Marekani kupigana vita na China 2025, Jenerali wa Marekani bw. Mike

Marekani kupigana vita na China 2025, Jenerali wa Marekani bw. Mike

Kuna nchi zinajua kukoromea nchi na kuvimbisha kifua lakini wenye mauwezo huzidharau saana!

Hivi ni kweli hata wewe mwenyewe unaamini Irani inaweza kuingia uwanjani na Marekani?

Nchi ambayo ndio kwanza inarutubisha mitambo ya siraha za nyukilia? Wakati mwenzake tangu vita vya kwanza huko anavyo?

Marekani ambayo inazichungulia siraha za Irani kila inapotaka na Irani hawezi kufanya hivyo!

Acha basi mkuu haya mambo!

Uchokozi nchi inaweza kuwa nao! Licha ya uchokozi ukaachwa tuu kwa sababu ukipigwa itakuwa ni kama kudhalilishwa! Nchi zote za kiarabu huwa zinaingiliwa kwa muda wowote na Marekani! Bora ibakie hiyo angalau nyinyi warabu wa madale mjisifu kuwa mko imara kumbe ndo hovyo kabisa
Acha kukalili vita sio kitu rahisi kama unavyo fikiri?
Marekani akijaga kujichanganya kuivamia Iran atakumbana na aibu ya karne.
 
General hajaambia waandishi wa habari wala hajayasema maneno yale in public. Kulingana na elimu yake, uzoefu, cheo na intelligence anayoweza access amefanya prediction muda wa vita ya Marekani na China ni 2025 na hapo ndio akaandika memo kwenda kwa maofisa. Alichokifanya ni kazi yake, kawaambia wanajeshi ambayo ndio kazi yao hiyo kukaa chonjo dhidi ya adui.

Hayo yangesemwa na Defence Secretary kwenye press conference ndio ungekuwa utata. Na uzuri wa US kuna uhuru wa habari hata memo ya siri inavuja na watu wanahoji au kuripoti. Hata China na Russia wanafanya assesment vizuri na kutoa mapendekezo ila hayatajwi hadharani.
Sio suala la kuiogofya China hili. Sio classified materials zile, memo ya mawazo ya mtu.

Na hiyo Taiwan haivamiwi kirahisi kama watu tunavyofikiria. Nchi inayotengeneza 40% ya microchips duniani sio ya kizembe na akili zao hazijalala hivyo na udogo wake. Na imezungukwa na maji, unahitaji one of the biggest naval landing operation kuwavamia fukwe zao zile na kusalimika anti ship missiles zao kwa kiasi fulani, sacrifice ya asilimia kadhaa ya kikosi cha kuvamia. Taiwan sio nchi ya China kupanga leo na ikavamia siku tatu zijazo, inahitaji wiki za maandalizi ambazo surveillance itaonyesha maandalizi hayo na Marekani itahamisha Pacific fleet kuja kazini (probability ni kubwa Marekani kuingilia kati)

Ili Marekani ichelewe kuingia Taiwan inabidi China iwe na navy kubwa kuliko sasa jambo ambalo wanakuja kasi, ila iwe na logistics nzuri zaidi. Pia Marekani ikomae kwenye microchips industry ijitosheleze ili isiogope source ya Taiwan kupotea. Yakitokea hayo mawili China inaweza vamia haraka ikapigana siku chache na kuingia Taiwan kukutana na resistance ya army kisha Marekani ikachelewa kurespond baadae ikaona haina haja sana kupigana na China (kama umuhimu wa Taiwan kwake umepungua). Hii scenario inategemeana ila inategemea ubeti kitu kimoja muhimu, response ya Marekani.

Ni maoni yangu
Mkuu hiyo bongo yako ipo vizuri sana👏👏
 
China hata pigana na rusia kwa miaka 50 ata 60 mbele na ata iyoo miaka 60 ikifika ata kama labda atakuwa ameushika ukiranja wa dunia bado hataweza tna kupigana vita na russia maana ataaribu kila kitu alichonacho lazima tujue china ana migogoro ya kimipaka na karibia nchi zote jirani saivi kaongeza mgogoro wa visiwa vya kusini na nchi zaidi ya tatu tena, Russia hanaga rafiki wa kudumu kila rafiki wa kudumu wote alionawo yuko nawwo sababu wote wanatapata kitu pamoja russia ana kila kitu anachotafuta yeye ni ushawishii na kutanua nguvu zake,

Rusia ni mfupa ulioshindikana kupigana naye vita ni kujitafutia balaa jingine anayetamani kupigana na rusia ni marakani labda na uingereza tu ila wote wanajua dhahama itakayowapata

Sent from my Infinix X571 using JamiiForums mobile app
Uingereza hana ndoto ya kupigana na Russia kabisa. Marekani hana haja wala nia ya kufanya uvamizi kwa Russia, anazo njia za kumdhibiti Russia mbona USSR ilivunjika bila risasi hata moja kurushwa. USSR ilikuwa tishio kuzidi Russia hii, na walifika hatua hatarishi mara nyingi kupigana ila haikutokea.

