Marekani na Israel ni mataifa tofauti yenye baadhi ya siri za pamoja, bila kulijua hilo, Iran au yeyote dhidi yao, ni mfu atembeaye!

Ni kweli marekani anapambana na hayo makundi kwa jina la Israel.

Ndiyo maana kufanikiwa kupata malengo yako:

"Surrender ili uishi au pigana hadi kufa bila kukoma ili u inflict maximum pain."

Hakuna option nyingine.
 

Tofautisha NATO au Marekani dhidi ya Russia na Marekani dhidi ya Iran, Israel ikiwa proxy.
 
Sasa mbona kwa mungu hawajalejea au mungu wao na wa kwenu nitofauti maana nyinyi mungu wenu yesu a.k.a ISSA lakini wao hawamtambui wanamchukulia
 
mkuu yeyote anayepigana na israel au U.S.A anawajua vizuri kuliko ulichoandika wewe hapa ila tu hao jamaa(hezbollah,hamas,iran n.k) sio waoga km wewe linapokuja swala la kupigania maslahi yao yaani wewe huijui israel na U.S.A zaidi wajuavyo ila bado mapigano yataendelea mpk mwisho wa dunia kwasababu hizi mbinge hazijaanza leo
 

1. Ni kweli kinachowala uliowataja kipo huko kwao na siyo miye, wewe wala awaye yote anayeweza kusimulia hilo vizuri kuliko wao.

2. Aghalabu mada nzima na nilipoandika hakuna popote nilipojaribu kuyasimulia hayo wala hata kuwa na nia hiyo.

3. Zaidi sana, sina hakika woga wangu ulioandika hapa unausoma wapi?
 
Toka ndani ya mfuko wa sandarusi.Iran hapambani na Israel. Anapambana na kundi la magangwe wa dunia.
 

Mkuu umeandika vyema.

Russia hana appetite yoyote kuelekea Iran, Palestina au Lebanon hasa ikizingatiwa kwa sasa ana yake ya kumtosha tu huko Ukraine.

Hakuna popote alipotoa hata tamko la maana, zaidi ya ku "urge restraint and de-escalation" ambako kila mwingine anafanya.

Haipo siri kuwa amekuwa akitafutwa Iran muda wote. Kisa na mkasa ile nuclear program ambayo inatakiwa kuwa crippled kama kwa yaliyomkuta Saddam.

Hapa amesakwa Iran hadi amepatikana na ni suala la muda kidogo tu sasa.

Kwamba anasubiri apigwe kwanza?!

"Ninadhani litakuwa pigo takatifu ambalo na ataujitia mno muda huu wa sasa alipokuwa akiweza kujitutumua, kutoutumia ipasavyo."

Ama hakika kwa vile kukubali yaishe haikuwa uchaguzi wake, heri angechagua kufa akipigana "in hot pursuit" ambapo angewapa angalau maumivu ya kutosha akiwa na nguvu.
 
Mkuu bado mateka wameshikiliwa na Hamas!

Mkuu Gaza umeiona ilivyo?

Israel anatafuta confirmation tu hapo, kuwa Sinwar is eliminated. Kisha utasikia kakubali ceasefire.

Hakuna mateka wazima hapo, wala hao bi Nyau si kipaumbele.
 

1. Kama haya umeandika hivi kuhusiana na mada hii, utakuwa uko nje kabisa ya mada. Iko kwenye mada:

"Hili si suala la ushabiki wala kiimani."

2. Mada inaongelea mataifa mawili ambayo nyuma ya pazia Kuna uwezekano mkubwa wana makubaliano ya siri dhidi ya mahasimu wao.

3. Hapo #2 zingatia mahasimu hao ni hawa:

"Ukimwua au kujaribu kumwua mwisrael au mmarekani au ukiyatishia mataifa yao au watu wao popote; tokea muda huo, tambua wewe ni mfu unayetembea, na watakuondoa."

4. Ukifuatilia kesi mbali, hasimu wao akiingia kwenye anga zao, hiyo ndiyo hatima yake.

5. Iko kwenye rekodi kuwa kuwa hawajawahi kushindwa na huu ni mfano wake:

Yale yale ya akina Osama bin Laden, Mula Omari, General Farrah Aideed, Saddam Hussein, Muamar Gaddafi nk.

6. Ni wazi kuwa Israel peke yake isingekuwa taabu sana kwa Iran:

Palestina ni wahanga, Iran na Israel hawachekani, ila Marekani wapewe maua yao

7. Sasa Marekani ndani wewe options hudhani ni hizi zina thamani?

"Kwa sababu mataifa wawili hawa kwenye haya ya kutishiana nyau ni wamoja, ziko namna mbili tu za kushughulika nao kwa mafanikio:

1. Kusalimu amri kama UAE, Saudi Arabia nk yaishe kama unataka kuishi. Au:

2. Kupambana nao relentlessly bila pause ukafe mkipigana, kama ni nia yako japo kuwagawia nao maumivu ya kutosha kwa kadri iwezekanavyo."


8. Au wewe unadhani kina options gani zaidi ndugu mjumbe?
 
Kukariri ni kuamini kwamba Isreal na USA hatatakuja kushindwa. Dogo ktk hii dunia hakuna kitu kisichowezekana
 
Kukariri ni kuamini kwamba Isreal na USA hatatakuja kushindwa. Dogo ktk hii dunia hakuna kitu kisichowezekana

Wapi niliposema hayo ya kuwa hatakuja kushindwa?

Huoni ni katika kukariri kwako kunakokufanya kudhani nimesema hivyo, na hata kufikia kuniita dogo labda kwa kuwa wewe ndiye?

Zingatia : Madogo mabandiko yenu, paragraph 1!
 
Wapi niliposema hayo ya kuwa hatakuja kushindwa?

Huoni ni katika kukariri kwako kunakokufanya kudhani nimesema hivyo, na hata kufikia kuniita dogo labda kwa kuwa wewe ndiye?

Zingatia : Madogo mabandiko yenu, paragraph 1!
🀣🀣🀣 Dogo bandiko lako lilikusudia kutoa ujumbe gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…