Mary Claire: Sikumlazimisha anilipie ada na sikujua kuwa ameoa

Mary Claire: Sikumlazimisha anilipie ada na sikujua kuwa ameoa

Waache kuamini hivyo, maisha yana option nyingi zenye faida. Hapa ni wazazi/ndugu wa kijana ambao they can tell ni shida kiasi gani wanapitia kumnusuru kijana wao na jela.

BTW, humu si huwa mnaambizana mchumba hasomeshwi, vipi tena mnamtetea kijana?
Yaliyomtokea Claire ni ushahidi kwamba bado tuna safari ndefu. Itachukua muda sana kwa wanaume wengi wa Kitanzania kuondokana na fikra ya kwamba mwanamke unayelala naye ni "mali" yako. "Mchumba hasomeshwi" ni kauli mbiu ambayo wengi bado hawaitekelezi.
 
Wanaume sisi ni wajinga sana kwenye mapenzi.

Tunasomesha sio kwamba tunapenda sana wapenzi wetu wawe na elimu, hapana. Tunasomesha kuongeza ushawishi ili tupendwe, tunasomesha ili kuweka mipaka mwanamke awe wa pekeyetu.

Sasa kama wewe unaweka ada mezani ili mwanamke ashawishike kubaki kwako, akija mwingine ana mentality kama yakwako akaweka nyumba na gari kwa huyo binti, utamlaumu binti akikukataa?
Swadakta jamaa alikuwa ananunua mapenzi sio akili zake anaendeshwa na hisia ila pamoja na hayo inaonekana mwanamke alikuwa na majibu ya shombo kwa mwanaume ndio maana yametokea yote hayo.
 
Suppose umepeleka mahari ukweni na wakwe wamepokea ila baadae wanagundua kuwa umeoa huwezi kufunga ndoa na binti yao wakaamua kukunyima mke.........utaenda kuwamwagia tindikali simply because walipokea hela yako? Would it be the best recourse?
Ukitoa mahari halafu wazazi wakatae kukuoza wanapaswa kurudisha mahari na lazima mahari irudishwe kwahiyo huyo binti alipogundua jamaa kashaoa alipaswa arudishe ada alizolipiwa
 
Mary Claire binti Aliye mwagiwa Tindikali na aliye kuwa mchumba wake aliye Msomesha amefunguka kuwa,

ā€œSikuwahi kumuomba huyo mwanaume anilipie ada ya shule. Ni yeye mwenyewe aliniomba nimpe maelezo ya akaunti ya shule, nikampa bila kujua kuwa angeanza kulipa ada. Nilijaribu hata kumzuia, lakini aliniambia ananipenda sana na yuko tayari kunifanyia chochote.

Katika kipindi chote tulichokuwa kwenye mahusiano, hakuwahi kuniambia kuwa tayari ameoa, na pia sikuwahi kumuona na mke wake. Baada ya kugundua kuwa ameoa, nilimweleza wazi kuwa siwezi kuendelea na mahusiano hayo, ndipo nikaamua kuyavunja.

Baada ya hapo, Elvis alianza kunitishia kwa hasira, na sasa hali imefikia hatua ya kutaka kuniangamiza, Ningependa kutoa wito kwa wanaume, mwanamke akikataa kuwa na wewe, muache na uendelee na maisha yako hata kama amekula pesa zako unaweza kupata zingineā€
Wa wapi huyo Mary Claire?
 
Wakati wa kulipiwa ada hujui kama kaoa ukimaliza tu shule unagundua.

Jitahidini sana kumchunguza mwanaume kabla hujakubali akugharamikie kwa kiwango kikubwa. Hakunaga pesa za bure. Mtatolewa makafara.

Wanaume, mabinti zetu tuwaambie. Usikubali kugharamikiwa bila kujiridhisha na anayekugharamikia kwamba umempenda na una future naye. Aje kwenu kujitambulisha. Maadili yazingatiwe. Pesa iheshimiwe.
Huyo mwanamke alivyomaliza chuo huenda alitoa majibu ya shombo na kama alimkataza kulipia ada baada ya kuombwa control namba kwanini zile pesa za mzazi wake za ada kwanini asizitume moja kwa moja kwa jamaa
 
Wakati analipa ada alimini kuwa dada anauza future yake sio?
Wakati unatoa kugharamia make sure your intention is pure as well. Sio baadae tunaanza kuleteana makando kando. Dada alikubali kugharamiwa na boyfriend wake (future husband) na sio mume wa mtu......masuala ya mume wa mtu yamekuja in between..... ulitaka afanyeje?

