Mary Claire: Sikumlazimisha anilipie ada na sikujua kuwa ameoa

Mary Claire: Sikumlazimisha anilipie ada na sikujua kuwa ameoa

Mwanaume anajua anachotaka, anajua kwanini anatoa pesa. Iwe kwa nia njema au ovu anajua yeye, Mwanamke ndo anayezila hizo pesa, yeye ndo alitakiwa achange karata zake vizuri. Unakula tu hujui unakula nini? Hujui nia ya anayekulisha? Ukilishwa na jini mnyonya damu?

Haya sasa karata zimechangwa na tindikali.
Jamaa hajui kuachika.
 
Mwanaume ndio alitakiwa achange karata zake vizuri. Unajua umeaoa halafu unaenda kumsomesha binti mwingine, hujiulizi tu kuwa binti akishamaliza akawa na uhitaji wa kuwa na familia yake we msomeshaji utawekwa upande gani??

Hii ni ujinga mnatetea.
Hahaha. Hautujui vizuri wanaume wa Kitanzania mkuu. Unashangaa kusomesha. Mwanaume wa Kitanzania anamchukulia mchepuko kama ni mke wake wa pili. Anaweza ua mtu kwa ajili ya mchepuko.
 
Hoja sio mwanaume aliamini nini, anaweza kuamini chochote maana ni mlipaji. Hoja ni unalipiwa ada ukiamini nini? Kwa utaratibu upi? Kuna taratibu za mchumba kufahamika mkalipiana ada.


Unamaanisha mwanaume akiwekeza uwe kimada wake unakuwa na haki ya kupokea uwekezaji ila wajibu wa kuwa kimada wake huna? Ndo nyota ya tindikali inavyoanzaga.


Alifata utaratibu wa kupewa hiyo title ya "future husband" au walipeana ada gizani wazazi hawajui?

Kila siku watu wanalaghaiwa na kutapeliwa. Tamaa imeleta tindikali.

Maybe Yes, maybe not. Asingekula pesa zake isingekuwa na maana hiyo nia yake.

Hicho ni kichaka. Unagunduaje usabato wa mwenzako baada ya kula pesa zake? Mbona hukuugundua kabla hujazila?

Tamaa haina utetezi. Ada ilikuwa tamu, utamu wa gizani sasa umekuja hadharani ukiwa na machungu ya tindikali.

Kama hutetei basi wahimize wasizile ili wasimwagiwe tindikali. Wale pesa zenye utaratibu rasmi.

Unadhani mhalifu alikuwa anaogopa kesi? Ni tukio la kwanza mwanaume hata kuua sababu ya uwekezaji kwenye mapenzi?

Hili halina msaada kwa mwanamke mwenye tamaa ya kula vya wanaume.

Pesa za wanaume hazina mwisho mzuri. Kama umezila ukapona, achana na hiyo tabia. Leo ni hadithi ya msabato, kesho hatujui itakuwa ya nani.
Hivi unavyoenda kuinvest kwa mtu ambaye unajua kabisa hawezi kuwa na wewe unakuwa una maana gani? Kwa vile kuna walio ua basi vijana waendelee kuinvest tu kwa sababu ukikataliwa kuna option ya kuua au kumwagia tindikali?

Nani kasema dada aligundua usabato baada ya kula hela?

Talking of utaratibu, hiyo pesa ilitolewa kwa utaratibu gani na mdada alitakiwa aipokee kwa utaratibu upi?

Suppose umepeleka mahari ukweni na wakwe wamepokea ila baadae wanagundua kuwa umeoa huwezi kufunga ndoa na binti yao wakaamua kukunyima mke.........utaenda kuwamwagia tindikali simply because walipokea hela yako? Would it be the best recourse?

BTW; mwanaume kujua anachokitaka sio guarantee kwamba apate kila anachokitaka. Vijana wajifunze kujicontrol. The fact kwamba imemtokea msabato na kesho hatujui itatokea kwa nani....sio sifa. Kwa sababu hata victim anaweza kuishi na kisasi na akaja kumfanyia kijana kitendo kama alichomfanyia au pengine hata cha kinyama zaidi.
 
Hapana ila nitajiandaa kwa lolote! si kila biashara inafanikiwa!

Wewe una mke, unaenda somesha binti mwingine ili iweje?

Kwanini umsomeshe mtu wakati una mke wako?

Nimekuelewa
Asande kushukuru!
Kawaida mwanaume kuoa zaidi ya mke mmoja, na mwanamke kulewa wengi na mume mmoja IPO sehemu nyingi tuu duniani.
 
