Marekani yaongeza ushuru wa asilimia 104% kwa China

Marekani yaongeza ushuru wa asilimia 104% kwa China

Ni kweli USA wana purchasing power kubwa na ni moja ya nchi ambayo ni soko kubwa la bidhaa za CHINA 14.7% ya bidhaa zinazotengenezwa China huuzwa Marekani, zaidi ya ambayo ina mchango wa zaidi ya $524.9 billion.
Hivyo kitendo cha Trump ya kuiongezea China ushuru ni kitendo cha kujiamini kwa sababu, Mchina hana jeuri juu ya hilo na akileta jeuri atakuwa ame drop kiuchumi kwa kiwango kikubwa
Lakini pili Lengo la Trump ni sera ya kiuchumi ya Protectionism Policy ambayo anahitaji kuimarisha Viwanda vya Ndani ya Marekani
Japo atapambana na changamoto kama bidhaa kupanda bei ghafla na kusababisha raia kulalamikia kuongeza ugumu wa maisha.
Raia wa marekani muda c mrefu vyuma vitaanza kukaza,maana soko Lao la bidhaa litakosa ushindani wa bidhaa kutoka nje hivyo bei zitapaa sana,haitaleta unafuu wa maisha kwao, japo maisha yao ni mazuri lakini sio wote
Wamerekani wenye wamenigomea wamedai kitu ambacho kwa sasa akiwezekani.
1.kujenga viwanda kama china ili viweze kutosheleza itawachukua miaka mingi.
2.gharama ya kumlipa mfanyakazi akiwa marekani ni kubwa kuliko china na matokeo yake bidhaa itakua ghali na itawasababishia kupanda kwa maisha.
3.malighafi kama ya gahawa ni ngumu kupatikana na kwakua yeye kawapiga wenzake nao watamkomoa kwa kumuuzia malighafi kwa bei kubwa.
 
Dunia imeishakuwa uwanja wa fuja. Baada ya Trump kuwapiga China na Tarriff ya 34% China wakajibu kwa 34%. Trump kawajibu kwa 104%!! Na zinaanza kazi kesho tarehe 9!! Kila mtu ajitafutie kashamba ka kulima mihogo, kufuga kuku, sungura, simbilisi nk. Nunua na baiskeli phoenix.

Seriously, haya yanamaanisha nini kwa dunia na sisi wa dunia ya tatu?
asubuhi china atatangaza the same 104% respectively
 
China usikubali kidali po kulala kwako, na wewe jibu.
 
Mchina ampige kwenye iPhone na Tesla. US watasanda.
IMG_20250408_222555.jpg
 
This is very unnecessary.

Sidhani kama Trump anajua anachokifanya.

Na kwa mtu anayedai alisoma Wharton School of Business, naona hana uelewa mzuri wa mambo ya uchumi!
ego ikiingia uelewa unatoka mkuu
 
This is very unnecessary.

Sidhani kama Trump anajua anachokifanya.

Na kwa mtu anayedai alisoma Wharton School of Business, naona hana uelewa mzuri wa mambo ya uchumi!
Tulia dawa isambae mwilini
Ulikuwa unamshangilia Trump, haya sasa kimeumana
Mchina yuko poa tu hata arudi tena kwenye stone age.....
We knew he is buffoon....
 
Trump anataka kufanya nini huyu mzee?

Ngoja nifatilie na popcorn kabla ya kuhemka kuiponda akili yake, maana ukiona darasani wale vipanga wote wamejaza jibu ni 4 na wewe umefanya jibu lako ni 32 anza upya kufanya hilo swali hata kama unahisi upo sawa.
 
Nafikiri ni wazo zuri kwa Trump kulinda soko la ndani na kuwafanya wamarekani kununua bidhaa za ndani. So far China lazima apambane mpaka kieleweke ili kulinda masoko yake pia
 
Back
Top Bottom