Marekani na Israel ni mataifa tofauti yenye baadhi ya siri za pamoja, bila kulijua hilo, Iran au yeyote dhidi yao, ni mfu atembeaye!

Tusubiri mkuu; muda ni mwalimu mzuri. Napata sana tabu kumuamini Russia kwenye case ya Iran (mjadara ungejikita kwenye jicho la kiitelenjensia badala ya mambo ya imani/dini ungekua mzuri sana ). Russia ni moja ya mataifa yanachukia sana mambo ya ugaidi, Iran ndio mfadhiri wa makundi mengi ya kigaidi duniani so hu urafiki wao hasa against Israeli ukweli napata nao shida sana kuuelewa, I'm sure watasaritiana huko mbele. Kuna uzi humu unasema, Netanyahu anamtafuta Putin waongee, hope hawa 2 sio mara yao ya kwanza kuongea, hawa ni marafiki, sema ugomvi wa USA na Russia ndio umesababisha Russia kua na urafiki wa mashaka na Iran ambao to me, hu ni urafiki wa muda.

Coming back to the thread; nakubaliana na mleta uzi, Israeli na USA ni mapacha on both intelligence, military and economically, nitafafanua baadhi ya hayo kwa mtazamo wangu. Kwenye issues za intelligence, Mosaid na USA inaonekana ni watu wanao badirishana sana taarifa, we all knows what happened on September 11, 2001; Mosaid walinusa hatari na wakalikisha information kwa CIA, CIA waka ignore but same Mosaid wakawalinda watu wao na hakuna aliyekufa pale World trade center building, ukisoma jinsi CIA walivomkamata na kumuua Osama Bin Laden, Mossaid wameshirikiana kwa kiasi kikubwa mno na CIA, these guys ni mapacha. Njoo kwenye vile vifaa vya mawasiliano vilivo lipuka vyenyewe na kuua viongozi na watendaji wengi wa Hezbollah, yasemekana hata rais Rais wa Iran nae aliuliwa kwa style hiyo hiyo but who invested to China on that technology? Is USA. Again, watazame matajiri wengi wa USA utagundua wana vinasaba vya Kiyahudi, this is why hata Steve Jobs mgunduzi mkubwa aliye leta mapinduzi kwenye sekta ya mawasiliano ilitakiwa atangulizwe mbele za haki, hakua mzungu, hakua Myahudi. Yale yale ya kina Magic Johnson, R. Kelly nk. Well, swali linabaki, hu mziki Iran atauweza? Let's wait and see
 
Mkongwe, ukifanya hivi na mimi itabidi nije na screenshot inayoonesha wanachokisema Persians kuwa nini watafanya Israel ikileta ubwege.

Hii ni kawaida tu, wote hawa wanachimbana mkwara.

Mkuu hoja yangu si screenshot; uliyaona haya?

"Ya kwamba watakusaka pamoja kukuondoa wao duniani bila kujali muda wala gharama. Ya kuwa kwenye hilo tangia mataifa yao yamekuwapo kwenye hilo hawajawahi kushindwa!

Yale yale ya akina Osama bin Laden, Mula Omari, General Farrah Aideed, Saddam Hussein, Muamar Gaddafi nk."

Mkuu huo ni ukweli labda unionyeshe walipowahi kuacha target yao.

Uliiiangalia ikiwamo reference ya "operation plasma" na al-Mabhouh Dubai?
 
Wewe ni mtu ambaye huamini ktk mabadiliko.. Bwana mdogo amini usiamini mambo hubadilika. Kukalili na kutojiamini ni ujinga kama ujinga mwingine

Mabadiliko ndiyo kitu gani ndugu? Kukariri au huko kutojiamini unakuona wapi?

Uliyaona haya kwenye mada?

"Kwa sababu mataifa wawili hawa kwenye haya ya kutishiana nyau ni wamoja, ziko namna mbili tu za kushughulika nao kwa mafanikio:

1. Kusalimu amri kama UAE na Saudi Arabia yaishe kama unataka kuishi. Au:

2. Kupambana nao relentlessly bila pause ukafe mkipigana kama ni nia yako japo kuwagawia nao maumivu ya kutosha kwa kadri iwezekanavyo.
"

Tafadhali fafanua isije kuwa kama manyani, mjinga kumbe ukawa wewe.
 
