Marekani yaishutumu Urusi kutumia Chakula Kama silaha ya kivita Ukraine

Swadakta!!!
 
sipat picha Putin akifer ujinga wake huu , dunia itakuja kumuona km rais kituko kuwai kutokea na dunia itasahau yote mazur aliyoyafanya kwa Urusi
 
Kajivamia sio ?
 
Sio wa kusikiliza ni kuendelea kumpelekea moto tu
 
Nadhani kama sikosei Ukraine ndiyo inayoongoza duniani kwa uzalishaji wa ngano ikifuatiwa na Russia! Yaani hapo Russia kashika kwenye mpini.
ww unashindiaga ngano?
 
kwan vinamuumiza ?
 
hakuna anaekuombea mafanikio , ukiwaza hivyo bas tambua huna tofaut na mwanamke anaetongozwa kila siku akiambiwa Sikuachi na bado anaachwa , JITEGEMEE KIAKILI HAYUPO WA KUPOTEZA MUDA WAKE KUKUAMKSHA
 
... ila huu ni ujinga sana! Tanzania sio nchi ya ku-import ngano; bali ku-export.
Kabisa,sazingine unaweza kusematumerogwa kumbe niujingawetu tu ndio unatufikisha huko kwenye kuagiza ngano nje ya nchi, Arusha mashamba kibao.

Ngano nizao labiashara tungewekeza huko tungekuwa nauwezo waku export saizi.
Hatuna kiongozi mwenye maono.
 
Sababu kuu mbili za kutoruhusu ngano kutoka ni hizi ambazo Urusi imerudia mara kadhaa kufafanua. Hata jana wamejibu tena.
1.Ngano mamilioni ya Tani za ngano kutoka Ukraine yalikuwa yanasafirishwa kinyemela kwenda nchi za Ulaya kufidia gharama ya msaada na silaha ambazo wamekuwa wakiisaidia Ukraine. Mrusi anasema ni uongo mkubwa na uzushi kwa nchi za magharibi kuudanganya ulimwengu kuwa ngano inaenda kwenye nchi zenye njaa ambazo zipo kusini, Afrika na Asia wakati zinakwenda Ulaya na wenye uhitaji wa hizo ngano haziwafikii. Lengo kuu ni kufidia gharama za wanayoiita ni msaada kwa Ukraine.
Ukweli ni kuwa ngano ya Ukraine ilikuwa ikiporwa tuu na haya mataifa bila kulipa chochote.

2.Urusi imesema bandari zote za Ukraine huko black sea zilitegwa mabomu mengi sana ya chini ya bahari.. Na baadhi ya mikanda ya mabomu yale ilikatika na yamesambaa black sea yote kuelekea hadi Mediterranean.. Kumbuka hadi uturuki walianza kuyavua.. Hivyo hakuna meli ya kiraia inayoweza kusogea au kutia nanga kwenye bandari hizo. Meli zaidi ya 75 zimezuiliwa na Ukraine yenyewe zisisogee maeneo hayo(meli za mizigo).
Suala la kuisafisha bandari na bahari lina endelea ingawa Odessa bado kabisa.

2.Urusi ina mamilioni ya Tani za ngano kuliko Ukraine na imezuia kusafirishwa nje ya nchi mpaka kuanzia mwezi juni au September baada ya mavuno tena. Urusi inasema inahakikisha usalama wa chakula wa watu wake kwanza.
Lakini imekataa kata kata ngano yake isiuzwe kwa mataifa adui.
Vikwazo walivyowekewa vinazuia makampuni mengi ya meli kusafirishwa bidhaa kutoka urusi kwenda nchi nyingine ila wametoa unafuu kwa meli zinazopeleka bidhaa Ulaya na Marekani tuu.. Eg gas, oil, nafaka na ngano. Urusi imekataa huo upuuzi ndio Maana inasema waondoe kwanza baadhi ya vikwazo ambavyo vinawatesa nchi maskini wasipate ahueni kutoka urusi Bali wao tuu.

Muhimu muhimu zaidi ni MBOLEA. DUNIA IKIWEMO MAREKANI WANATEGEMEA MBOLEA KUTOKA URUSI NA MISIMU YA KILIMO NDIO IMEANZA.. MEDVEDEV KASISITIZA MBOLEA YA URUSI INAYOTEGEMEWA DUNIA NZIMA HAITOTOKA KWENDA KWA NCHI ADUI KAMWE. NA AKASEMA HIZO NCHI BILA MBOLEA YA URUSI HAWAWEZI KULIMA AU KUZALISHA CHOCHOTE ZAIDI YA JUISI YA MAGUGU.

KUMBUKA TANZANIA TUNATEGEMEA MBOLEA YA URUSI PAMOJA NA NGANO KWA ZAIDI YA ASILIMIA 70.hatuna mgogoro na urusi ila Marekani na Ulaya wanaziwekea sana vizuizi na vipingamizi kampuni za usafirishaji zozote zinazotoa bidhaa kutoka urusi.
 
Kabisa,sazingine unaweza kusematumerogwa kumbe niujingawetu tu ndio unatufikisha huko kwenye kuagiza ngano nje ya nchi, Arusha mashamba kibao.

Ngano nizao labiashara tungewekeza huko tungekuwa nauwezo waku export saizi.
Hatuna kiongozi mwenye maono.
... kama kuna sekta iliyaonzishiwa kaulimbiu, maazimio, mipango mikakati, na miradi mingi lakini haikuwahi kutoboa mojawapo ni kilimo - Azimio la Musoma, Kilimo ni Uti wa Mgongo, Kilimo cha Kufa na Kupona, Kilimo cha Umwagiliaji, Kilimo Kwanza, sijui takataka gani but all ended in vain!

Unajiuliza tatizo ni uongozi? Maono? Utashi? Ufisadi? Chama kinachotawala? Au nini; hupati majawabu ya kueleweka!
 
Hapa ndio namuelewa sanaPUT-IN_deep
 
Hapa tatizo kubwa ni chama.
Kwamfumo walio jiwekea,chama kimeona hakiwezi kuwajibishwa na wananchi kwa kushindwa kutekeleza ahadi yoyoteile.

Uzalendo pia hakuna.
Viongozi wakisha chaguliwa uzalendo ni kwenye familiazao na wao binafsi hakuna anaewaza kuhusu maendeleo ya nchi na wananchi.

Hauwezi kuniambia miaka 60 ya uhuru eti hatujui umuhimu wakilimo.

Hizo kaulimbiu wanazianzishaga ilikutuzubaisha tu wakati tunasubiria uchaguzi, lakini hakuna hata chembe ya dhamira ya utekelezaji.

Ni laana hata kwa Mungu kwa nchi kama Tanzania kulialia kuhusu bei za vyakula,niswala la viongozi kuwa serious tu na kilimo.
Angalau hii vita ya Ukrain labda itatushtua kujua kilimo ni muhimu kiasigani.

Ngoja tumuone mama na Bashe watafanyanini, sababu tumezoea kusikia mipango lukuki kama ulivyo orodhesha hapo juu lakini haieleweki inaishiaga wapi.
 
Yfafanuz mzur Sana huu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…