Hahaha. Hautujui vizuri wanaume wa Kitanzania mkuu. Unashangaa kusomesha. Mwanaume wa Kitanzania anaamini mchepuko ni mke pia. Anaweza ua mtu kwa ajili ya mchepuko
Waache kuamini hivyo, maisha yana option nyingi zenye faida. Hapa ni wazazi/ndugu wa kijana ambao they can tell ni shida kiasi gani wanapitia kumnusuru kijana wao na jela.

BTW, humu si huwa mnaambizana mchumba hasomeshwi, vipi tena mnamtetea kijana?
 
hilo jina mary claire nikadhani ni mdada wa kizungu, kumbe mmatumbi mweusi
 
Hivi unavyoenda kuinvest kwa mtu ambaye unajua kabisa hawezi kuwa na wewe unakuwa una maana gani? Kwa vile kuna walio ua basi vijana waendelee kuinvest tu kwa sababu ukikataliwa kuna option ya kuua au kumwagia tindikali?

Nani kasema dada aligundua usabato baada ya kula hela?

Talking of utaratibu, hiyo pesa ilitolewa kwa utaratibu gani na mdada alitakiwa aipokee kwa utaratibu upi?

Suppose umepeleka mahari ukweni na wakwe wamepokea ila baadae wanagundua kuwa umeoa huwezi kufunga ndoa na binti yao wakaamua kukunyima mke.........utaenda kuwamwagia tindikali simply because walipokea hela yako? Would it be the best recourse?

BTW; mwanaume kujua anachokitaka sio guarantee kwamba apate kila anachokitaka. Vijana wajifunze kujicontrol. The fact kwamba imemtokea msabato na kesho hatujui itatokea kwa nani....sio sifa. Kwa sababu hata victim anaweza kuishi na kisasi na akaja kumfanyia kijana kitendo kama alichomfanyia au pengine hata cha kinyama zaidi.

Utaandika mambo mengi sana ila dawa ya kukwepa tindikali, visu, kubwakwa, kuuwawa unaijua, sasa we kuwa na maujanja ujanja mengi.
 
Mary Claire binti Aliye mwagiwa Tindikali na aliye kuwa mchumba wake aliye Msomesha amefunguka kuwa,

“Sikuwahi kumuomba huyo mwanaume anilipie ada ya shule. Ni yeye mwenyewe aliniomba nimpe maelezo ya akaunti ya shule, nikampa bila kujua kuwa angeanza kulipa ada. Nilijaribu hata kumzuia, lakini aliniambia ananipenda sana na yuko tayari kunifanyia chochote.

Katika kipindi chote tulichokuwa kwenye mahusiano, hakuwahi kuniambia kuwa tayari ameoa, na pia sikuwahi kumuona na mke wake. Baada ya kugundua kuwa ameoa, nilimweleza wazi kuwa siwezi kuendelea na mahusiano hayo, ndipo nikaamua kuyavunja.

Baada ya hapo, Elvis alianza kunitishia kwa hasira, na sasa hali imefikia hatua ya kutaka kuniangamiza, Ningependa kutoa wito kwa wanaume, mwanamke akikataa kuwa na wewe, muache na uendelee na maisha yako hata kama amekula pesa zako unaweza kupata zingine”
Chai
 
Ushauri:
Humtaki mwanaume usile pesa zake. Hakuna amani kwenye unyang'anyi, kichaka cha alitoa mwenyewe huwa hakisaidii. Humtaki mwanaume usile pesa zake. Ziogope kama ukoma. Kula pesa za umpendaye.
Prof Assad kasema wanawake wale pesa za Baba zao na kaka zao tu.
 
Kumwagia tindikali huyo dada ni matokeo ya ujinga wake mwenyewe. Unatoa kitu you cannot afford to loose.
Huyo kaka alitaka nini labda? Kwamba binti akimaliza chuo ataendelea kuliwa nae as kimada for the rest of her life? Yaani alitegemea binti ange sacrifice maisha yake yote, angekataa hata wanaotaka kumuoa only to remain as his concubine kwa vile tu alilipiwa ada? Is it possible??
Sitetei dada kula hela ya watu ila mambo mengine ni ujinga wa mwanaume mwenyewe. Wewe utatakaje kitu alafu ulazimishe kiwe ilihali kinategemea maamuzi ya mwingine?
Mkiwalea mabinti zenu kwa kuwaaminisha mbadala wa pesa ni mbususu, yakuwa hata akilipiwa ada akishatoa mbususu hadaiwi mabint zenu watafanyiwa ukatili wa kila aina

Wafunzeni mabinti zenu kubana mbususu wasitoe kwa namna yoyote ile hadi waolewe pia wasipokee zawadi ya aina yoyote ile kutoka kwa mwanaume kama mwanaume anataka kutoa zawadi aende kwa wazazi wake akatoe huko sio kupokea zawad gizani
 
Back
Top Bottom