Martin Masese: Tumezungumza na dereva, ni kweli hilo gari halina kamera!

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Kada na mwanachama wa CHADEMA, Martin Marnja Masese ametumia ukurasa wake wa Twitter kudokeza kuwa wakati wanaelekea kwenye mazishi ya mzee Ali Mohamed Kibao walikutana na dereva wa basi la Tashriff.

Kwenye tweet hiyo, MMM alisema kuwa walikutana na Tashriff express eneo la Mbwewe mkoani Tanga ambapo dereva wa basi hilo alisema kuwa gari hilo halikuwa na camera na hivyo ni ngumu kupata picha ya nini hasa kilitokea ndani ya gari.

"Tukielekea Sahare, Tanga kwenda kumsitiri mzee Ally Mohamed Kibao tumekutana na wanetu TASHRIFF Express eneo la Mbwewe, basi ambalo alitekwa na kushushwa pale Kibo, Tegeta. Tumezungumza na dereva, ni kweli gari hilo halina camera. Ngumu kupata picha halisi ya kilichotokea ndani"

photo_5978616690059100803_y.jpg

SOMA PIA: Ally Mohamed Kibao auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana
 
Hakuna hata Abiria aliyerekodi lile tukio kwa kutumia Simu yake kweli?!

Lakini angepanda Mwanamuziki au Mchezaji wa Yanga/Simba abiria wote wangerekodi na kushea.
 
Kada na mwanachama wa CHADEMA, Martin Marnja Masese ametumia ukurasa wake wa Twitter kudokeza kuwa wakati wanaelekea kwenye mazishi ya mzee Ali Mohamed Kibao walikutana na dereva wa basi la Tashriff.

Kwenye tweet hiyo, MMM alisema kuwa walikutana na Tashriff express eneo la Mbwewe mkoani Tanga ambapo dereva wa basi hilo alisema kuwa gari hilo halikuwa na camera na hivyo ni ngumu kupata picha ya nini hasa kilitokea ndani ya gari.

"Tukielekea Sahare, Tanga kwenda kumsitiri mzee #AliMohammedKibao tumekutana na wanetu TASHRIFF Express eneo la Mbwewe, basi ambalo alitekwa na kushushwa pale Kibo, Tegeta. Tumezungumza na dereva, ni kweli gari hilo halina camera. Ngumu kupata picha halisi ya kilichotokea ndani"

SOMA PIA: Ally Mohamed Kibao auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana
Ujinga... Yaani mtu anatekwa ndani ya bus anapelekwa kusikojulikana na dereva yule yule wa Bus lile lile yupo mzigoni!
Yaani ni kama hakuna kitu kimetokea!
Tumefikaje fikaje huku??
How? Why?
 
Ujinga... Yaani mtu anatekwa ndani ya bus anapelekwa kusikojulikana na dereva yule yule wa Bus lile lile yupo mzigoni!
Yaani ni kama hakuna kitu kimetokea!
Tumefikaje fikaje huku??
How? Why?
Inaonekana ungekua mamlakani ungekua unasukuma watu ndani bila sababu za msingi sasa dereva hapo kosa lake lipi mpaka asiwepo kazini
 
Back
Top Bottom