Marekani na Israel ni mataifa tofauti yenye baadhi ya siri za pamoja, bila kulijua hilo, Iran au yeyote dhidi yao, ni mfu atembeaye!

Marekani na Israel ni mataifa tofauti yenye baadhi ya siri za pamoja, bila kulijua hilo, Iran au yeyote dhidi yao, ni mfu atembeaye!

Ni kweli marekani anapambana na hayo makundi kwa jina la Israel.

Ndiyo maana kufanikiwa kupata malengo yako:

"Surrender ili uishi au pigana hadi kufa bila kukoma ili u inflict maximum pain."

Hakuna option nyingine.
 
😂😂😂😂
Hivi karibuni NATO walikuwa wanaangalia uwezekano wa kumruhusu Ukraine kutumia silaha za NATO kushambulia ndani ya Russia, nadhani unajua Russia amejibu nini!

Kwanini Russia isifanye inachotaka kufanya sasa kabla ya kusubiri Ukraine apate kibali cha kuishambulia Kremlin?

Pia, NATO wamekuwa wakitoa misaada ya kijeshi kwa Ukraine, military bases za NATO hapo Ulaya zinajulikana, kwanini Russia asiingie tu mazima kupigania survival yake?
Maana nia ya NATO ni kuidhoofisha Russia kadiri inavyowezekana, na Russia analijua hili?
Kwanini Russia asitangaze vita moja kwa moja na NATO?

Tofautisha NATO au Marekani dhidi ya Russia na Marekani dhidi ya Iran, Israel ikiwa proxy.
 
Mpaka sasa Israel bado ni Taifa lenye ngugu sana na hasa kiteknolojia, ogopa sana watu wako million 9 ambao ni wananchi pamoja na Jeshi humo humo lakini wana nguvu sawa na China,Russia,America pia,..Teknolojia kubwa za kivita na hata Satellite ni ujuzi wa kwao,japo Satellite iko America lakini wao ndo Controls.

Miaka kama 70 iliyopita kama sikosei,walivamiwa na majeshi matatu ya Syri,Jordan na Egypt na waliyashinda wakiwa watu laki 6 tu nchi nzima kwa maana ya Raia na Jeshi kwa ujumla

Tukirudi kwenye Imani kwa maana ya maandiko,ni kweli MUNGU aliwapa mapigo mawili makubwa iwapo wataenda kinyume naye, Magonjwa(Tauni) pamoja na kuwekwa mikononi mwa Adui,lakini wakirejea kwa MUNGU basi hakuna Taifa litaweza kuwashinda kivita,akili na uwezo wa juu wa kupambanua mambo.

Yote kwa yote vita vyao havituhusu,sisi ni watu wengine kabisa na maisha yetu
Sasa mbona kwa mungu hawajalejea au mungu wao na wa kwenu nitofauti maana nyinyi mungu wenu yesu a.k.a ISSA lakini wao hawamtambui wanamchukulia
 
Hili si suala la ushabiki wala kiimani. Uungwana siku zote ni kujitendea haki mwenyewe kwa kuukabili ukweli hata kama ni mchungu.

Sote ni wafu watarajiwa na kwa mola tutarejea. Hata ipo tofauti linapokuja suala la kurejeshwa na binadamu wengine, ndiyo maana kelele zinapigwa.

Rejea "Operation Plasma" ya MOSSAD kumhusu Mohamed al-Mabhouh kamanda wa HAMMAS, aliyeuwawa Dubai 19 January 2010:

The Dubai Operation: Mossad, Murderer & Mayhem in the Desert

Hiyo ni case moja yenye kufanana na nyingi za namna hiyo, zenye kuwahusisha Israel au Marekani.

Pattern ni hiyo hiyo kote, kila mmoja wa wawili hao akiguswa popote. Si vigumu kutambua iko kama sheria isiyo rasmi (rule of the thumb) kuwa:

"Ukimwua au kujaribu kumwua mwisrael au mmarekani au ukiyatishia mataifa yao au watu wao popote; tokea muda huo, tambua wewe ni mfu unayetembea, na watakuondoa."

