Tetesi: Marufuku ya kuzidisha abiria ili kupambana na Corona, Daladala zimeanza kugoma Dar es Salaam

gomeni hakuna shida...
 
Ukiona biashara hiyo hailipi acha fanya mengine yenye maslahi mkuu, watu waambukizane korona kisa nyie kupata hela?
hawa watu wa daladala wana tamaa sana asee, kila wakati wao wanataka super profit hata wakati wa majanga, hawajui kusoma alama za nyakati kabisa...
 
Nimekuelewa mkuu lakini naomba kuuliza; bus mfano Eischer ukilinunua jipya unaweza kulitumia kwa muda gani?
 
Level seat kwa daladala za Dar mmh haiwezekani, kuna kipindi walileta hii sheria ila iligonga mwamba.
Unajua kwanini iligonga mwamba? Mwaibula hana hamu nao
 
Kwa utaratibu huu itakuwa vigumu sana. Biashara ya dalal dala ni ngumu sana. Mfano hapo Mwanza dalala kwa kawaida inatoza Tshs.400 kwa tripu na nyingi zina viti vya abiria 15 kwahiyo kama ni level seat itachukua abiria 15 @ 400 = 6000 na kwa siku inaenda safari 20 yaani kwenda safari 10 na kurudi safari 10 na hivyo Tshs.6000x20 Tshs.120,000. Mafuta kwa siku ni kama lita 30x2260 = Tshs.67,800, Hela ya Tajiri kila siku Tshs.50,000. Hela ya wale wajamaa Tshs.5,000, Hela ya dereva na tingo Tshs.20,000, Mafuta kwa siku inayofuata Tshs.67,800. Hvyo gharama yote kwa siku ni Tshs.210,000. Mapato kwa siku ni Tshs.120,000 - 210,000 (-90,600) ambayo ni hasara. Kwa utaratibu huu itabidi Serikali ikae chini na Wadau wote wanaohusika na usafiri ili muafaka upatikane.
 
Wamiliki punguzeni hela ya makusanyo ya siku.
Pia bei ya mafuta ipunguzwe ili tuweze kufikia malengo.
 
...Tatizo linakuwa kwa abiria was vituo vya njiani!
Wakiifuata sheria hiyo basis abiria wengi was vituo vya katikati hawatasafiri...ushahidi kamili kuwa mabasi bado in machache sana jijini...!!!
Level seat kwa daladala za Dar mmh haiwezekani, kuna kipindi walileta hii sheria ila iligonga mwamba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uganda wamepiga marufuku kwa wiki 2 usafiri wa umma,boda boda na mambo kama hayo.
 
Sasa Kama daladala zikijaza bado raia wanapelea kusafiri hii SI italeta tatizo upya?,au ratiba zibadilike,daladala zianze kazi saa Tisa usiku mpaka saa Saba usiku na nauli ipande kidogo,maana level seat kea nauli ya Sasa,watu watapack magari tu
Mkuu kwa dar, daladala zinakesha , zipiga kazi 24 hours, labda kwa mikoani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunasubiri tamko moja tu la kila atulie nyumbani kwake hakuna kutoka nje/kuzurura hili la kuzuia msongamano kwenye madaladala kulikontroo ni vigumu
 
Unaenda mjini kufanya Nini?
Vyuo vimefungwa,shule zimefungwa.

Level seat kwa daladala za Dar mmh haiwezekani, kuna kipindi walileta hii sheria ila iligonga mwamba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…