Madhara ya kutohudhuria Masjid na kuacha kufanya swala ndiyo haya, unajikuta unaiona dunia katika uhalisia wake ma kuuongea ukweli kama ulivyo ingawa ni mchungu.
🤣🤣🤣🤣

We jamaa, itabidi unilipe aisee

Si kwa kuumiza mbavu zangi kihivi chief
 
Sio siri za pamoja bali Israel ni mojawapo ya kambi kubwa zaidi ya kijeshi ya umoja wa kijihami wa nchi za magharibi/NATO.

NATO inahusisha nchi nyingi sana.

Kwenye mada ni siri (yamini) ya nchi mbili tu.

NATO? Humo hata Uturuki, Poland, Hungary, nk huko, wamo ndugu?
 
Amuka utajikojolea maana uko unaota
 

Nguvu unazozisema ni za Marekani kwenye yamini hii isiyotenguliwa ya kuwasaka wabaya wao kokote waliko.

Kumbuka mataifa hayo ni tofauti yenye yamini moja dhidi ya watishia nyau wao popote walipo.

Atatoboa nani hapo?
 
naona umeandika kiushabiki sana..kwanza tofautisha kati ya kushambulia nchi iliyokamilika kijeshi na vifaa vyoye kivita kama alivyonavyo Israel na US basi na Iran pia anavyo ipo tofauti kubwa kupigana vita na nchi kamili na vikundi vya wana mgambo kina Hezbollah,IS,Ouath, na Hamas hivi ni vikundi vya wahuni tu ni sawa na kina Alshabab,M23 na Bokoharam wa huku afrika..hapo Israel anajizolea point na misifa kibao ila kwa Iran hiyo ni piga nikupige sababu wanakaribiana kiuwezo pia Iran ana uwezo wa kupaharibu Israel kama ambavyo yeye anafanya huko gaza na lebanon..
 

Ulichosema ni kweli kabisa ila.. watu wataleta udini na utapingwa.. kwa Iran ukisoma between the lines unajua kabisa anatumia Udini kuplay victim
hana nia dhabiti ya kuwapa Nchi palestina

Ukiangalia charter ya hamas unajua kabisa ni kikundi kilichotengenezwa nje ya Palestina kwa lengo maalum


Hayo hapo juu ni moja ya maneno kwenye charter yao.. hivi unategemea Kama wewe. Ndo israel halafu jiran yako kwenye miongoz yake na malengo ni kuhakikisha anakufuta kwenye ulimwengu utafanyaje

Iran alitaka ku destabilize Egypt kupitia muslim brotherhood, baada Eygpty kuwastukia na kuwatimua wakaenda palestina na kugeuka hamas na ndo maana hata palestina iligawanyika ile ya west bank haikuwa chini ya hamas

Hatukatai hata western wanatengenza proxy nje ya nchi zao ila utofaut US na Europe wanazilinda proxy zao kwa gharama zozote..

Tumeshuhudia Mara kibao US akiingiza jeshi kwa mgongo wa UN na NATO kwenda kulinda proxy zake.. ila
Iran anatoa Silaha kama ulivyosema

kama aliamua kukinukisha pale israel alivyovamia Gaza kujibu shambulio la 7th Oct basi nae angepeleka jeshi palestina akatanga vita na Israel

Angalia Urusi alivyosaidia kwa hali na mali Syria.. ameweka. Had kambi na "state of the Art" facilty kumlinda proxy wake Saad

.. iran anajua marekan na Israel wanamtafuta miaka mingi alishasoma alama za nyakati kwa saddam, Libya na almanusura ya Yule wa Syria ambaye nayo imekuwa "stalemate" maana wakubwa wawili wako pale..