Ya kwamba watakusaka pamoja kukuondoa wao duniani, bila kujali muda wala gharama. Ya kuwa kwenye hilo tangia mataifa yao yamekuwapo kwenye hilo hawajawahi kushindwa!

Yale yale ya akina Osama bin Laden, Mula Omari, General Farrah Aideed, Saddam Hussein, Muamar Gaddafi nk.

Angetoboa Haniyeh, Nasrallah au Sinwar? Watatoboa Ali Kamenei, yule wa Houthi, au nani?

Kwa sababu mataifa wawili hawa kwenye haya ya kutishiana nyau ni wamoja, ziko namna mbili tu za kushughulika nao kwa mafanikio:

1. Kusalimu amri kama UAE, Saudi Arabia nk yaishe kama unataka kuishi. Au:

2. Kupambana nao relentlessly bila pause ukafe mkipigana, kama ni nia yako japo kuwagawia nao maumivu ya kutosha kwa kadri iwezekanavyo.

Hili la pili ndipo alipokosea Hezbollah na ndipo anapokosea Iran kwani hawako tayari kusalimu amri. Ni wazi wamekuwa tayari kufa lakini wame "pause" na sasa cha mbwa koko kitawakuta.

Kwamba watapigwa surprise? Kwa hakika lile la aina ya "pagers na walkie talkies" si muda mrefu litawakuta Iran.

Kumbe kipi kipo salama nao chenye technolojia yoyote ya mmarekani? Ni TVs, computers, magari au gadgets zozote zenye chipsets zozote zenye lolote na wamarekani?

Kutowatokea wote wawili hawa bila kukoma (in hot pursuit) na kuwapelekea moto vilivyo sasa, yatamkuta Iran kama ya Hezbollah, asishangae hatakuwa na uwezo hata kurusha ngumi.

Alipoletewa moto rasmi Hezbollah, maelfu ya wapiganaji wake walikuwa tayari ni mahututi hosipitalini: vipofu, mikono hamna, miguu hamna, matumbo yamefumuliwa, nk.

Kwamba Hezbollah alianzishiwa vita rasmi, makamanda wote wakuu wakiwa marehemu na hawezi kutumia vifaa vyovyote vya mawasiliano.

Haihitaji macho ya kinabii kumwona Iran naye yulee ..., kama Hezbollah au kama kuku bandani akisubiria zamu yake ya kuchinjwa!

"Na huo ndiyo ulio ukweli mchungu .
mkuu yeyote anayepigana na israel au U.S.A anawajua vizuri kuliko ulichoandika wewe hapa ila tu hao jamaa(hezbollah,hamas,iran n.k) sio waoga km wewe linapokuja swala la kupigania maslahi yao yaani wewe huijui israel na U.S.A zaidi wajuavyo ila bado mapigano yataendelea mpk mwisho wa dunia kwasababu hizi mbinge hazijaanza leo
 
mkuu yeyote anayepigana na israel au U.S.A anawajua vizuri kuliko ulichoandika wewe hapa ila tu hao jamaa(hezbollah,hamas,iran n.k) sio waoga km wewe linapokuja swala la kupigania maslahi yao yaani wewe huijui israel na U.S.A zaidi wajuavyo ila bado mapigano yataendelea mpk mwisho wa dunia kwasababu hizi mbinge hazijaanza leo

1. Ni kweli kinachowala uliowataja kipo huko kwao na siyo miye, wewe wala awaye yote anayeweza kusimulia hilo vizuri kuliko wao.

2. Aghalabu mada nzima na nilipoandika hakuna popote nilipojaribu kuyasimulia hayo wala hata kuwa na nia hiyo.

3. Zaidi sana, sina hakika woga wangu ulioandika hapa unausoma wapi?
 
Kwa Iran hapana, sikubaliani na wewe!
Sioni namna Israel anaweza kuishinda Iran bila Tel Aviv kugeuzwa majivu.

Covert operations haziwezi kumpa ushindi dhidi ya Iran, zitampa tu ujiko machoni kwa wapuuzi.

Kwa Hezbollah na Palestine sawa, hapa nakubaliana na wewe, hawa shughuli yao imekwisha, anayefuatia ni Yemen.
Toka ndani ya mfuko wa sandarusi.Iran hapambani na Israel. Anapambana na kundi la magangwe wa dunia.
 
