Marekani yaongeza ushuru wa asilimia 104% kwa China

Wabongo mna focus na China huku kawaumiza hapo bongo kuliko maelezo, kaongeza 10% , kaua contract zote za AGOA vile viwanda vyote vya jeans , korosho na kila kitu sasa kaua maelfu ya kazi kwisha, ARV na USAID projects zote kaua, misaada ya budget kwisha na soon mtawekwa kwenye list ya travel ban, chekeni tuu ila maelfu ya wabongo wameumizwa kuliko China
 
Kiujumla, kwenye huu mvutano baina ya Marekani na China, kila nchi duniani itaathirika. Hii ni kwa sababu nchi hizi mbili kwa pamoja zinashikilia takribani nusu ya uchumi wa dunia. Kwahiyo kudhoofika kwa biashara baina yao kutasababisha kuzorota kwa biashara duniani.

Kwa sababu dunia nzima imeona kuwa Trump ndiye aliyeanzisha kupandisha kodi na, kwa sababu amepandisha kwenye nchi nyingi sana duniani, China inakuwa na fursa ya kusikilizwa na nchi nyingine zilizoathirika na kodi hizi. Ni rahisi kwa China sasa kufanya makubaliano na nchi nyingine hasa za Ulaya, Canada na Mexico ukilinganisha na ilivyokuwa kabla ya kodi hizi za Trump.

Tukumbuke kuwa China ina teknolojia kubwa ya kuzalisha vifaa vya kielektroniki ambavyo vingine Marekani haina uwezo wa kutengeneza. Kwahiyo, pamoja na athari kufika kwa nchi zote, Marekani ina uwezekano mkubwa wa kuathirika mapema zaidi na kwa kiasi kikubwa zaidi.

Trump anataka viwanda virudi Marekani, lakini wafanyabiashara wanasita kufanya hivyo kwa sababu gharama za uzalishaji ndani ya Marekani ni kubwa mno. Inaweza kuwa rahisi kwa viwanda vya Canada na Mexico kuhamia Marekani, lakini sio vya China. Viwanda vya China vinaweza kuhamia nchi kama India, Vietnam, Malaysia na nyingine za maeneo ya Asia. Ikitokea hivyo, bado lengo la Trump la kuvirudisha Marekani litakuwa halijatimia.

China kwa upande wake, inaweza kuongeza kuuza bidhaa kwenye nchi nyingine. Ikiwa hivyo,itasaidia nchi zisizo na viwanda vikubwa kama vile nchi za Afrika kupata bidhaa kwa unafuu. Lakini kwa nchi ambazo zina viwanda vikubwa kama nchi za Ulaya, hiyo itaongeza ushindani kwenye viwanda vyao na kuhatarisha kupoteza ajira.

Tuendelee kufuatilia...
 
Wellsaid, what a fantastic analysis
 
Hata hueleweki!

🖕.
 
Huu ni muda mzuri kwa sisi tuliokataa huduma ya starlink tuwekwe kwenye list...
Uchaguzi wa ujanjaujanja na wizi tupigwe tariffs za kufa mtu.. mpaka akili zikae sawa..
 
Huyo Trump anajitia kitanzi mwenyewe. Anatapatapa kutafuta njia kuwatupia wengine mzigo wa deni la marekani
Ni muda umefika ampe mchina uongozi
 
Tukumbuke kuwa China ina teknolojia kubwa ya kuzalisha vifaa vya kielektroniki ambavyo vingine Marekani haina uwezo wa kutengeneza.

Vietnam(46%), Malaysia,(24%) Cambodia (49%), Laos (48%)...
Trump kabana kote kote, aliyeachiwa hapo ni Singapore(10%)...

Hali si hali...
 
Mwamba anapambania uchumi wa nchi yake kwa kujitoa muhanga,na hamskizi yeyote.
Walichelewa sanaaa,China viwanda ndo vimempaisha na nchi yeyote yenye viwanda vingi lazima ipae kiuchumi.
Sasa viwanda pekee vilivyokua vimebaki na uhakika wa biashara ni viwanda vya silaha TU,Na silaha sharti lake ili uuze lazima upiganishe vita kwa kumwaga damu za watu.
Hatua ya Trump kiuchumi ni kubwa sana na China anaenda kudondoka kiuchumi si muda mrefu Kwa kua marekani uwezo wa kuidhibiti anao tena ni chap tu.
Wafanya biashara wa Marekani wanataka kuingiza ubinafsi TU wakati wanaitwa warudishe viwanda ndani watu wapate ajira,walipe Kodi,wajenge nchi kama ilivyokua miaka ya 1970'S.


China aendelee kuteneneza mafake yake aje alete kwetu mafeki zake,kwa Dunia ya kwanza lazima
 

Si sahihi kusema kuwa wafanyabiashara wa Marekani wanaleta ubinafsi.

Biashara duniani siku hizi iko complex sana. Kampuni inaweza kuwa ya Marekani, lakini ikiingia kwenye soko la hisa, hisa zake zinanunuliwa na watu na makumpuni toka sehemu mbalimbali duniani.

Kwahiyo, usitegemee biashara ya kisasa kuendeshwa kwa siasa za uzalendo. Biashara za kisasa zinaendeshwa kwa hesabu za faida na hasara. Lengo ni kuzalisha faida kwa ajili ya wanahisa. Hakuna biashara inayolenga kujenga nchi fulani.
 
you said it all, ndio maana kule juu kuna mtu nmemwambia kwamba China ana uwezo mkubwa wa kumudu sideeffect za huu mchezo kuliko USA,

Investors hawapendi 'uncertainity' na ndio sabb kuu manufacturing na production haifanyiki USA, hio ni sababu ya uncertainity kutokana na namna ya utawala wa marekani ulivo lakini kwa nchi kama China unakua certain kabisa sabab hata kama utawala ubadilike kuna policies hazitobadilika sabab chama ni kimoja tu.

Sasa CEOs na CSOs wa haya makampuni makubwa wanafanya vile investors wanapenda.

Trust me, trump will taste his own medicine this time.
 
We unajua kwann marekani Kawa super power!
Au unafikiri ni Tanganyika hyo inayochezewa hovyo.
MAKE AMERICA GREAT AGAIN inamaana kubwa
 
Hana uwezo huo,uchumi WA china umekua kiujanja ujanja na hauna miziz imara,na waliitumia USA kukua.
 
0
Asante naona watu wanajitoa ufahamu hapa!
Wabongo kazi ni kushadadia, upepo unakovuma twende.....

Mi sijui uchumi lkn ht basics facts km hizi hao wanaojiita wachumi,wasomi hawazioni?
Yaani nyie muingize vyenu Kwa ushuru mdogo ila yeye mmpige Kwa ushuru wa juu?

No way!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…