Hautoi uwoga kwa kukaripia ugonjwa, unatoa uwoga kwa kupima na kutoa takwimu, hamna kitu cha hovyoo kama kuishi mnavyoishi yaani hamjijui japo mumejipa mzuka wa kujiaminisha corona imeikimbia Tanzania kisa rais aliongea, lakini wengi wenu kwenye nyoyo zenu ndani kwa ndani mnaujua ukweli kwamba corona ni tatizo la kisayansi na halimalizwi kwa matamko ya wanasiasa.
Leo hii kwenu mumefanya corona kama gonjwa la aibu, hakuna Mtanzania anayeweza kujitokeza sasa hivi na kukiri anaumwa corona, atatukanwa sana na kunyanyapaliwa, huo ndio tunaita uwoga na kushikiliwa akili na wanasiasa, hamna uwezo wa kuhoji.
Juzi aliyekua rais wenu marehemu Mkapa alipoaga dunia ghafla, ikawa hofu kote, familia ikapata tabu sana kueleza kwamba rais kafa kwa malaria....hayo maisha ya hovyoo kabisa, yaani mumefanya nichukie ujamaa, maana nchi yote hadi wataalam wote chali hakuna mwenye jeuri ya kuhoji chochote.
Bora huu uhuru tulio nawo huku.