Utawala wa ayatollaah iran wanajua kuwa tokea wachukue nchi kwa mapinduz na kuiondoa pro Western Govt maana yaake "They will always keep looking over their shoulders"sasa kuhakikisha wana wakeep busy marekan na wenzie ndio wakaamua kutengenza proxies za lebanon, yemen na palestina..
ni strategy nzuri maana dunia ya sasa aidha tunisha msuli au kuwa chawa.. hakuna neutrality .. neutrality bila nguvu ni bure

Lakini mkakati wao wa mihemuko ya udini hapo ndo wanafeli.. kama nia ya dhat kuwapa nchi palestinians au kupeleka warning kwa western allies kuwa " two can play this game" wasingesukumiza palestina wafanye shambulio ya Oct kisha wao wakapiga kimya

Ningekuwa ndio Iran govt ambacho ningefanya ningemleta kiduku karibu, urusi, turkey na wengine ant western huku tayar nina puppet kwenyw failes state kama yemen na lebanon nina mecernaries kibao.. kisha tukatengeneza " pact" kama ya NATO tukalishana yamin kuwa akivamiwa mmoja tunaingia wote tukatengeneza base za hiyo "pact" kwenye nchi zetu

Kisha nawambia palestina walianzishe israel akijibu natangaza vita kwa kigezo cha kulinda marginalized ppl same playbook anayotumia US.. hapo lazima kuwe na "stalemate" kama ile ya syria

Maana mzani utabalance.. US na watu kwe sie na watu wetu wote tuna "nuke" kisha kuna kundi la 3 ambao wako neutral.. tukiitwa mezan nasema haina shida palestina wapewe utaifa watu waishi kwa aman kisha naweka puppet gov pale palestina..
 
Samahani wakuu, nje ya mada.
Hivi Marekani kule Afghanistan alikimbia au alikabidhi nchi Kwa magaidi ya Taliban.

Nadhani umeshajibiwa bila kumsahau General Aideed kule Somalia.
 
Nadhani hapa tunapishana sehemu ndogo sana mkongwe!
Ndani ya Iran kuna Mazayuni zaidi ya 1000, Israel hashindwi kufanya uhuni wake kwa kuwatumia MOSSAD, ameshafanya sana, na bado ataendelea kufanya, kwasababu mazingira yanamruhusu.

Mimi nazungumzia mashambulizi ya moja kwa moja, yaani kama hiki ambacho Israel inakifanya kwasasa hapo Lebanon, hiki ni kitu ambacho Israel hana uthubutu wa kukifanya kwa Iran.

Mtoa mada amesema kilichowakuta Hamas na Hezbollah ndicho kitakachowakuta Iran, mimi nalikataa hili. Iran ni taifa kubwa sana kijeshi hapo Middle East, kwenye upande wa manpower mpaka military infrastructures sio rahisi kuwatia ulemavu kama Hezbollah na Hamas.

Nikukumbushe tu, hii sio mara ya kwanza Iran kuishambulia Israel na Marekani, ameshapiga kambi za Marekani pale Iraq, miezi kadhaa iliyopita amerusha mvua ya mabomu kuishambulia Israel na mwanzoni mwa mwezi Oktoba amezishambulia kambi za jeshi za Israel kwa missiles na hili shambulio la mwisho limethibitisha kuwa Iran ina uwezo wa kupiga popote ndani ya Israel, Iron dome,David's Sling na ushubwada gani sijui, vyote ni njiwa tu mbele ya mwewe linapokuja suala la kuzuia Iran hypersonic missiles.

Hilo shambulio la mwisho ni ujumbe tosha kwa Marekani na Israel, kama Israel itaishambulia Iran, hakuna sehemu itabaki salama ndani ya Israel, pia Iran imeshasema kuwa next time watashambulia miundo mbinu, sio maeneo ya kijeshi tena.

Kwahiyo Israel na mpambe wake Marekani chaguo ni lao, wana option mbili tu, moja kujificha nyuma ya operesheni zao za kiuwoga kupitia CIA na MOSSAD (ni za kiuwoga kwasababu hawatangazi kuwa ni wao wamefanya, wakiulizwa wanaruka kimanga, huu ni uwoga), pili kuingia mazima na kuishambulia Iran kwa kutumia mavyuma yao tofauti tofauti waliyokuwa nayo. Wote tunajua option gani watachagua, na ndio option ambayo wamekuwa wakienda nayo miaka yote dhidi ya Iran, tukiachana na ile option ya vikwazo ambayo sasa imekuwa kama kumpigia mbuzi kinanda kwa mataifa yanayojitambua.
 
