- Thread starter
-
- #61
Nimekuelewa.
Hiyo ni hatua jema.
Haniyeh wa Hamas, Nasrallah wa Hezbollah. Hawa wote ni wadogo sana kulinganisha na Israel, tumekuwa tukiwasapoti kwa chuki zetu tu dhidi ya ubabe wa Israel na USA.
Haipo shaka kuwa hapa pia tuko pamoja.
Atabondwaje, unamaanisha kupitia covert operations za CIA na MOSSAD?
Ili tuelewane vyema naomba unielekeze anabondwaje!
Iran ameshalipua kambi za jeshi za Marekani hapo middle east na bado Marekani hakumbonda, kwanini iwe sasa? Alikuwa anasubiri waungane na Israel kumpiga kwa pamoja? Unamaanisha Marekani peke yake hamuwezi Iran? Au unamaanisha Marekani ana uchungu zaidi na Israel kuliko taifa lake?
Mkuu kumbuka Marekani hambondi mtu wazi wazi kwa kuchelea kujiingiza wa saizi yake (Russia au China).
Tambua kwa hii dunia ni wawili hao asioweza kujifanyia lolote atakalo. Wengine wote, ukweli mchungu hayupo mmoja popote anayeweza kuhimili.
Kwamba atafanya je? Si ulisikia kifo ni kifo? Hiyo mbona si kesi? Kwamba CIA, Mossad, nk? Kwani inajali nini? Si wanasema "the end justifies the means."
Marekani anaijua Iran vilivyo tokea angani na amekuwa na wakaguzi physically na cameras zake installed kibabe ndani ya Iran.
Tofauti ya hapa na huko ulikosema atampiga Iran sasa vilivyo, Israel kama proxy tu! Si china wala Russia wataingilia kwa njia hii.
Ndio, vita ni gharama mzee!
Kila taifa linajaribu kuepuka vita kadri inavyowezekana.
Mkuu hawa jamaa wawili kwa yamini yao, kwao muda au gharama si hoja:
"Ukimwua au kujaribu kumwua mwisrael au mmarekani au ukiyatishia mataifa yao au watu wao popote; tokea muda huo, tambua wewe ni mfu unayetembea, na watakuondoa."
Wasiwasi wako tu mkongwe!
Shida ni kwamba uliwekeza matumaini makubwa sana kwa Hezbollah, hiki kichapo wanachokula Hezbollah kinakufanya ujiulize maswali mengi, ni kawaida.
Ila ni vyema kujua, mtindo uliotumika kumpiga Hezbollah na Hamas hauwezi kufanya kazi kwa Iran.
Mkuu niliyoandika, umekuwa ndiyo msimamo wangu wa siku zote.
Hakuna cha kufanya hapo na kipigo anachopata Lebanon au Palestina ambapo kwa uhakika ninaumia na wapongeza mno wote wanaowaunga mkono:
Iran, Hezbollah na wenzao mfano mzuri wa upendo wa Yesu Kristo aliyetufia msalabani
Zingatia haya hayako na chembe ya woga wala kukata tamaa kokote:
"Kwa sababu mataifa wawili hawa kwenye haya ya kutishiana nyau ni wamoja, ziko namna mbili tu za kushughulika nao kwa mafanikio:
1. Kusalimu amri kama UAE na Saudi Arabia yaishe kama unataka kuishi. Au:
2. Kupambana nao relentlessly bila pause ukafe mkipigana kama ni nia yako japo kuwagawia nao maumivu ya kutosha kwa kadri iwezekanavyo.
Lione neno "mafanikio" kwenye bold pale kwa maana yake.
Sina hakika ni wapi unasoma wasiwasi wowote kwangu.
"Tofautisha machungu dhidi ya udhwalimu na bazazi, na kuusema ukweli hata kama unauma!"