Marekani kupigana vita na China 2025, Jenerali wa Marekani bw. Mike

Nadhani swala la ukubwa wa bajeti ya wizara ya ulinzi una sababu zake.

Sidhani kama U.S.A ana uwezo wa kusimami zaidi ya tatu zinazo husisha mataifa makubwa licha ya kuwa sipuuzii nguvu zake za kijeshi alizo nazo.
Uchumi wakw unaruhusu
 
Marekani kwa mikwala mbuzi tu hawajambo. Mpiganaji wa kweli hakutangazii lini atakupiga na marekani kamwe hawezi kuanzisha vita na China
 
V.O.A majuzi hapa wametoa doc moja ya kambi za jeshi za kimkakati kule Alaska wanataka kuidominate arctic zone, wanasema wining is not an option! They will fight to win na hakunaga kitu kama kushika nafasi ya pili kwenye vita anasema four star general mmoja.

Kitu walisisitiza ni kuwa marekani inaweza kupigana na nchi ndogo kama north korea lakini kuhusu mrusi na mchina kutakuwa na 'mutual distruction' hivyo wao sio maboya!
 
Kwa hiyo huyu general bwana Mike amefanya kiburi cha kupuuza uwezo nq guvu za China pqsipo kujali madhara ya hiyo vita ikitokea ?
 
sijui kwa kweli kama wanafikiria hili soko la wapiganaji. Msimu wa machungwa hapo tanga mpaka yanozea shambani, tungepeleka tu hata kwa shingi mia mia na sisi tukajitutumua mbele ya jirani zetu.
 
sijui kwa kweli kama wanafikiria hili soko la wapiganaji. Msimu wa machungwa hapo tanga mpaka yanozea shambani, tungepeleka tu hata kwa shingi mia mia na sisi tukajitutumua mbele ya jirani zetu.
Kweli mkuu, tatizo la upungufu wa chakula cha kutosha lina isumbua dunia kwa sasa.
 
Kwanin marekani kila siku yeye anawashwawashwa tu na china kulikoni

Mjinga sana mUSA
 
Kwa hiyo huyu general bwana Mike amefanya kiburi cha kupuuza uwezo nq guvu za China pqsipo kujali madhara ya hiyo vita ikitokea ?
Anamaanisha kuwa ni hatari sana kupigana vita na mchina au mrusi!
 
Marekani imeshapoteza ramani, ule usupa pawa wake unatia sana mashaka. Na mchina amemkalia kooni kwenye maendeleo ya kiuchumi na kitekinolojia. Afrika sasahivi bidhaa zake wanachukua china
Kwahyo kashindwa kupambana kiuchumi,anataka watumie chuma

Yaan hata huwa yakitokea maandamano ya raia lazima mUSA aingilie hasa akisikia raia ya china wananyanyaswa na wana usalama
 
Mkuu hapo kwenye Korean wars. China hataki kabisa Marekani amsogelee zaidi, China anazungukwa na bases za Marekani na washirika wake kina South Korea, Japan na Taiwan kisha anazungukwa na adui wakubwa wa Marekani hao Russia na North Korea. Hivyo China anakuwa karibu na Marekani kwa namna mbili, sasa hataki kuzungukwa kuzidi. Ndio maana kufa na kupona atahakikisha North Korea iko chini ya influence yake, jaribio lolote la kuleta demokrasia ndani ya North Korea ni kuifanya ifunguliwe duniani na kuwa wazi kwa mataifa ya kigeni ikiwemo Marekani. China ndio maana alikomalia North Korea kwenye vita ile, na hata sasa inamsaidia Kim Jong kiusalama, kifedha na kukwepa sanctions ya vitu muhimu. Ikitokea North Korea imepigwa na Marekani majeshi yakakaa hapo kutakuwepo na build up ya Marekani kujipanga dhidi ya Russia na China kwa vile N. Korea ina land border na nchi hizo mbili. China na Russia wako tiyari kulipa gharama yoyote N. Korea ikae hivihivi, waliipotezea South Korea si unaona hakuna land border nao

Urafiki wa Russia na China ni "the enemy of my enemy is my friend" hauna nguvu sana kama tunavyodhani. Kadri siku zinavyoenda Russia anapungua vitu vya kuoffer kwa China. China kafanya reverse engineering na licence production ya silaha za Urusi kamaliza sasa yuko na concepts zake mpya, kashapata kila kitu kwa Urusi kama nuclear program na fighter jet ila kanyimwa jet engine technology ambayo sioni kama atakaa hii miaka mitano bila kuwa sawa na Russia.

Haya mataifa yapo kimaslahi, ukikosa umuhimu unachukuliwa kawaida. Miaka ya 1980s Marekani iliiuzia Black Hawk helicopters China na ikaisaidia kutengeneza J-8 fighter jet hapo Wachina wakiwa na mawazo muda wowote vita na USSR itaanza. Na miaka hii, Russia inaiuzia silaha India wakati huo inaziuza kwa China tena na hao wawili ni maadui. Kinachowaweka pamoja China na Russia ni tishio la Marekani, sio upendo wao. China angalau inataka mshirika anayejiweza ila wale sio kufa na kupona kwamba ukivamia Ukraine nakuunga mkono, China inafanya assessment yake indepently inatafuta maslahi yake.

Na China kugombana na majirani ni sawa na Russia. Ila China kuamua sasa ifanye uvamizi kwa Marekani ni sawa na hakuna, wanagombea nini? Labda iwe preemptive strike.
At the right time China inazo sababu za kuivamia Urusi, haikutokea tu kwamba Urusi ina uwanda wa Siberia mkubwa vile.

Na Marekani ina uwezo wa kubadilisha adui kuwa rafiki ndani ya muda mfupi sana, inavyo vitu vya kuoffer. Na inaweza mfanya rafiki awe adui umuhimu wake ukiisha. Russia iliiuzia Marekani ile Alaska kipindi kile Uingereza na Marekani ni maadui wakubwa
 
Hiyo aliyosema ni fact. Ingekuwa General kasema wajiandae kuivamia Ujerumani hapo kungezua utata mkubwa na Ujerumani ingeshtuka kuona mshirika wetu anawaza kupigana na sisi. Ila sio kwa hao, China bila kuambiwa na yeyote inajua itapigana na Marekani. Hata Wamarekani wangefanya mkutano wa majenerali wote kusema jinsi ambavyo hawatoivamia bado China ingeamini uwezekano wa vita upo. Ni kama Iran inavyodai itaiangamiza Israel, nani hajui pale Israel kwamba Iran inapanga kuwakabili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…