Marekani kupigana vita na China 2025, Jenerali wa Marekani bw. Mike

Tatizo la Taiwan ni eneo dogo. China inaweza ita artillery strike kubwa na naval bombardment ikisaidiwa na air raids to overwhelm Taiwan. Bila msaada wa Marekani wanaweza hold for few days ndio maana nasema maamuzi ya kupindua meza pale ni je Marekani itaingia kati au haiingii. Taiwan always haina confidence 100% kwamba Marekani itakuja no matter what. Marekani inatoa assurance kwamba itasaidia ndio kama ile ziara ya Speaker Pelosi. Na China inabeti maamuzi, Marekani itahusika kweli au itaghairi.

Na muda mzuri wa China kuvamia ni pale Marekani inakuwa occupied na vita nyingine. Mfano ingeingia direct pale Ukraine ikawa ni vita ya ukweli dhidi ya Russia. Wakati huo Israel ikapigana na Iran, ndipo China inaweza tumia nafasi hiyo. Ila China sio wajinga muda Marekani iko iddle eti ndio wavamie Taiwan.
 
Fuatilia ujue Ukraine anatumua silaha kiasi gani kwa siku urudi hapa
Hata kama anatumia Baruti Tani tilioni moja kwa siku ilo kwangu si hoja. Hoja yangu ni kuwa" hizo silaha anazipata kwa kuomba omba". Mara anyimwe, mara asipewe.
Yaani hata we leo ukichukua panga lako ukalipeleka kwa Ubalozi wa Ukraine litapokelewa kwa shukrani kubwa.
 
Marekani imeshapoteza ramani, ule usupa pawa wake unatia sana mashaka. Na mchina amemkalia kooni kwenye maendeleo ya kiuchumi na kitekinolojia. Afrika sasahivi bidhaa zake wanachukua china
Nadhani marekani ameona njia ya kutumia vita ndio njia pekee aliyo nayo ya kumzuia China kwenye uchumi kwake imeonekana kuwa njia ngumu sana.
 
Kwahyo kashindwa kupambana kiuchumi,anataka watumie chuma

Yaan hata huwa yakitokea maandamano ya raia lazima mUSA aingilie hasa akisikia raia ya china wananyanyaswa na wana usalama
U.S.A wapo kutetea kiti chao cha usuperpower wasi pokonywe na China.
 
China hata pigana na rusia kwa miaka 50 ata 60 mbele na ata iyoo miaka 60 ikifika ata kama labda atakuwa ameushika ukiranja wa dunia bado hataweza tna kupigana vita na russia maana ataaribu kila kitu alichonacho lazima tujue china ana migogoro ya kimipaka na karibia nchi zote jirani saivi kaongeza mgogoro wa visiwa vya kusini na nchi zaidi ya tatu tena, Russia hanaga rafiki wa kudumu kila rafiki wa kudumu wote alionawo yuko nawwo sababu wote wanatapata kitu pamoja russia ana kila kitu anachotafuta yeye ni ushawishii na kutanua nguvu zake,

Rusia ni mfupa ulioshindikana kupigana naye vita ni kujitafutia balaa jingine anayetamani kupigana na rusia ni marakani labda na uingereza tu ila wote wanajua dhahama itakayowapata

Sent from my Infinix X571 using JamiiForums mobile app
 
Ni kweli kabisa China hataki kuipoteza North Korea na ndio maana wana mkataba wa kiulinzi walio saini 1961, China na Korea zimepakana.
 
Marekani hawezi thubutu kuingia vitani na China,angekuwa na hizo guts angeshaipiga Iran siku nyingi
Kuna nchi zinajua kukoromea nchi na kuvimbisha kifua lakini wenye mauwezo huzidharau saana!

Hivi ni kweli hata wewe mwenyewe unaamini Irani inaweza kuingia uwanjani na Marekani?

Nchi ambayo ndio kwanza inarutubisha mitambo ya siraha za nyukilia? Wakati mwenzake tangu vita vya kwanza huko anavyo?

Marekani ambayo inazichungulia siraha za Irani kila inapotaka na Irani hawezi kufanya hivyo!

Acha basi mkuu haya mambo!

Uchokozi nchi inaweza kuwa nao! Licha ya uchokozi ukaachwa tuu kwa sababu ukipigwa itakuwa ni kama kudhalilishwa! Nchi zote za kiarabu huwa zinaingiliwa kwa muda wowote na Marekani! Bora ibakie hiyo angalau nyinyi warabu wa madale mjisifu kuwa mko imara kumbe ndo hovyo kabisa
 
Ni kweli urafiki wa China ni wa kimachale sana baina yao licha kuwa watu wengi hawa fahamu ili ugomvi mkubwa baina yao unaanzia kipindi cha unyang'anyi wa ardhi alio fanya Russia toka kwa China jambo lililo mkera sana China na ndio maana miaka ya 1970 mpaka 1971 baada ya mgogoro wao wa mpakani wa mwaka 1969 China alijenga urafiki mkubwa sana na U.S.A jambo lililo pelekea yeye kushinda kiti cha uwakilishi cha UN kutoka ROC/Taiwan urafiki ulipelekea miaka hiyo hiyo ya 70 China kumtupa USSR na kufanya ufunguzi wa nchi kiuchumi kwenda magharibi jambo lililo wafanya watu kusema kuwa China imefanya usaliti wa ujamaa na kufuata Ubepari jambo ambalo halikuwa sahihi bali alifanya usaliti kwa USSR kutokana na ugomvi wao na kwenda na nchi za magharibi ili ajiimarishe zaidi kiuchumi.

Urafiki wao wa kimachale ulifufuka miaka ya 2000s jambo lililo pelekea kuzaliwa kwa hii BRICS iliyo wahusisha Brazil, India,na S.A pia kwa sasa wamekuwa na urafiki zaidi kutokana kwa sasa Russia ana muhitaji China zaidi kutokana na swala la vikwazo alivyo wekewa na mataifa ya magharibi.
 
🤣🤣🤣 Mkolofi wewe kwa mrusi umefikaje?
 
wale muslim wa xianjing....au umesahau
Unafuatilia mambo vizuri!?...Kama wanataka kutumia proxy kwa nini waandae air force yao!?..hao Muslims si wamefungwa kwenye makempu huko china!!
 
Vita ya kirafiki
 
Jielimishe, Iran siyo waarabu,pili Iran ndiyo nchi yenye makombora mengi ya Masafa marefu,na si kwa bahati mbaya,lengo ni hao wachokozi wakianzisha zogo basi nyumbani kwao Nako kuwake moto,pili Kambi za marekani Arabian peninsula hazitokua salama,Iran alidungua drone ya marekani aliyodai ni stealth,Iran angekuwa bwege Kama unavyodhani basi Israel angeshaingia akisaidiwa na ma Wana zake.....mwisho ni silaha na si siraha,jifunze kuandika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…