World Bank kama sehemu ya UN hupitisha mambo yanayojadiliwa na kupitishwa na vikao vya UN.
Na hili kupitishwa kwenye vikao vya UN si rahisi.
Kumbuka, China si Iran, nayo ni permanent member wa Security Council UN, na ina ushawishi mkubwa.
Zaidi, ujinga inayoufanya serikali ya Marekani - Trump for the most part-sasa hivi ni kudharau hata rafiki zake, kujifanya inaweza kufanya mambo peke yake.
Sasa hapo ndipo utakapokuja muda wa kupiga kura halafu rafiki za China wote wakapiga kura na China, rafiki za Marekani nao wengine wakapiga kura na China, wengine wasipige kura na wachache wakapiga kura na Marekani.
Kwa hiyo Mmarekani kwa sasa akishindana na Mchina kwenye mambo kama haya, na ikaonekana wazi Mmarekani analeta ubabe, atachinjwa kwenye kura tu hapo UN.