Tusubiri mkuu; muda ni mwalimu mzuri. Napata sana tabu kumuamini Russia kwenye case ya Iran (mjadara ungejikita kwenye jicho la kiitelenjensia badala ya mambo ya imani/dini ungekua mzuri sana ). Russia ni moja ya mataifa yanachukia sana mambo ya ugaidi, Iran ndio mfadhiri wa makundi mengi ya kigaidi duniani so hu urafiki wao hasa against Israeli ukweli napata nao shida sana kuuelewa, I'm sure watasaritiana huko mbele. Kuna uzi humu unasema, Netanyahu anamtafuta Putin waongee, hope hawa 2 sio mara yao ya kwanza kuongea, hawa ni marafiki, sema ugomvi wa USA na Russia ndio umesababisha Russia kua na urafiki wa mashaka na Iran ambao to me, hu ni urafiki wa muda.

Coming back to the thread; nakubaliana na mleta uzi, Israeli na USA ni mapacha on both intelligence, military and economically, nitafafanua baadhi ya hayo kwa mtazamo wangu. Kwenye issues za intelligence, Mosaid na USA inaonekana ni watu wanao badirishana sana taarifa, we all knows what happened on September 11, 2001; Mosaid walinusa hatari na wakalikisha information kwa CIA, CIA waka ignore but same Mosaid wakawalinda watu wao na hakuna aliyekufa pale World trade center building, ukisoma jinsi CIA walivomkamata na kumuua Osama Bin Laden, Mossaid wameshirikiana kwa kiasi kikubwa mno na CIA, these guys ni mapacha. Njoo kwenye vile vifaa vya mawasiliano vilivo lipuka vyenyewe na kuua viongozi na watendaji wengi wa Hezbollah, yasemekana hata rais Rais wa Iran nae aliuliwa kwa style hiyo hiyo but who invested to China on that technology? Is USA. Again, watazame matajiri wengi wa USA utagundua wana vinasaba vya Kiyahudi, this is why hata Steve Jobs mgunduzi mkubwa aliye leta mapinduzi kwenye sekta ya mawasiliano ilitakiwa atangulizwe mbele za haki, hakua mzungu, hakua Myahudi. Yale yale ya kina Magic Johnson, R. Kelly nk. Well, swali linabaki, hu mziki Iran atauweza? Let's wait and see

Mkuu umeandika vyema.

Russia hana appetite yoyote kuelekea Iran, Palestina au Lebanon hasa ikizingatiwa kwa sasa ana yake ya kumtosha tu huko Ukraine.

Hakuna popote alipotoa hata tamko la maana, zaidi ya ku "urge restraint and de-escalation" ambako kila mwingine anafanya.

Haipo siri kuwa amekuwa akitafutwa Iran muda wote. Kisa na mkasa ile nuclear program ambayo inatakiwa kuwa crippled kama kwa yaliyomkuta Saddam.

Hapa amesakwa Iran hadi amepatikana na ni suala la muda kidogo tu sasa.

Kwamba anasubiri apigwe kwanza?!

"Ninadhani litakuwa pigo takatifu ambalo na ataujitia mno muda huu wa sasa alipokuwa akiweza kujitutumua, kutoutumia ipasavyo."

Ama hakika kwa vile kukubali yaishe haikuwa uchaguzi wake, heri angechagua kufa akipigana "in hot pursuit" ambapo angewapa angalau maumivu ya kutosha akiwa na nguvu.
 
Mkuu bado mateka wameshikiliwa na Hamas!

Mkuu Gaza umeiona ilivyo?

Israel anatafuta confirmation tu hapo, kuwa Sinwar is eliminated. Kisha utasikia kakubali ceasefire.

Hakuna mateka wazima hapo, wala hao bi Nyau si kipaumbele.
 
naona umeandika kiushabiki sana..kwanza tofautisha kati ya kushambulia nchi iliyokamilika kijeshi na vifaa vyoye kivita kama alivyonavyo Israel na US basi na Iran pia anavyo ipo tofauti kubwa kupigana vita na nchi kamili na vikundi vya wana mgambo kina Hezbollah,IS,Ouath, na Hamas hivi ni vikundi vya wahuni tu ni sawa na kina Alshabab,M23 na Bokoharam wa huku afrika..hapo Israel anajizolea point na misifa kibao ila kwa Iran hiyo ni piga nikupige sababu wanakaribiana kiuwezo pia Iran ana uwezo wa kupaharibu Israel kama ambavyo yeye anafanya huko gaza na lebanon..