Ili Russia ipigane na Marekani inabidi ianze yenyewe, sio ichokozwe. Hakuna kitu ambacho Marekani inaidai Russia wala hakuna tishio lolote Russia inaleta kama haitovamia. Wakati huo, China ina kitu inaidai Russia na ni ya muhimu kwake kuliko Russia ilivyo muhimu kwa China
ChinaRussiaTradeUnequals_v5.jpg


Data zote zinaonesha China ni muhimu kwa Russia kuliko kinyume chake. Kwahiyo usiseme Russia ina kila kitu
2-Figure1-1.png
 
Unazungumzia Urus hii hii inayopigana na ukraine mwaka mzima kwa silaha za kuomba omba kutoka kwa nchi za Ulaya na marekani ama kuna Urusi nyingine nje na hii?.
Ukraine ni uwanja wa mapambano tu, wanaopambana ni US na washirika wake nchi 30+ kupambana na jabali moja.
 
Kinachoendelea kwenye uwanja wa mapambano kipo wazi na hakihitaji ujuzi wala ubobezi wa masuala ya kivita.
Kinachondelea kila kitu kipo wazi kwa mujibu wa nini?.
Unajua bomu lililorushwa ndani ya dakika tano zilizopita ndani ya UKRAINE?.
Unataka kusema-: vita hii ya Ukraine ndiyo vita ambayo kila kitu kinawekwa wazi na kila upande?.
Secret,tacts na strategie vyote vipo wazi katika hii vita? Kweli?.
 
Marekani hawezi thubutu kuingia vitani na China,angekuwa na hizo guts angeshaipiga Iran siku nyingi
Kwanini Marekani iipige Iran
Kwa nini iiwekee vikwazo na kutaka kukagua silaha zake Kama Iraq ya Saddam Hussein!?
Vikwazo ni kwa sababu Iran inatumia silaha hizo kuwapatia Hezbollah, Hamas na jihadists wengine.

Kwanini unataka Marekani iipige Marekani
 
Kwanini Marekani iipige Iran

Vikwazo ni kwa sababu Iran inatumia silaha hizo kuwapatia Hezbollah, Hamas na jihadists wengine.

Kwanini unataka Marekani iipige Marekani
Vikwazo Iran imewekewa lini na hizbullah imeanzishwa lini!?..
 
Huwezi elewa kwa vile umejifungia akili. USSR na China waligombea mipaka miaka ya 1960s mwishoni hadi vifaru vilihusika na watu walikufa kwenye mapigano ya rasharasha kwa miezi zaidi ya mitano. Baadaye ndio wakasaini ceasefire na kurudia mipaka ya zamani, walikuja kusaini makubaliano kumalizana na madai 2008 au 2009 kama sikosei.

Wakati China ikiwa weak enzi za dynasties kina Qing na Ming na wengine pale Russia ilichukua maeneo kadhaa na ilikiuka mikataba ya mipaka. Miaka mingine maeneo yalichukuliwa, mji wa Vladivostok pale Russia ni eneo la China lile. Waulize Wachina wakwambie Outer Manchuria ni nini, eneo lote la Russia lililoibiwa kutoka China wanaita hivyo.

Mapigano kati ya Russia/USSR na China yametokea kwenye mipaka yao ila mapigano kati ya Marekani na China hayajatokea kwenye mipaka. Kwenye WW2 Marekani ilifanya airlifting campaign "The Hump" kuipa silaha China ipigane na Japan. Zilipitia India na kuvuka nyanda za milima mikali kukwepa eneo la Manchuria lililokaliwa na Japan.

China na Marekani ni wagomvi kimaslahi na kuishawishi, ila China na Russia ni mgogoro wa mipaka ambao ni frozen na mgogoro wa mipaka huwa haufi kirahisi. Ugomvi wa China na Marekani ni baada ya WW2, ila China na Russia wana fujo zao since 1800s uko.
Duh sio mchezo...... Dunia itatawaliwa na vita siku zote kama ndio ivo...... Ni swala la muda
 
Back
Top Bottom