Uchaguzi 2020 Marekani: Kuanzia leo, tunaweka vizuizi kwa waliohusika na kuvuruga Uchaguzi nchini Tanzania

Uchaguzi 2020 Marekani: Kuanzia leo, tunaweka vizuizi kwa waliohusika na kuvuruga Uchaguzi nchini Tanzania

Kama humjui sasa umejuaje imechezewa! Hiko kitakuwa ni kihoja
Nimejua baada ya acc ya Trump ambayo anayotumia,kwani kwakufanya hivyo ni sawa umeminya UHURU WA KUJIELEZA na kwa kuminya uhuru huo manake,immeenda kinyume na KATIBA .

Au Kwani acc ya Trump imefungwa au haijafungwa?

Wewe kama unamjua niambie ni nani ambaye yupo juu ya KATIBA.
 
Kumzuia mtu kwenda Marekani nayo ni adhabu?
Wanazuia watembeza bakuri wetu mkuu.WB iliyotupa pesa ya kujenga flyover ubungo na barabara za mwendo kasi ipo Washington DC mkuu kama hujui
 
Sasa kwani ni serikai ya Trump iliyomfungia Trump account yake ya twitter? 😁
Huoni kumfungia ni sawa na kumnyima HAKI YAKE YA UHURU WA KUJIELEZA.

MANAKE KWA KUMINYA UHURU WA KUJIELEZA MANAKE UMEENDA KINYUME NA KATIBA YA NCHI.

AU labda US kuna watu wapo JUU YA KATIBA.
 
Sijui kama account yake imefutwa,ameifuta imesimamishwa au ameiuza. Wewe niambie imepatwa na nini.
Nimejua baada ya acc ya Trump ambayo anayotumia,kwani kwakufanya hivyo ni sawa umeminya UHURU WA KUJIELEZA na kwa kuminya uhuru huo manake,immeenda kinyume na KATIBA ...
 
Ahaaa... Yani mtoto wa Mahera apate tabu kisa baba kazuiwa kwenda USA?....
Ukiwa mr.wahapa hapa ni ngumu kuelewa tamko la wamarekani,lakini pia wanaccm huwa ni slow learners so just wait kama US wako serious you will see
 
Mahera inakuhusu hii
Hebu nikuulize...yeye huyo Pompeo mbona Ulaya wamemsusa alipotaka kwenda kuwaaga. Wote wamemkataa? Trump's era has got no influence at all. He should mention the names. And Biden can reverse the order as he will do with many others that are controversial
 
IMO they need to do more. This is not sufficient enough. The whole illegal cabinet and members of parliament from ccm should be included in this. Also economic sanctions similar to those of Zimbabwe should be put in place ASAP.
Habari njema sana hii kwa wapenda demokrasia.
 
Secretary Pompeo must be joined with Trumph to face charge of inciting supporters storm Capitol DC and couse death to innocent people.
Pompeo get ready for that don't bother with Tanzania, your hands are not clean to point Tanzania's general election.

Sent using Jamii Forums mobile app
ngoja Baiden aingie kesho white house
 
Sijui kama account yake imefutwa,ameifuta imesimamishwa au ameiuza. Wewe niambie imepatwa na nini.

Sijui kama account yake imefutwa,ameifuta imesimamishwa au ameiuza. Wewe niambie imepatwa na nini.
Jibu hilo hapo 👇👇
images (34).jpeg


Sasa nani aliyefanya hivyo ambaye yupo juu ya KATIBA YA US.
 
Ikiwa imebaki siku moja kwa Rais wa Marekani Donald Trump, kumaliza muda wake, Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani, Michael Pompeo (Pichani), amesema Marekani imewawekea vikwazo vya kuingia nchini humo Maafisa wa Serikali ya Tanzania waliohusika katika kuvuruga mchakato wa Kidemokrasia na uvunjwaji wa Haki za binadamu kabla, wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa October 28.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani ambayo hatahivyo haijawataja viongozi hao imesema, serikali ya Marekani inaitaka serikali ya Tanzania kuwachukulia hatua wale wote wanaohusika na matendo hayo.

''Tunaitaka serikali ya Tanzania kuchukua hatua kwa wale wote waliohusika, na hatutasita kuchukua hatua zaidi iwapo tutaona inafaa'' imesema taarifa hiyo.

