Nangu Nyau
JF-Expert Member
- Jul 1, 2022
- 5,015
- 14,139
Dunia inapaswa sasa kuitambua haki ya wapalestina na kuacha kutoa upendeleo kwa Israeli, Wapalestina nao ni binadamu wanahitaji kuishi na kuwa na Taifa lao.
Dunia ijitahidi kubalance mambo ili amani ipatikane na Wapalestina wawe na Taifa lao pia.
Leo Wangoni wakiamua kutengeneza kitabu Chao na kusema ardhi yao ya ahadi ni South Africa Kwa Babu zao maana yake tutawaacha waende pale SA.
WaAfrica tunapigia kelele za uvamizi wa Boers pale SA, tutakuwa tayari kuwaunga mkono wakituambia pale ndio nchi yao ya ahadi kupitia kitabu chao?
Wachaga watoke Kilimanjaro waende kwao Ethiopia sijui na Mbilikimo wa DRC warudi kwao Kilimanjaro kwenye ardhi ya Babu zao aka nchi yao ya ahadi.
Dunia ilisimamia Timor mashariki wanapata nchi na kumeguka kutoka Indonesia na mpaka Leo hii amani imepatikana pale.
Leo hii Dunia inaisaidia Ukraine na kumuita Russia mvamizi na hata kumpa silaha Ukraine.
Kwanini ni Ngumu Palestina kuwa na Taifa lao na ilikuwa rahisi kuanzisha Taifa la Israeli miaka hii ya 1900 ilihali Wapalestina walikuwepo hapo na waisraeli waliondoka mahala hapo?.
Wapalestina kwao ni wapi? na asili yao ni wapi? Mbona tunaambiwa Ibrahim Baba wa Imani alitokeo Kaldayo (inasema ni Saudia) kwanini sasa Waisraeli wasiende kwenye asili ya Babu yao Ibrahim Kaldayo na kuamua kubaki kwenye maandiko ya kitabu ambacho kimsingi wanakiamini wao kwa Imani yao?
Kesho Hinduz wakiamka wakatuambia kwao ni USA kwa mujibu wa kitabu Chao basi tunaamini, Kesho ikizuka dini pale Buza na wakazi wa Buza wakatuambia kiasili na kiimani Kwa mujibu wa kitabu Chao na mitume yao ni UK nayo tuseme sawa wapishwe.
Wapalestina nao ni binadamu na wanapenda kuishi Kwa amani ndani ya Taifa lao kama Israeli na wengine wanavyoweza kuishi ndani ya mataifa yao.
Mwenyezi Mungu awabariki wote na kuwapa hekima yakuleta amani mashariki ya kati na watu wote pale wakaishi kwa amani kama kwingineko duniani.
Mwenyezi Mungu awafanyie wepesi wengine walio kwenye mtaziko wa vita na kutesa maisha yao mfano DRC, CAR, nk.