Zacht
JF-Expert Member
- Jul 17, 2020
- 1,026
- 2,266
Meya wa Hamtramck Michigan Amer Ghalib, alipata wadhifa huo wa Umeya, mnamo 2021 baada ya kumkosoa mtangulizi wake kwa kupeperusha bendera ya LGBTQ nje ya ukumbi wa jiji.
Baraza la jiji la Hamtramck, Michigan, ndio jiji pekee la Marekani lenye baraza linaloongoza Waislamu akiwemo na Meya, lilipitisha azimio hilo la kupiga marufuku maonyesho ya bendera za LGBTQ kwenye majengo ya umma.
Upigaji kura kwa kauli moja ulifanyika Jumanne usiku, na azimio lililowasilishwa na Meya pamoja na Diwani Mohammed Hassan.
Azimio hilo linafafanua kwamba, “Serikali ya Jiji la Hamtramck hairuhusu bendera zozote zenye kuonyesha kikundi cha kidini, kikabila, rangi, kisiasa au makundi ya kijinsia kupeperushwa kwenye majengo ya umma ya Jiji, ila bendera ya Marekani pekee."
Huku kukiwa na upinzani dhidi ya pendekezo hilo, Hassan aliwaambia wanao leta pingamizi "Tafadhali msitutishe. Mimi ndiye afisa nilyechaguliwa. Ninafanya kazi kwa ajili ya watu, na kile ambacho watu wengi wanapenda."
Detroit Free Press iliripoti.