Marekani yaipatia Tanzania billioni 12 kukabiliana na Corona

Marekani yaipatia Tanzania billioni 12 kukabiliana na Corona

Marekani imetangaza kuwa kupitia Shirika lake la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) itaongeza USD 2.4 M (Tsh. Bil. 5.6) ikiwa ni msaada kwa sekta ya afya kuimarisha uwezo wa maabara na upimaji wa kimaabara, jitihada za utoaji taarifa na miradi mingine mbalimbali. #MillardAyoUPDATES

Taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani leo imesema fedha hizi ni nyongeza ya msaada wa USD milioni moja unaolenga kusaidia mapambano dhidi ya kirusi corona uliotolewa hivi karibuni hivyo kufanya kiasi kipya cha pesa zilizotolewa kwa Tanzania kukabiliana na corona kufikia USD milioni 3.4.

Taarifa hiyo imesema kiasi kingine cha dola za kimarekani milioni 1.9 zilibadilishwa matumizi na kuelekezwa kwenye mapambano dhidi ya corona na kufanya jumla ya pesa zilizotolewa na Marekani katika kukabiliana na corona Tanzania hadi sasa kufikia jumla ya USD milioni 5.3 (Bilioni 12 Tsh. )
Zito upo wapi kwani?
 
Kuna watu inawauma utasema Ela za mabeberu ni urith wa Baba zao Yan hawataki kabisa hahaha vip naona marekan anatupa hela ili tupate nguvu ya kuwanyima watu Uhuru wa kuish [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi Kama chadema nimechukia marekan hamueleweki mnamsupport dicteta kwnn imeniuma sn
Mimi kama UVCCM...sikubali hizo pesa za mabeberu na watu wanao kubali ushoga!
Sisi ni Taifa huru na tunajiweza
 
(NJE YA MAADA) .Mkuu chama kinamfia mbowe huko,nimeangalia video sasa hivi kuna wabunge wakike wawili wamekihama CHADEMA kisa unyanyasaji wa kingono unaofanywa na DJ Mbowe

Nasikia anatembeza miti kama hana akili timamu kwa wabunge wanawake

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe jamaa bhana...unapoelekea utauliza nani alimuwekea sumu Mzee Philipo Mangula?
 
Hii imeniuma Sana ...nilidhani USA wataisakama serikali ya TZ lakini kumbe wako pamoja na JPM...Mimi sipendi kwa kweli...
Tehtehteh....Sasa sisi wapinzani tutamwendea Nani kupeleka umbeya wetu ?!?!..tehtehteh
Tuwashangilie Mabeberu... Oyeeeee
Kweli mwanamke matunzo
 
Igweee

Siku chache baada ya mkuu wa Taifa kuviambia vyombo vyote vya nchi kutopokea msaada wowote wa vifaa vya kusaidia covid 19 Serikali ya Marekani kupitia shirika lake la misaada limetangaza msaada wa vifaa vyenye thamani ya USD 2.4M

Kwangu mimi naliita jaribu kwa utawala wa Mzee Magufuli. Maana huwenda kupitia wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki wanaweza kukataa vifaa nakuitaji pesa jambo litaenda kuibua kituko.

Hapa kuna siri kubwa sana na kuishinda ni serikali kupokea msaada ila wakiukataa nakutaka pesa kutaibuka kituko. Na wakiukataa msaada hapo pia wataenda kuamsha shinikizo kali kutoka USA jambo litausumbua uchumi wetu.

Ikumbukwe USD inasimamia Tshs 2338.86 wakati tukiwa na uwitaji mkubwa wa USD wenye USD wanatuambia watatuletea mzigo wa ku support Afya USD 2.4M hivi ni vifaa tiba na Wala sio dolari.

Let's keep silence and see what will happen.
Hakusema wasipokee misaada la hasha isipokuwa ni lazima wizara ya afya wakague na kujiridhisha kama ni salama!
 
Back
Top Bottom