Putin is well and alive!
Au hafit your scenario?

Mkuu ulipaona hapa:

"Ya kwamba watakusaka pamoja kukuondoa wao duniani bila kujali muda wala gharama. Ya kuwa kwenye hilo tangia mataifa yao yamekuwapo kwenye hilo hawajawahi kushindwa!"

Operation Plasma, al-Mabhouh alisakwa kwa karibu miaka 30.

Tofautisha Putin a nuclear power au hata China.

Unadhani kwa nini hawataki Iran awe na nuclear capability au hawa North Korea, India na Pakistani wanakwenda nao pole pole?
 

Mkongwe, kumuua Ayatollah kwa kutumia dark arts sio ushindi kwa Israel dhidi ya Iran, sijui tunakubaliana katika hili?
 
Ulichosema ni kweli kabisa ila.. watu wataleta udini na utapingwa..
Ulivyoanza na hizi mbanga, tayari inaonesha na wewe una udini ndani yako, kwahiyo post yako yote iko biased. Hoja yoyote ya kumpinga mtoa mada kwako haitofaa kwasababu tu inaendana na unachokiamini.
 
Ni ukweli usio pingika kwamba Wayahudi ni watu werevu sana, na inasemekana uchumi wa Marekani kwa asilimia kubwa unaendeshwa na hawa watu. Lakini tunasahau kwamba msaada mkubwa wa kijeshi tena wa wazi ( dola bilions of money) anaupata kutoka Marekani, Israel hapambani na nchi bali anapambana na vikundi vya wanaharakati ambavyo vinamsaada kiduchu tena usio wa halali/ wakificho wa silaha kutoka kwa washirika wao, laiti kama hao anaopigana nao wangekuwa na access za facilities kama za kwake tungekuwa tunaongea mengine, huo ndio msingi wa nguvu aliyonao Israel, ila ukweli ni kwamba Israel hawezi kuivamia Iran kama tunavyodhani, Iran ni nchi sio kikundi cha wanaharakati kama hao wengine anaowapiga hovyo. Israel kapoteza maisha ya watu wengi huko Gaza, watoto, wanawake, wazee karibia elfu sijui arobaiini na ngapi huko. Israel hii ni ya wahuni sio watu wa Mungu kama tunavyoaminishwa. Kipindi kile Iran ikiwa chini ya utawala wa Rais Mahmoud Ahmadinejad nilijuwa kita waka, chokochoko zilikuwa nyingi lakini ilipita, ni kwa sababu Israel hawezi kuwa under estimate Iran hata siku moja nguvu yao ya kijeshi anaijua na pia hata wao ni werevu sana.

 
Hakuna “siri”. Nguvu kubwa ya kiuchumi, kijeshi na kiteknolojia inayofanya kazi Marekani na Israel iko Marekani. SWALI LA MSINGI ni ukaribu mkubwa wa mataifa hayo msingi wake ni nini?

Tafuta kujua “jamii” zenye nguvu kubwa ya kisiasa kwenye nchi hizo ni zipi? Kumbuka, nchi mbili hizo ni nchi za kidemokrasia. Katika mambo ambayo anayetaka kuongoza USA lazima ayaweke mbele kabisa ya ajenda zake ni usalama na ustawi wa Israel.

Asipokuwa tayari kwa hilo basi hana budi kuachana na siasa za Marekani kwani hatafika popote. Jiulize Netanyahu anapata wapi jeuri ya kumpuuza Rais wa USA nyakati fulani fulani? Hakuna siri hapo.
 
Kuna wakti kaka Juma (J) akili zina kukaa sawia kuna wakt pia zina hama leo ume zungumza ukweli mchungu apo Sheikh ubwabwa bwana Malaria 2 au Webabu Ritz Hawa wezi kubali ili suala
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…