Marekani na Israel ni mataifa tofauti yenye baadhi ya siri za pamoja, bila kulijua hilo, Iran au yeyote dhidi yao, ni mfu atembeaye!

Marekani na Israel ni mataifa tofauti yenye baadhi ya siri za pamoja, bila kulijua hilo, Iran au yeyote dhidi yao, ni mfu atembeaye!

Kama ambavyo USA hana uwezo wala uthubutu wa kuingia vitani na Russia, na Israel hana uwezo wala uthubutu wa kuingia vitani na Iran, anachoweza kufanya Israel ni covert operations kupitia MOSSAD, na hata hizo covert operations zake zikifanikiwa bado hatoweza kuchukua credit kuwa ni yeye amefanya.
Israel ni nini/nani na MOSSAD ni nini/nani?
 
Kwa Iran hapana, sikubaliani na wewe!
Sioni namna Israel anaweza kuishinda Iran bila Tel Aviv kugeuzwa majivu.

Covert operations haziwezi kumpa ushindi dhidi ya Iran, zitampa tu ujiko machoni kwa wapuuzi.

Kwa Hezbollah na Palestine sawa, hapa nakubaliana na wewe, hawa shughuli yao imekwisha, anayefuatia ni Yemen.
You are wrong. Resistance haitakufa middle East yatabadilika majina tu leo Hezbollah kesho Fatah kesho kutwa jina jingine Hii ni movement ambayo haina kikomo cha msingi inaangaliwa interest kwa kipindi hisika
 
Hili si suala la ushabiki wala kiimani. Uungwana siku zote ni kujitendea haki mwenyewe kwa kuukabili ukweli hata kama ni mchungu.

Sote ni wafu watarajiwa na kwa mola tutarejea. Hata ipo tofauti linapokuja suala la kurejeshwa na binadamu wengine, ndiyo maana kelele zinapigwa.

Rejea "Operation Plasma" ya MOSSAD kumhusu Mohamed al-Mabhouh kamanda wa HAMMAS, aliyeuwawa Dubai 19 January 2010:

The Dubai Operation: Mossad, Murderer & Mayhem in the Desert

Hiyo ni case moja yenye kufanana na nyingi za namna hiyo, zenye kuwahusisha Israel au Marekani.

Pattern ni hiyo hiyo kote, kila mmoja wa wawili hao akiguswa popote. Si vigumu kutambua iko kama sheria isiyo rasmi (rule of the thumb) kuwa:

"Ukimwua au kujaribu kumwua mwisrael au mmarekani au ukiyatishia mataifa yao au watu wao popote; tokea muda huo, tambua wewe ni mfu unayetembea, na watakuondoa."

Ya kwamba watakusaka pamoja kukuondoa wao duniani, bila kujali muda wala gharama. Ya kuwa kwenye hilo tangia mataifa yao yamekuwapo kwenye hilo hawajawahi kushindwa!

Yale yale ya akina Osama bin Laden, Mula Omari, General Farrah Aideed, Saddam Hussein, Muamar Gaddafi nk.

Angetoboa Haniyeh, Nasrallah au Sinwar? Watatoboa Ali Kamenei, yule wa Houthi, au nani?

Kwa sababu mataifa wawili hawa kwenye haya ya kutishiana nyau ni wamoja, ziko namna mbili tu za kushughulika nao kwa mafanikio:

1. Kusalimu amri kama UAE, Saudi Arabia nk yaishe kama unataka kuishi. Au:

2. Kupambana nao relentlessly bila pause ukafe mkipigana, kama ni nia yako japo kuwagawia nao maumivu ya kutosha kwa kadri iwezekanavyo.

Hili la pili ndipo alipokosea Hezbollah na ndipo anapokosea Iran kwani hawako tayari kusalimu amri. Ni wazi wamekuwa tayari kufa lakini wame "pause" na sasa cha mbwa koko kitawakuta.

Kwamba watapigwa surprise? Kwa hakika lile la aina ya "pagers na walkie talkies" si muda mrefu litawakuta Iran.

Kumbe kipi kipo salama nao chenye technolojia yoyote ya mmarekani? Ni TVs, computers, magari au gadgets zozote zenye chipsets zozote zenye lolote na wamarekani?

Kutowatokea wote wawili hawa bila kukoma (in hot pursuit) na kuwapelekea moto vilivyo sasa, yatamkuta Iran kama ya Hezbollah, asishangae hatakuwa na uwezo hata kurusha ngumi.

