Marekani wanasumbuliwa na Umasikini sio Ubaguzi

Facts ni facts tu hazijali nchi yako au sio yako.
Fuatilia pia na masuala kama tofauti za Life span, maternal mortality rate na child mortality kati ya nchi yako na huko uliko kama ni kweli uko huko uliko
Kwani Marekani wote ni wazungu?.

Sihitaji kubishana, uzuri nimekuelewa nikupe ushindi. Ila sintokaa kuichafua nchi yangu au kuidharau kwa sababu ya facts. Kama kunachanga moto nitajitahidi nichangie kupunguza. Mfano miaka iliyopita nilisomesha wanafunzi sekondari wasiopungua miamoja. Ilikuwa kipindi wanafunzi wanalipa Ada wa sekondari. Niliwatafutia ufadhili wanafunzi watano wa vyuo vikuu waliokoswa mikopo wakati huo. Niliwasaidia walemavu wasio na uwezo kujiajiri kwa kupewa mitaji na mashirika ya kitanzania. Pia nilisaidia baadhi ya vijana kupata ajira katika sekta binafsi. Uwa sina muda wa kulaumu nchi yangu na kuikashfu. Bali nipo kutoa mchango wangu ktk Taifa langu. Kikubwa nione ni nini nimefanyia nchi yangu. Naona fahari kuwa mtanzania na natangaza mazuri ya nchi yangu. Changamoto zilizopo haziishi siku kwa siku moja. Hivyo mawazo au nilichonacho kidogo nashirikiana na watanzania wenye nia njema kusaidia kupunguza tatizo. Na sio kubeza na kuikashfu. Tusisubiri viongozi kutuletea maendeleo tujumuike kama jamii. Bila kujali nafasi zetu au uwezo wetu. Hata leo Mungu akinichukua akaniuliza uliifanyia nn nchi yako ninalao la kumwambia na kujivunia. Kuwa niliitumikia nchi yangu kwa haya.
 
Mungu hatakaa akuulize uliifanyia nini nchi yako kwa sababu hizi nchi hazikuundwa na Mungu.Labda atakuuliza ulimtendeaje binadamu mwenzako aliyekuwa karibu na wewe.

Nchi ni mipango tu ya kufikirika ya jamii fulani tu za watu walioamua kujitwalia vipande fulani vya ardhi kujiita sisi ni Ufaransa,Ujerumani n.k.

Kwa Africa nchi zetu ni wakolini tu walikaa mezani Berlin mwaka 1884/1885 na kuichora hii mistari leo inayoitwa mipaka inayomtenganisha Mmasai wa Kenya na Tz kisha kuipa majina kama vile Tanganyika au Bechuanaland kisha baadaye wakoloni walipoondoka tukaamua kujiita Tanzania, Botswana n.k
 
Hebu nipeni mkwanja niende marekani kuwaletea ushuhuda.
Tatizo ukienda huko na ukaona maendeleo ya vitu na ukilinganisha na ulipotoka laxima utapaona peponi huko, lazima upinge kukubali kuwa et huko nako kuna maisha magumu.
 
We ungekuwa umewahi fika USA ungeongea ukaeleweka Tz ndo kuna umaskini wakutupwa sio USA.

We jamaa sikutegemea kuwa kichwani ni empty.
Umasikini America upo bwana we nae sema ukifika wewe na ushamba wako ndo unaona kama wote ni matajiri kwa sababu ya miundo mbinu iliyowekwa na serikali yao toka zamani kwa kua ni nchi tajiri..sasa kila nchi ina masikini na huwezi pia kutaka kufananisha umasikini wa America na hapa kwetu hiyo inakua wala haina maana yoyote,hata masikini wa hapa na Malawi hawafanani pia. America ina masikini wengi tu na wengi wao ni wale waliojiaminisha wakienda America watatoboa kimaisha,mwisho wa siku wanakuta taratibu zilizo wekwa na serikali ile huwezi kuchuma pesa ya kule ukaihamisha kuja nchi zingine,ndo mana utaona wengi wana kwenda huko na wanarudi na migogo tu huku wamevaa miwani za jua na hawana pesa.
 
Acha uongo.. Marekani maskini anamiliki vipi shamba au ardhi.. Tanzania mtu hana hata mia lakini ana shamba lake la kulima .

Tanzania kila ukoo una shamba.. kila familia ina shamba kijijini kwao...je usa ardhi inapatikana kiurahisi kama Tanzania
Acha kubishana na wanachadema hao utaumia mbavu zako bure mkuu...
 
Nimekuona ni 'mpumbavu' nisamehe kwa hilo, unazisemea jamii za kifugaji yani wamasai na wasukuma umesahau kuna zaidi ya hao watu

Hao ng'ombe 500 na ardhi kubwa msafwa,mnyakyusa,mkinga,mmagoma azitolee wapi?

