Ungesema koran ni kitabu ambacho kina maneno ambayo ili kuelewa lazima yajaziwe nyama na scholar, hakina maelezo ya kotosha kuhusu jambo flani, unakuta kinataja jina from no where Ukitaka kujua huyo ni nani huwezi mpaka uende kwa scholar au hadith (kuna waislamu wengine wanapinga hadith)
Mfano unasoma haya kama hizi
- Koran 66:1 1. Ewe Muhammad! Kwa nini unaharimisha alicho kuhalilishia Allah?... -unajiuliza huyu muhammad aliharimisha nini ambacho allah alikuwa amemuhalalishia ? Koran haina majibu ila inabidi uende kwa binadamu scholar waislamu ndio wakwambie ni nini hicho!
- Koran 36:14 Tulipo watumia wawili, wakawakanusha. Basi tukawazidishia nguvu kwa mwingine wa tatu. - ukijiuliza Hawa watu ni kina nani? koran haina majibu inabidi uende kwa binadamu scholar waislamu ndio wakutajie majina ya watu hao NB: unakuta scholar wenyewe wanatofautiana hayo majina kwa hiyo unatoka kapa
UNAKOSEA KIONGOZI.
Quran inajitosheleza sio mpk ujazie maneno ya wanazuoni.
Je hao wanazuoni hayo maneno ya kujazia wanayatoa wapi?
Nani alofanya wanazuoni wawepo?
Je maneno wanayosema wanazuoni ni ya kujazilia?
Na je hao wanazuoni wanaokhitilafiana ni wa zama gani ?
Na wanakhitilafiana ktk nini?
Umeingiza mada nyingine ndefu.
Ila wacha nikujuze kuhusu Quran.
Ambaye ameshushiwa Quran ni Mtume(s.a.w).
Yeye ndiye anayejua sababu ya kushuka kila ayah.
Na yeye kama mtume ndiye mwalimu wetu ambaye anatakiwa atufundishe kila ayah inaposhuka.
Quran inaongea kauli za mafumbo mafumbo ambayo yamejitosheleza na ambaye aliyekua akituelekeza ni Mtume wetu na yeye ndiye aliyewarithisha wanazuoni.
Na wanazuoni hawakhitilafiani ktk Quran bali wanakhitilafiana ktk hadith na fiqhi.
Pia wanazuoni wanaokhitilafiana sana ni wale wa miaka ya 600 baada ya kufa mtume.
Mathalan hiyo ayah ulioleta ya suratil tuharrim juzuu ya 28 inamzungumzia mtume ambaye aliharamisha asali kisa kutaka radhi za wake zake.
Kwahiyo aliyeeleza kuhusu hilo ni ye mwenyewe mtume aliyeshushiwa ayah.
Na pindi mtume alipokua anawafundisha maswahaba zake kina abuu hurayrah,Abdillahi Ibn masoud ambao ni moja ya wanazuoni walofundishwa directly na mtume aliwafundisha kwamba kila ayah imeshuka na sababu yake na kisa chake .
Wao wakarithishwa na mtume na wao wakaturithisha sisi.
HAkuna mtu anayepinga hadithi ila kuna hadithi thabiti na kuna hadith batili na kuna vigezo vya kuikagua km hadith thabiti au batili na hiyo ni elimu nyingine