Alipoletewa moto rasmi Hezbollah, maelfu ya wapiganaji wake walikuwa tayari ni mahututi hosipitalini: vipofu, mikono hamna, miguu hamna, matumbo yamefumuliwa, nk.

Kwamba Hezbollah alianzishiwa vita rasmi, makamanda wote wakuu wakiwa marehemu na hawezi kutumia vifaa vyovyote vya mawasiliano.

Haihitaji macho ya kinabii kumwona Iran naye yulee ..., kama Hezbollah au kama kuku bandani akisubiria zamu yake ya kuchinjwa!

"Na huo ndiyo ulio ukweli mchungu ."
Bila
Nadhani hapa hukupasoma ukapaelewa,Israel anaweza akafanya uhuni kupitia hizi devices akajeruhi watu bila kujali siha zao kama ni wananchi wa kawaida au wanajeshi wakati taifa likiwa ktk taharuki ya tukio hili aka-attack vibaya Muajemi akagaragara mavumbini.

Vita ni mbinu na Zayuni kwa upande huu ameweza.
Iran sio mtegemezi kama alivyo israle . Hizo mishen unazotamba zinakuwa na maana kama nchi ni sole dependant kwenye foreign tech
 
Tarehe 1 Oktoba ulikuwa pangoni?

Israel kipi imefanya ambacho kinaonesha ana dalili ya kumshinda Iran?
Walokole mahabuba kwa israle hauwaambii kitu . Kuna yule professor wao anaitwa marand alisema . Iran inauwwzo wa kurusha 2000 missle in singel wave achana na hizo 180 2000 zikapenye hata 700 si waisrale wataihama hiyo nchi moja kwa moja achillia mbali madhara. Uwezo wa iran hata inch za ulaya hazina huo uwezo kwa sasa
 
Nadhani hapa tunapishana sehemu ndogo sana mkongwe!
Ndani ya Iran kuna Mazayuni zaidi ya 1000, Israel hashindwi kufanya uhuni wake kwa kuwatumia MOSSAD, ameshafanya sana, na bado ataendelea kufanya, kwasababu mazingira yanamruhusu.

Mimi nazungumzia mashambulizi ya moja kwa moja, yaani kama hiki ambacho Israel inakifanya kwasasa hapo Lebanon, hiki ni kitu ambacho Israel hana uthubutu wa kukifanya kwa Iran.

Mtoa mada amesema kilichowakuta Hamas na Hezbollah ndicho kitakachowakuta Iran, mimi nalikataa hili. Iran ni taifa kubwa sana kijeshi hapo Middle East, kwenye upande wa manpower mpaka military infrastructures sio rahisi kuwatia ulemavu kama Hezbollah na Hamas.

Nikukumbushe tu, hii sio mara ya kwanza Iran kuishambulia Israel na Marekani, ameshapiga kambi za Marekani pale Iraq, miezi kadhaa iliyopita amerusha mvua ya mabomu kuishambulia Israel na mwanzoni mwa mwezi Oktoba amezishambulia kambi za jeshi za Israel kwa missiles na hili shambulio la mwisho limethibitisha kuwa Iran ina uwezo wa kupiga popote ndani ya Israel, Iron dome,David's Sling na ushubwada gani sijui, vyote ni njiwa tu mbele ya mwewe linapokuja suala la kuzuia Iran hypersonic missiles.

Hilo shambulio la mwisho ni ujumbe tosha kwa Marekani na Israel, kama Israel itaishambulia Iran, hakuna sehemu itabaki salama ndani ya Israel, pia Iran imeshasema kuwa next time watashambulia miundo mbinu, sio maeneo ya kijeshi tena.

Kwahiyo Israel na mpambe wake Marekani chaguo ni lao, wana option mbili tu, moja kujificha nyuma ya operesheni zao za kiuwoga kupitia CIA na MOSSAD (ni za kiuwoga kwasababu hawatangazi kuwa ni wao wamefanya, wakiulizwa wanaruka kimanga, huu ni uwoga), pili kuingia mazima na kuishambulia Iran kwa kutumia mavyuma yao tofauti tofauti waliyokuwa nayo. Wote tunajua option gani watachagua, na ndio option ambayo wamekuwa wakienda nayo miaka yote dhidi ya Iran, tukiachana na ile option ya vikwazo ambayo sasa imekuwa kama kumpigia mbuzi kinanda kwa mataifa yanayojitambua.
Iran apewe tu maua yake ni nchi gani inauwezo ule aiyounyesha iran unarusha makumbora 2000 km na yanafika pale yalipokusudiwa hata nchi za ulaya huo uwezo hawana
 
Back
Top Bottom