Maridhiano ya CCM na CHADEMA Ndiyo Kawaida ya Vyama vya Siasa Duniani Ilivyo?

Kinachoendelea ni wanasiasa kuungana kuwakandamiza wananchi.

Tukatae huu usanii unaoendelea maana sisi ndio tunaopoteza zaidi.

Kwani hakuna wa kuzungumzia hali ngumu za wananchi katika mazingira haya ambayo wote ni kitu kimoja.
Hakuna mwenye 'conviction' wala 'commitment' juu ya jambo lolote katika hawa wanaojiita wanasiasa tulionao sasa hivi. Mwanzo hadi mwisho wao ni kujinufaisha wao wenyewe.

Ndiyo maana watu kama Mbowe, baada ya kupitia kwenye misukosuko mikubwa sana kama ile aliyoipitia, na baada ya kuona kama watu hawatambui kujitoa kwake, amefikia hatua ya "kwa nini nihangaikie watu wasiokuwa na shukrani!
Hii ndiyo tafsiri ninayoipata kutokana na matendo yake na maamuzi yake baada ya kutoka jela.
 
Wewe umezuiwa na nani kuzungumzia hali ngumu za maisha ya watu? Wakati chadema wanafanyiwa Kila aina ya uhuni na ukatili ulikuwa wapi hadi ukashindwa kukemea? Tatizo lenu nyie chipukizi wa ccm hamjui hata mnachohitaji zaidi ya kuwaza matumbo yenu tu.
Nyie bavicha kuna mnalolijua zaidi ya kukubali kila anachokisema mwenyekiti??
 
Hakuna mwenye 'conviction' juu ya jambo lolote katika hawa wanaojiiaaa ita wanasiasa tulionao sasa hivi. Mwanzo hadi mwisho wao ni kujinufaisha wao wenyewe.
Kila anayeingia lazima ateue watoto wa wastaafu au machawa wao ili kulinda madaraka.

Unakuta cycle ya uoza inaendelea tu over the years.

Kwa staili hii matabaka hayataisha nchi hii.

Daima kutabakia tabaka la watawala na watawaliwa jambo ambalo kwa mfumo wa kimemokrasia sio sawa ukizingatia kwamba hatuna ufalme hapa kwetu na tulishaachana na habari za uchifu.

Sasa kwakua watawala watataka kulinda nafasi zao daima dumu hawatataka kuona mtu wa chini akiwa na elimu bora ama vitu vingine kuwa rahisi kwake ili abakie katika hali hiyo iwe rahisi kumtawala.
 
Sina hakika kama hali ya "ubwanyenye", ambayo Mbowe kajitambulisha kuisimamia sana itakuja kuwepo Tanzania.
Mimi siamini hilo litatokea Tanzania.
Haya ni mambo ya mpito tu kwa muda mfupi.
 
Sawa Kabisa.

Sasa swali ni hilo la CHADEMA kwenda tena kuungana na watu hao, badala ya kukaza nati ili nasi tuondokane na hiyo hali mbovu.
Ni kipi kinachowaingiza CHADEMA kwenye mtego wa kwenda kuendeleza hayo maovu?
 
Sasa maana ya maridhiano haya ni nini, yaani tuendeleze mfumo huo huo mbovu?
 
Nilitaka kumjibu rafiki yangu Kalamu , lakini kwa maelezo haya nanyamaza
 
Ninakubaliana nawe, lakini huwezi kuniambia kutekana, kuiba kura, kuonea vyama vya upinzani na mengine yote mabaya ndizo mila zetu. Hilo sikubaliani nalo kabisa.
Na zaidi ya hayo, tusitumie hii misemo kuhalalisha hali mbovu inayotukabili na kutafuta njia za kurekebisha mambo tunayoona hayafai hata kama ni mila zetu.

Kwani tumeiga mambo mangapi?
 
Mbowe ni fundi. Kuweza kuifanya siku ya wanawake kitaifa iadhimishwe kama siku ya wanawake wa CHADEMA bila Samia kuwa na habari wala kuona hilo, inaonesha kuwa Mbowe na watu wake ni manguli wakubwa kisiasa.
 
Nilitaka kumjibu rafiki yangu Kalamu , lakini kwa maelezo haya nanyamaza
Dah!
Nshamsoma mkuu, Mshana, na nikajichekea mwenyewe.
Kama ilivyo kawaida yake mkuu huyu, kama ulivyo wewe, hana papara katika majibu yake. Lakini kwa kumjibu kifupi tu, nitam'refer' kwa aliyoyasema mwenyekiti wa CCM, tena leo hii hii; mada hiyo imo humu humu.

Ngoja nikamjibu huyu mkuu.
 
Mbowe ni fundi. Kuweza kuifanya siku ya wanawake kitaifa iadhimishwe kama siku ya wanawake wa CHADEMA bila Samia kuwa na habari wala kuona hilo, inaonesha kuwa Mbowe na watu wake ni manguli wakubwa kisiasa.
Sijui ni kwa nini umeamua kuona ufundi toka upande mmoja, na ukasahau ufundi mkubwa zaidi kutoka upande wa pili.

Hapa ndipo watu hupoteza fahamu bila kutambua!
 
Asante kwa mada mzuri mkuu.

Wacha nijifunze waandamizi mnavyorushiana hoja.
 
Siyo lazima kila kitu kianzie kwa democrat vs Republican (USA), Labour party vs Conservative (UK) . Ukisubr kila kitu uige kwa wengine hautakuwa mbunifu
 

Ubunifu wa CHADEMA.
 

Asante kwa ufafanuzi mzuri
 
Maridhiano haya ni ubunifu wa CHADEMA na CCM ndio mtekelezaji.. Wengi wana wasiwasi kama huu wako, lakini CHADEMA ni chama chenye think tank kubwa sana na wasomi wenye weledi na maono ya kutosha sana
Kama hii ndiyo kweli, basi inakulazimu uwe na wasiwasi mkubwa sana kwa kumfanya CCM kuwa ndiye "mtekelezaji."

Akikataa kutekeleza utamfanya kitu gani?

Atakupotezea muda, na mwisho wa siku utaambulia ukoko tu.

Msome vizuri umwelewe Mwenyekiti wa CCM. Yeye anahotuba za visentensi vifupifupi tu, na hana maneno mengi sana.

Jitahidi umsome/umsikilize vizuri. Hana makuu mama wa watu, na wala hazungushi zungushi sana ukimsikiliza kwa makini.
Nenda karejee hotuba yake, kwa mfano ile ya leo.
 
Ukijua maana ya conspiracy utaelewa mengi sana
Wewe mtoa mada kwani ni lazima kila siku sisi ndo tuwe watu wa kuiga, kwani na hao unaowasema hawawezi kuja kuiga huku?.Nadhani ifike wakati na sisi tujione kiwa tunaweza kifanya jambo letu na likaigwa na tuondokane na hizo fikra za kitumwa.
 
Siyo lazima kila kitu kianzie kwa democrat vs Republican (USA), Labour party vs Conservative (UK) . Ukisubr kila kitu uige kwa wengine hautakuwa mbunifu
Tungekuwa na ubunifu wa kiasi hicho unachokifikiri wewe hapa tungekuwa mbali sana kama nchi kimaendeleo.

Lakini najua uliyoandika hapa ni kama unajazia nafasi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…