekea vikwazo ni kwamba wana mbadala wa hicho wanachokipata kwako.

US na Europe walikubaliana kuweka vikwazo baada ya kujua watakabiliana vipi na kile ambacho Russia anaoffer kwao. Na ndio maana pia walikimbilia kuseize mali nyingi za matajiri wa Russia zilizopo sehemu mbalimbali ili pia waweze kufinance hiyo vita. Sasa kwa muktadha huu tuanze kuimagine (kama ambavyo mleta uzi ameweka nadharia) solutions zote za ambacho US anaoffer kwa dunia zikapatiwa substitute na mali zote za US na Mabilionea wake zilizoko duniani zikanyakuliwa then US akabaki na washirika wachache kama UK, Canada, Australia ambao pia wao watabaki kutoa tu matamko na sio kumsaidia direct, Je ataweza kupambana na kushinda vita mwenyewe??

Lakini pia, Je unadhani Dunia inamuhitaji zaidi US kuliko US anavyoihitaji Dunia??
 
Back
Top Bottom