Mary Chatanda awashauri wanawake kuwapa ngono waume zao ili wamkubali Rais Samia

Mary Chatanda awashauri wanawake kuwapa ngono waume zao ili wamkubali Rais Samia

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
1,242
Reaction score
4,813
Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake wa CCM (UWT), Mary Chatanda leo Oktoba 28, 2023 alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara eneo la Darajani Mjini Magharibi Unguja amesema

Mumeo akija mpokee mwambie pole mzee na kazi, mwambie tunamtaka Samia na Mwinyi. Ukiona anakuwa mgumu msubiri saa 11 asubuhi. Ukiona anakuwa mgumu msubiri saa 7 mchana akiwa mgumu msubiri jioni,"

20231029_092215.jpg
 
Ukiwa kiongozi halafu ukaona unapigiwa kampeni kibao miaka miwili au mitatu kabla ya uchaguzi ujue hutakiwi na mfumo huo uliokuweka!!

"Mimi ndio baba yako niliyekuzaa"kauli kama hii ya Baba kwa mtoto ikiwa inajirudia ujue Baba ana mashaka na mtoto kuwa si wake!!!

Marehem nae aliekua hivi hivi Kila mtu akimpigia kampeni kuwa amepita na kweli akapita akapitiliza hadi kwa mwenyezi!!

Wenye mamlaka kemeeni hiki kinachoendelea huo ni uchuro kwake,na yeye akanushe aseme tuchape kazi coz ya 2025 Mungu ndio mpangaji na chama kitafanya tathmini juu ya awamu ya sita!!!

Naendelea kuandika kwa unyenyekevu na adabu!

Mungu ibariki Tanzania!
 
Kaongea kitu cha kawaida sana tena kilichosheheni tafsida ila kwa nongwa zenu mnatafsiri ndivyo sivyo,

kwani kuna ubaya gani ukisubiri mtu asubuhi saa 11 na umueleze tena???

Nani asiyejua kazi zinachosha mtu umetoka kwenye foleni huko halafu unaletewa habari za uchaguzi, lazima somo likuingie saa 11 asubuhi

Kwa kifupi 2025 mwendo ni mmoja tu. . . . . Chama pendwa Mbele kwa Mbele🔥🔥🔥
 
Back
Top Bottom