Marekani yaanza kutafuta uungwaji mkono ili kuiwekea vikwazo China

Marekani yaanza kutafuta uungwaji mkono ili kuiwekea vikwazo China

g7.jpg
Kwa mujibu wa Reuters, mashauriano hayo yapo hatua ya awali yakilenga kupata Washirika kutoka mataifa mbalimbali, hasa Kundi la Nchi 7 Tajiri Duniani (G7) ili kuratibu vikwazo vyovyote vinavyowezekana.

Uamuzi huo unafuatia #Washington na washirika wake kuituhumu #China kuwa inataka kuisaidia #Urusi Silaha za Kivita ili kupambana na #Ukraine, licha ya Serikali ya Rais #JoeBiden kutoweka wazi ushahidi.

Aidha, #Marekani imeidhinisha kibali cha kuiuzia #Taiwan Silaha za Tsh. Trilioni 1.4 yakiwemo Makombora ya Meli (F-16), Makombora 200 ya kukinga Ndege (AMRAAM) na 100 ya AGM-88B HARM.

==============

The United States is sounding out close allies about the possibility of imposing new sanctions on China if Beijing provides military support to Russia for its war in Ukraine, according to four U.S. officials and other sources.

The consultations, which are still at a preliminary stage, are intended to drum up support from a range of countries, especially those in the wealthy Group of 7 (G7), to coordinate support for any possible restrictions.

It was not clear what specific sanctions Washington will propose. The conversations have not been previously disclosed.

The U.S. Treasury Department, a lead agency on the imposition of sanctions, declined to comment.

Washington and its allies have said in recent weeks that China was considering providing weapons to Russia, which Beijing denies. Aides to U.S. President Joe Biden have not publicly provided evidence.

The United States has approved the potential sale of $619 million in new weapons to Taiwan, including missiles for its F-16 fleet, as the island reported a second day of large-scale Chinese air force incursions nearby.

The arms sales are likely to further sour already tense ties between Washington and Beijing, which has repeatedly demanded such deals stop, viewing them as unwarranted support for democratically governed Taiwan, an island China claims as its own territory.

The Pentagon said on Wednesday the U.S. State Department has approved the potential sale to Taiwan of arms and equipment that includes 200 anti-aircraft Advanced Medium Range Air-to-Air Missiles (AMRAAM) and 100 AGM-88B HARM missiles that can take out land-based radar stations.

REUTERS
Joka la kibisa a. k. a USA sasa ni wakati wake wa kuvuliwa pichu
 
Wakubwa wakikorofishana sisi huku ndio inakua balaa huyu USA na China wakae chini wamalize tofauti zao wamemuacha Putin kavamia Ukraine bila kutafuta suluhu leo wao ndio wanatoa siraha tena ingawaje najua wanatoa kwa faida yao...China katafutwa na Huawei yake sijui chip mara goggle naona wanamtafutia kesi mpya..
Acha ujinga, kila mtu na rafiki zake. China na Russia na marekani na mazezeta wenzake. Tusichoshane wala tusipangiane
 
Haijawahi na haitawahi kuja kupoteza,keep dreaming.
Unaonekana hujasoma historia bro. Soma kuhusu Dola ya Kirumi (Roman Empire), soma kuhusu dola ya Ottoman (Waturuki) na British Empire (makoloni ya Waingereza). Then uje tujadili. Marekani haina miaka 20 hapo mbele, ita cease kuwa muonevu na muanzisha vita wa dunia! Mark this thread tukiwa hai.
 
Sasa hivi si ajabu mitaaa kadhaa ukakuta hakuna bidhaa yoyote ya Marekani lakini si rahisi kukosa bidhaa ya kichina
Kuna watu hawatakuelewa bro, sijui ufafanueje hawa Pro-USA wakuelewe. China ndio global manufacturing hub kwa sasa na ndio yenye uchumi unaokuwa kwa kasi ya tarakimu mbili ikifuatiwa na India. Kampuni almost zote kubwa za mabeberu wa Marekani zinazalishia bidhaa zake China, akina Apple, General Motors nk.
 
Hawa muwezi mchina hata kwa dawa walahi, na sasa huko marekani kumejaa Ma bipolar psychopath tu walahi!
Kaa kimya 😊😊😊

Hao wakipigana hatapatikana bingwa na ndo mwisho wa dunia siku hiyo. ACHANA NA MAREKANI KABISA! NA USIICHUKULIE POA.
 
Shetani Marekani.
Raia wa nchi zote dunia wanaishi Marekani. Ukimtafuta raia wa urusi, china, india, Tanzania, kenya n.k wote utawakuta Marekani. Hakuna nchi yoyote isipokuwa Marekani inayoishi na raia wa kila nchi.
Acha iitwe Marekani. Kwenye hii migogoro anapiga hela sana kwa kuuza silaha. Tayari keshamuuzia silaha Taiwan. Capitalist achana naye, ana akili nyingi sana za kutengeneza hela
 
Raia wa nchi zote dunia wanaishi Marekani. Ukimtafuta raia wa urusi, china, india, Tanzania, kenya n.k wote utawakuta Marekani. Hakuna nchi yoyote isipokuwa Marekani inayoishi na raia wa kila nchi.
Acha iitwe Marekani. Kwenye hii migogoro anapiga hela sana kwa kuuza silaha. Tayari keshamuuzia silaha Taiwan. Capitalist achana naye, ana akili nyingi sana za kutengeneza hela
Na ndo nchi pekee itakayoshika dola ya duniani kwa kipindi kirefu zaidi kuzidi zote duniani! Huenda yeye ndo akaongoza mpaka Qiyyama... anayebisha ahifadhi uzi huu. 😊
 
Ikubali tu ishapoteza umonita wa dunia bado ukiranja
Kama Russia, korea kaskazini na China wanawekewa vikwazo nani aliyebaki hapo?
Ni nchi gani iliyowahi kumuwekewa vikwazo marekani au yenye uwezo wa kumuwekewa vikwazo?
Hizi vita russia na china wanazozianzisha zinamnufaisha sana Marekani kwa kuuza silaha. Tayari Marekani ameshamuuzia silaha Taiwan za pesa ndefu.
Ukijua kuwa Marekani wale watabaki kuwa ni kiranja wa dunia. Ukitafuta raia wa nchi yoyote ile dunia km Tanzania, somalia, kenya, nigeria, india, china n.k wote utawakuta wanaishi Marekani.
 
Back
Top Bottom