ARVs ziko za aina nyingi sana na za gharama kubwa kadiri unavoweza afford uko Marekani. Cha ajabu wabongo wanaamini hizi ARVs za mtumba tunazopewa huku ni za sawa na wanazopata uko duniani.
Kuna dawa za zaidi ya dola 300 nani akulipie, tutaishia kupata hizi cheap ambazo patents zake ni rahisi na zina miaka kibao sokoni, wafadhiri wanalipia dozi mamilioni ya Waafrika hawawezi leta dawa advanced wataishiwa hela mapema. Unaona kama hao J&J (Johnson&Johnson) hawawezi toa ruhusa utumie tech yao wakati hawajapiga faida na kurejesha research & development cost.
Ni kama kwenda Kidimbwi kwa ofa ukataka ununuliwe Hennessy kisa haina hangover, utaishia kupata Serengeti Lite. Hizo dawa zisizo na side effects kubwa tutazisikiliza ukouko. Kwetu kuna mama mmoja anafanya kazi NGO moja anachukua dawa US hatumii hizi za Buguruni unazoenda umevaa sunglasses na ushungi.