Bado unaongea kuhusu vijijini vipi kuhusu hali ya umasikini mjini? Huku ndio watu wanaishi kama mashetani na sipo kupiga porojo kama mleta mada ukitaka kuthibitisha kaangalie foleni ya TASAF

Kabla hamjatetea upuuzi mbele ya wenye akili inabidi ufikirie mara mbili mbili, Tanzania asilimia 30 ya watu na zaidi wanaishi chini ya kipato cha dollar 1 lakini US sidhani kama kuna aina ya hizo sampuli sasa sijui naanzaje kuwaelewa watu ambao wanakwambia 1usd ni sawa na 100usd

Acheni propaganda nyie watawala ipo siku yenu isiyo na jina mtawashiwa moto kuliko hata huo unaoendelea huko US
 
Mkuu, kupata ukweli ungeangalia viashiria vya umasikini kati ya nchi mbili Tanzania [emoji1241] vs United States [emoji631]

Iwapo mmoja anaviashiria vifuatavyo basi huyo ndiyo masikini.

Hapa nimeweka viashiria 4 ambavyo ni vya msingi kabisa.

1 • Makazi duni.

2 • Lishe duni.

3 • Magonjwa (hasahasa yale yanayoweza kuzuilika kwa urahisi kabisa mf cholera, typhoid etc)

4 • Elimu duni.
 

Kumbe unafahamu Tanzania ni tajiri halafu kila siku unamnanga JPM? Au huo ni wivu tu?
 
Maskini wa Tanzania ndiye anayelala njaa ila maskini wa Ulaya na Marekani hawezi kulala njaa.
Tanzania sio nchi ya kijamaa,ni nchi ya kibepari.
US watu mbona hata wengine hulala nje hata pakulala hawana MKUU

Ila ukweli usiopingika nikwamba wenzetu huduma nyingi nazamsingi wameziimarisha

Ijapokua hapa alokosea mleta mada nikunyoosha maelezo maana kapindisha pindisha maneno sijui anaficha nini

Ukweli upo wazi kwamba US ukikutana namaskini ujue si maskini nifukara ila ukweli zaidi nikwamba jamaa kwenye huduma nyingi wakopoa

Ila ukweli pia nikwamba waafrika wengi hasa wakusini mwajangwa lasahara kula kwao imekua shida sana mtu kupata milo mitatu imekua tatizo

Ambalo hakulisema mleta mada angeweka wazi madhaifu yaubepari ambayo yapo wazi kabisa yakwamba wenye mali niwachache sana nandio wanaofaidika namfumo husika kuliko wengi wao

:-suala lamaandamano US ukweli limedhihirisha kwamba hali ya Uchumi haikia vyema hasa katika kipindi cha LOCKDOWN...
 
Familia nyingi za kifugaji, nenda umasaini, usukumani, nenda huko singida kwa wafugaji. Nimechukua kama sample. Hata Marekani kuna majimbo Watu wanaishi chini ya dollar moja.

Ila ndo nashangaa kila kona kwa hisani ya watu wa marekani .
 

Acha hizo mkuu
Chakula mtu hawezi kukukaribisha.


Tulikuwa tumekaribishwa hapo mkuu.
Au unamaanisha ya aina gani

Wamarekani wana utamaduni wa kupika chakula na kualika majira marafiki na watu wengne kula pamoja
Unaweza kuwa unafanya hvyo kila mwaka,mwez,wiki.

Hata dinner,launch,kahawa mtu anaweza kualika marafiki zake hotelin na bills zote akalipia.

Picha ninazo nyingi sana nimepewa mihaliko ya chalula mara nyingi.

Ukitaka picha zaidi nitakutumia
 
Ndio yanayonitokea mm hayo

Sent from my JSN-L21 using JamiiForums mobile app
 

Sina haja ya picha nachoongea ni kuwa mzungu hawako free ukaenda kwake akakupa chakula free kama ilivyo kwa watanzania. Achia mbali hivyo vimihaliko vya msimu unavyopata na kuweka picha humu. Hivyo mtu yoyote anaweza pata. Ebu nenda Leo kwa huyo alokukaribisha bila taarifa kama atakukaribisha akupe chakula. Sijaongelea mihaliko. Mimemahanisha ukarimu wa mtu kwenda kwake bila taarifa na akakukubali na bado akakupa chakula. Hiyo tabia ya mihaliko hipo kila sehemu duniani. Weka picha zako tukuone unavyokula na wazungu! Ha ha ha ha! Hongera! Ila ungejaribu kwenda wakati ujakaribishwa! Ila hongera kwa picha za kukaribishwa na wazungu. Weka nyingi tukuone!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…