Ningetamani sana Iran abakie mfano wa kama China, mchina mchokozee atakukoromea tu na kukuonyeshea videge na vijimabomu na mazoezi uchwaraa..! Kumbe mwenzako yuko mbaaali mno na ukweli huo huku akiendelea kujenga uchumi wake
Irani ni Taifa ambalo sio tu Israel imejitahidi kujenga uwezo wa kuitandika Iran, bali hata mataifa ya Magharibi yanamtamani sana huyo Iran, na ndiyo maana Israel, hapo Middle ni yeye tu mwenye Nuclear huku Iran akiwa kwenye vikwazo vingi kuhusiana na mradi wake wa Nuclear
Hata hivyo, Irani anachukiwa na mataifa mengi makubwa, akijichanfanya tu aipige Israel, atashindwa kujua ni nani hasa anayempiga, maana atachapwa kama mtoto mdogo na kuharibu mazima uchumi wake na kurudi uchumi wa kama Iraq, Yemeni, Syria n.k
Kwa ushauri wangu, asijaribu kufanya hivyo
Niwaombe na waislamu watukutu, waache kumvimbisha kichwa Iran, kwani wao watakuwa ni mashabiki watazamaji tu