1. Kama haya umeandika hivi kuhusiana na mada hii, utakuwa uko nje kabisa ya mada. Iko kwenye mada:

"Hili si suala la ushabiki wala kiimani."

2. Mada inaongelea mataifa mawili ambayo nyuma ya pazia Kuna uwezekano mkubwa wana makubaliano ya siri dhidi ya mahasimu wao.

3. Hapo #2 zingatia mahasimu hao ni hawa:

"Ukimwua au kujaribu kumwua mwisrael au mmarekani au ukiyatishia mataifa yao au watu wao popote; tokea muda huo, tambua wewe ni mfu unayetembea, na watakuondoa."

4. Ukifuatilia kesi mbali, hasimu wao akiingia kwenye anga zao, hiyo ndiyo hatima yake.

5. Iko kwenye rekodi kuwa kuwa hawajawahi kushindwa na huu ni mfano wake:

Yale yale ya akina Osama bin Laden, Mula Omari, General Farrah Aideed, Saddam Hussein, Muamar Gaddafi nk.

6. Ni wazi kuwa Israel peke yake isingekuwa taabu sana kwa Iran:

Palestina ni wahanga, Iran na Israel hawachekani, ila Marekani wapewe maua yao

7. Sasa Marekani ndani wewe options hudhani ni hizi zina thamani?

"Kwa sababu mataifa wawili hawa kwenye haya ya kutishiana nyau ni wamoja, ziko namna mbili tu za kushughulika nao kwa mafanikio:

1. Kusalimu amri kama UAE, Saudi Arabia nk yaishe kama unataka kuishi. Au:

2. Kupambana nao relentlessly bila pause ukafe mkipigana, kama ni nia yako japo kuwagawia nao maumivu ya kutosha kwa kadri iwezekanavyo."


8. Au wewe unadhani kina options gani zaidi ndugu mjumbe?
 
Mabadiliko ndiyo kitu gani ndugu? Kukariri au huko kutojiamini unakuona wapi?

Uliyaona haya kwenye mada?

"Kwa sababu mataifa wawili hawa kwenye haya ya kutishiana nyau ni wamoja, ziko namna mbili tu za kushughulika nao kwa mafanikio:

1. Kusalimu amri kama UAE na Saudi Arabia yaishe kama unataka kuishi. Au:

2. Kupambana nao relentlessly bila pause ukafe mkipigana kama ni nia yako japo kuwagawia nao maumivu ya kutosha kwa kadri iwezekanavyo.
"

Tafadhali fafanua isije kuwa kama manyani, mjinga kumbe ukawa wewe.
Kukariri ni kuamini kwamba Isreal na USA hatatakuja kushindwa. Dogo ktk hii dunia hakuna kitu kisichowezekana
 
Kukariri ni kuamini kwamba Isreal na USA hatatakuja kushindwa. Dogo ktk hii dunia hakuna kitu kisichowezekana

Wapi niliposema hayo ya kuwa hatakuja kushindwa?

Huoni ni katika kukariri kwako kunakokufanya kudhani nimesema hivyo, na hata kufikia kuniita dogo labda kwa kuwa wewe ndiye?

Zingatia : Madogo mabandiko yenu, paragraph 1!
 
Wapi niliposema hayo ya kuwa hatakuja kushindwa?

Huoni ni katika kukariri kwako kunakokufanya kudhani nimesema hivyo, na hata kufikia kuniita dogo labda kwa kuwa wewe ndiye?

Zingatia : Madogo mabandiko yenu, paragraph 1!
🤣🤣🤣 Dogo bandiko lako lilikusudia kutoa ujumbe gani?
 
🤣🤣🤣 Dogo bandiko lako lilikusudia kutoa ujumbe gani?

GFfUGgLWkAAh9uE.jpeg
 
Back
Top Bottom