Serikali ya Marekani imesema kwamba vikwazo hivyo vya kutoingia nchini humo, haviwahusu wale wote walioshiriki mchakato huo wa kidemokrasia kabla, wakati na baada ya uchaguzi mkuu kwa amani na kwa kuheshimu haki za kibinadamu bali, vinawahusu waliohusika kuharibu mchakato huo na kwamba ipo tayari kuendelea kufanya kazi na wanaolinda misingi ya kidemokrasia.

Haya kumekucha Tume ya Uchaguzi na CCM
Screenshot_20210119-213231_Facebook.jpg
 

Uchaguzi Tanzania 2020: Marekani yatangaza vikwazo vya kusafiri dhidi ya maafisa wa Tanzania​

Saa 1 iliyopita
Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Marekani imetangaza kuwawekea vikwazo vya kuingia nchini humo maafisa wa Tanzania ambao nchi hiyo inawatuhumu kwa kile wanachokitaja kuwa kuharibu uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, mwaka 2020.

Maofisa hao wanatajwa kuhusika kuingilia mchakato wa uchaguzi na kuminya utekelezaji wa demokrasia.
Hata hivyo taarifa hiyo ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani haijabainisha ni viongozi gani hasa kutoka Tanzania waliowekewa vikwazo vya kuingia Marekani.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo, Waangalizi wa uchaguzi na mashirika ya kiraia wanadai kuwepo kwa udanganyifu katika uchaguzi huo pamoja na uvunjifu wa haki za binadamu wakati na baada ya uchaguzi.

Marekani inasema kuzimwa ama kuzimika kwa mitandao, kuminywa kwa waandishi wa habari na nguvu kubwa iliyotumiwa na jeshi la Polisi kunafanya uchaguzi huo kutokua huru na wa haki.

Katika uchaguzi huo, baadhi ya wagombea kutoka vyama vya upinzani walienguliwa kwa sababu mbalimbali na wengine kukamatwa.
Tume ya uchaguzi nchini humo na hata Serikali kupitia waziri wake wa mambo ya nje, Palamagamba Kabudi ilieleza kwamba uchaguzi ulikua huru na wa haki.

''Kuna madhara ya kuingilia mchakato wa kidemokrasia. Kuanzia leo tunawawekea vikwazo wale wote walioshiriki katika kuingilia mchakato wa uchaguzi Tanzania...'' ameeleza Waziri Pompeo kupitia ukurasa wake wa twitter.
Ruka Twitter ujumbe, 1
There are consequences for interfering in the democratic process. Starting today, we are imposing visa restrictions on those involved in election interference in Tanzania. We remain committed to working together to advance democracy and mutual prosperity for both our countries.
— Secretary Pompeo (@SecPompeo) January 19, 2021
Mwisho wa Twitter ujumbe, 1
Marekani inasema pamoja na hatua hii iliyochukua dhidi ya maafisa wa Tanzania, inaendelea kufuatilia kwa karibu maendeleo ya hoja hiyo, huku ikisema haitasita kuchukua hatua zaidi dhidi ya wale wanaominya demokrasia na kuvunja haki za binadamu.

''Tunaitaka Tanzania, kuwachukulia hatua wale wote waliohusika kuvuruga uchaguzi, kufanya vurugu na kuleta vitisho'' ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Juhudi za kumpata msemaji wa serikali ya Tanzania kuzungumzia suala hilo mpaka sasa hazijazaa matunda, na tutaendelea kuwatafuta kwa ajili ya kuzungumzia suala hilo.

Haya ni moja ya maamuzi ya mwisho ya utawala wa rais Donald Trump ambaye amebakiza saa chache kuachia mamlaka ya urais. Mpaka sasa haijafahamika iwapo utawala wa rais mpya Joe Biden kama utatekeleza maamuzi hayo. Tayari ofisi ya Biden imetangaza kuwa itatengua sera kadhaa za Trump mara tu baada ya kuingia ofisini kesho.

chanzo: bbc/swahili
 
Tunataka majina yao rasmi wazi. Mabeberu naona hawalali ni Tanzania tu
 
Back
Top Bottom