Marekani wanasumbuliwa na Umasikini sio Ubaguzi

Naunga mkono hoja, inatakiwa uwe kama roboti ili uweze kukidhi maisha huko, wengine wanafanya kazi zaidi ya sehemu moja ili kumudu gharama za maisha, inaitwa hakuna kulala......mfumo wa kibepari ni mfumo wa kiibilisi unawafanya watu waishi kama maroboti...
 
Wana kitu kinaitwa food stamps
 
Kabla sijafika huko nilikua na akili kama zako za kwenye kahawa Ila baada ya kufika huko nilijionea mwenyewe !!!!achana na hawa jamaa
 
Mtoa mada nisiende kwenye kukubaliana na kwamba hili tatizo ndilo linqsababisha maandamano ila USA maisha magumu yapo tena yanayosababisha msongo wa mawazo.....


Wanaokuambia haujafika waambie kuna reality shows kibao zitafute uangalie wanavyoishi maisha ya hovyo....sisi tabu yetu kubwa miundombinu....kwetu maisha hajawa tight saana.
 
Anasave hvyo hlf kashindwa kulipa dola elf 17 za kutibiwa sikio...[emoji1787][emoji1787][emoji1787] hakunaga watu choka mbaya kama madayaspora [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Maisha tumia akili hata kama unayo si lazima ulipe.

Kwanini nilipe na ninajua kuna watu wanaweza kulipa.
 
Kama ni kweli, sisi tunanjaa kuliko wao, pia jamaa wameendelea sana.
 
S Sio Shamba, kumiliki nyumba US lazima uwe tajiri kweli kweli, wengi wamepanga
 
Umasikini ni nini?
 
Kwahyo unatakaje. Ule bila kufanya kazi kama watz mlivyozoea?
 
S
Sio Shamba, kumiliki nyumba US lazima uwe tajiri kweli kweli, wengi wamepanga

Sio kweli mfumo wa marekani kumiliki nyumba ya kuishi ni kitu rais

Unaweza kwenda serekali ukaomba wakujengee nyumba utakuwa unalipa taratibu mfano kila mwezi dola 500

Kuna nyumba za mkopo unaweza kununua pia ukawa unalipa kila mwz $ 1000 ila inategemea nyumba ina bei gani

Kumbuka ishi kulingana na kipato chako

Mfano kipato chako ni $ 2000 unataka nyumba ya trump,mambo hayaendi hvyo
 
Ila nimependa unavyojibu na kupangilia majibu yako; Hongera.
 
Ninavyojua Mimi, Huko US Kama wewe ni raia wa nchi ile ufanye kazi usifanye kazi huwezi kukosa chakula Wala kulala nje kwenye mtaro labda uamue mwenyewe kuishi kwenye mtaro otherwise Kodi ya nyumba haiwezi mfanya raia wa US aishi mtaroni
Siyo kweli. Kuna raia wengi tu wa Marekani, tena wa Kuzaliwa; halafu ma Veteran sasa. Kwa maana ya kwamba walikuwa jeshini huko na wakaenda vitani. Hawana kazi na ni ma homeless. Kwa hiyo wewe kuwa raia hakukufanyi kuwa na mtelemko wa maisha. Ukizubaa unaishi mtaroni kweli. 😀😀
 
Tofautisha hectare na acre
 
Socialism,education for self reliance in Tanganyika.
 
Hebu nipeni mkwanja niende marekani kuwaletea ushuhuda.
 
Maskini Tanzania, ana ng'ombe 500 hadi 1000. Ana mbuzi na kondoo wapatao 100, anakuku wa kienyeji ambao ukimtembelea muda wowote unachinjiwa, Maskini huyu anamashamba hekari si chini ya ishirini, anaishi kijijini, hana TV wala hana simu ya touch. Zaidi anasimu ya button. Ok wewe unaelipwa na serikali umekatiwa na bima. Ukijilinganisha na Maskini wa Tanzania wa kijijini ni nani alie na vitega uchumi. Nimeishi Ulaya mara nyingi niliwaambia swala si umasikini ni "life style" kwa sababu Mmasai anae kaa porini na kuitwa masiki wakati ana ng'ombe 1000 hadi 5000 si sawa. Au msukuma aliye na ng'ombe na mashamba kusema ni masikini sidhani. Kwani Ulaya au Marekani kuna wengi wasio na uwezo wa kumiliki ng'ombe 5000 kuwa na mashamba na nyumba hata ukiwambia waje huku kununua. Wengi wanaishi kupata hela kulipia pango na kula basi. Chukulia mfano yule mzee wa kimasai alojenga shule yake kwa familia alikuwa na watoto Zaidi ya 80. Wote aliwalisha. Huko Marekani wewe unaejisifia kupewa hela na serikali ungeweza? Hata ulipwe na serikali miaka 10 uwezi mfikia huyu mzee. RIP Mzee wetu wa Ngorongoro. Watu wanazuzuka tu na maisha ya Ulaya na Marekani lakini hakuna kitu. Tazama vijana walioko Tanzania wanavyopata mafanikio Zaidi ya walioishi Ulaya miaka kibao.
 

Hivi watanzania wangap wamemilik hayo unayoyataja hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…