Martin Masese: Tumezungumza na dereva, ni kweli hilo gari halina kamera!
Nilitaka kushangaa yani wafanye tukio kwenye basi lenye kamera,kumbukeni kunamtu alikaa nae karibu alishuka huyo kazi yake ilikuwa kukagua kwenye gari inann ndani

Kama ingekuwa dar -mbeya kilakitu sahizi lingekuwa wazi ,basi liwe na kamera au laa....SHIDA ni watu watanga
 
Huyo Dereva apewe ulinzi wanaweza kumteka na kumpoteza kwani ni shahidi muhimu sana.
 
Asilimia kubwa watu wana simu janja
Mpaka maiti wanapiga picha na kuzirusha
Ina maana tukio hilo hata mmoja hakupiga hata picha moja?
Lazima wapo
Utekaji ule ulikuwa ni wa hatari si ule tunaojua, huu ulikuwa wa sinema za kimafia. Watekaji walilibana basi kwa mbele na nyuma, mmoja akasimama na bunduki dirishani kwa dereva, wengine wakaingia ndani ya basi mpaka kwenye kiti alichokaa wakiongozwa na mmoja wao aliyekuwa abiria ambaye aliteremka na wenzake walipotimiza misheni yao ya utekaji, kwa hali hiyo yeyote angejaribu kupiga picha ni wazi naye wangeteremka naye.
 
Kada na mwanachama wa CHADEMA, Martin Marnja Masese ametumia ukurasa wake wa Twitter kudokeza kuwa wakati wanaelekea kwenye mazishi ya mzee Ali Mohamed Kibao walikutana na dereva wa basi la Tashriff.

Kwenye tweet hiyo, MMM alisema kuwa walikutana na Tashriff express eneo la Mbwewe mkoani Tanga ambapo dereva wa basi hilo alisema kuwa gari hilo halikuwa na camera na hivyo ni ngumu kupata picha ya nini hasa kilitokea ndani ya gari.

"Tukielekea Sahare, Tanga kwenda kumsitiri mzee #AliMohammedKibao tumekutana na wanetu TASHRIFF Express eneo la Mbwewe, basi ambalo alitekwa na kushushwa pale Kibo, Tegeta. Tumezungumza na dereva, ni kweli gari hilo halina camera. Ngumu kupata picha halisi ya kilichotokea ndani"

SOMA PIA: Ally Mohamed Kibao auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana
Watakuwa waling'oa hizo kamera kwa makusud kwa maagizo kutoka juui ili kuwanusuru watekaji.
 
Ila nyinyi humu mnavituko sana. Nimecheka balaa. Asante mkuu kwasababu imepunguza majonzi hahaha
🤣🤣 Hata Mimi wakati nakusoma first time nilicheka sana 🤣🤣 ulinipunguzia stress
 
Inaonekana ungekua mamlakani ungekua unasukuma watu ndani bila sababu za msingi sasa dereva hapo kosa lake lipi mpaka asiwepo kazini
Kumsimamisha kazi ni kumtuliza akili yeye na konda wake.Kumsaidia asiweweseke na kukutana na dhahma yoyote.
 
Asilimia kubwa watu wana simu janja
Mpaka maiti wanapiga picha na kuzirusha
Ina maana tukio hilo hata mmoja hakupiga hata picha moja?
Lazima wapo
Mkuu hata mie niliwaza na kujiuliza hivyo pia; Nina amini, na ninatumaini yupo walau mmoja ambae alipiga picha.
 
Utekaji ule ulikuwa ni wa hatari si ule tunaojua, huu ulikuwa wa sinema za kimafia. Watekaji walilibana basi kwa mbele na nyuma, mmoja akasimama na bunduki dirishani kwa dereva, wengine wakaingia ndani ya basi mpaka kwenye kiti alichokaa wakiongozwa na mmoja wao aliyekuwa abiria ambaye aliteremka na wenzake walipotimiza misheni yao ya utekaji, kwa hali hiyo yeyote angejaribu kupiga picha ni wazi naye wangeteremka naye.
Sababu za kumteka zilikuwa n nini hasa?
 
Ni wakati muafaka sasa kuwa na 360 degrees hiden camera kwa nguo - camera ambazo zina live coverage kusaidia kama ukipotea watu wapate pa kuanzia.

Kumbuka hiden camera inaweza kuwa ndogo zaidi ya kifungo cha shati.

Mbinu ya kujilinda.
 
Mkuu hata mie niliwaza na kujiuliza hivyo pia; Nina amini, na ninatumaini yupo walau mmoja ambae alipiga picha.
Inawezekana ingawa kuna mdau anasema waliwatishiwa kubebwa kama wakipiga picha
Ila ni ukatili sana
 
Kada na mwanachama wa CHADEMA, Martin Marnja Masese ametumia ukurasa wake wa Twitter kudokeza kuwa wakati wanaelekea kwenye mazishi ya mzee Ali Mohamed Kibao walikutana na dereva wa basi la Tashriff.

Kwenye tweet hiyo, MMM alisema kuwa walikutana na Tashriff express eneo la Mbwewe mkoani Tanga ambapo dereva wa basi hilo alisema kuwa gari hilo halikuwa na camera na hivyo ni ngumu kupata picha ya nini hasa kilitokea ndani ya gari.

"Tukielekea Sahare, Tanga kwenda kumsitiri mzee #AliMohammedKibao tumekutana na wanetu TASHRIFF Express eneo la Mbwewe, basi ambalo alitekwa na kushushwa pale Kibo, Tegeta. Tumezungumza na dereva, ni kweli gari hilo halina camera. Ngumu kupata picha halisi ya kilichotokea ndani"

SOMA PIA: Ally Mohamed Kibao auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana
Sawa basi watu wote waliokuwepo ndani pamoja na dereva hawana simu?
Watu waliopo nje hapo tegeta hawana simu?

Maana hakuna hata picha moja au picha mjongeo inayo onesha kadhia hiyo.

hawa watu kazi yao kuchukuwa picha za kipuuzi tuu.

Inasikitisha sana.
 
Inasikitisha basi zima watu waliogopa kusnap hata kwa gizani gizani hivyo hivyo tungejua pakuanzia? Si mnakumbuka picha zilivyowaambua wasiojulikana waliovamia studio za clouds ?
 
Back
Top Bottom