Makubaliano yoyote yanayojengwa kwa ulaghai hayo sio makubaliano na yanafaa yavunjwe no matter how huge the investment is.
Mkaka alikuwa na nia ovu from the beginning. Yeye ni msabato ana mke na mtoto, lakini bado anaenda kuiengage na mwanamke mwingine (the victim) ambaye na yeye pia ni msabato ilhali akijua wazi kabisa yeye mkaka dini yake haimruhusu kuwa na wake wawili na binti pia hatokubali kuwa mke wa pili. Na ili ku cover uhalifu wake kwa ujinga wake bado akawa analipa ada! Yaani unafanya mtihani si grade yako alafu ukifeli unaanza kulaumu watu!
Aiseee peleka mboga pale unapoona utakula bila masimango.

N:B Sitetei binti kula hela ya mtu ila ujinga wa mtu usiwe lawama kwa mwingine. Huyo binti angekufa ingekuwa ni murder case. Au ni faida kwenda jela ukaacha familia yako inateseka only kwa ujinga wa kulipa kisasi?
Waambieni wadogo zenu wawe makini. Kuna wanyonge kama Mary Claire mtawamwagia tindikali ila pia kunao watakula pesa zenu, watawaacha na hamtawafanya chochote!
Unatetea ujinga somehow mdada kasema hampendi mshikaji na kingine anasema kwamba mwanaume alikuwa na mke how come ?mwanamke anatamaa sanaa hakika matokeo yake ameyaona na hii ni kwa wanawake wote kama humpendi tembeza kwato kwingine acheni hizo mbanga za kula pesa za usimpenda na huna future nae .
 
Kwanini asomeshe binti mwingine hilo ni lake binafsi hatuwezi jua sababu, hivyo hatuwezi kumsemea.

Kuhusu kujiandaa kwa lolote ni kweli kiasi ila utmost tunategemea kupata faida kwasababu ndio LENGO KUU.
Kosa letu ni kusikiliza upande mmoja na kutoa maamuzi.

Kama haijakupata huwezi fikiria.

Hawa mabinti huwa wanabadilisha maneno.

Naamini Hasira za kijana pengine zilitokana na tabia zao za kulazimisha, wakati mwingine huna hela ila yeye atalazimisha; meseji kila dakika za ada; matishio kama yote mpaka unakopa ili umridhishe. Amemaliza chuo, anasema nimepata mwingine hata bila kukuandaa.

Kwa sisi wazoefu, huwa hatutoi mtaji (maana mtaji unauma ajabu) tunatoa hela ya ziada ambayo hata mkiachana kesho haikuumi. Pili lazima na wewe uwe na ubinaadam; umeoa na yeye akipata wa kumuoa, mwachie asambae kwa salama. Wewe njia ya kufanya ni kutafuta kisu kingine umri wa chini yake. Maisha yanasonga.
 
"Ningependa kutoa wito kwa wanaume, mwanamke akikataa kuwa na wewe, muache na uendelee na maisha yako hata kama amekula pesa zako unaweza kupata zingineā€

MJINGA KWELI HUYU, ATI UNAWEZA KUPATA ZINGINE.
MWISHO WA UTAPELI NI MAUMIVU, AHSANTE ELVIS.
 
Amemwagiwa tindikali maeneo gani ya mwili? na huyo baradhuli amekamatwa? Yani mtu ameoa na bado analazimisha kulipia ada mabinti wa watu anakataliwa anamdhuru hilo lishamba la wapi? limeshakamatwa? na lenyewe limwagiwe tindikali kwenye korodani zake, shwaaain!
Mtajamba sanaaaa.
 
Mary Claire binti Aliye mwagiwa Tindikali na aliye kuwa mchumba wake aliye Msomesha amefunguka kuwa,

ā€œSikuwahi kumuomba huyo mwanaume anilipie ada ya shule. Ni yeye mwenyewe aliniomba nimpe maelezo ya akaunti ya shule, nikampa bila kujua kuwa angeanza kulipa ada. Nilijaribu hata kumzuia, lakini aliniambia ananipenda sana na yuko tayari kunifanyia chochote.

Katika kipindi chote tulichokuwa kwenye mahusiano, hakuwahi kuniambia kuwa tayari ameoa, na pia sikuwahi kumuona na mke wake. Baada ya kugundua kuwa ameoa, nilimweleza wazi kuwa siwezi kuendelea na mahusiano hayo, ndipo nikaamua kuyavunja.

Baada ya hapo, Elvis alianza kunitishia kwa hasira, na sasa hali imefikia hatua ya kutaka kuniangamiza, Ningependa kutoa wito kwa wanaume, mwanamke akikataa kuwa na wewe, muache na uendelee na maisha yako hata kama amekula pesa zako unaweza kupata zingineā€
haijakamilika hii habari kwa kweli
 
Hapana ila nitajiandaa kwa lolote! si kila biashara inafanikiwa!

Wewe una mke, unaenda somesha binti mwingine ili iweje?

Kwanini umsomeshe mtu wakati una mke wako?

Nimekuelewa
Asande kushukuru!
Kwani mwanaume anatakiwa aoe wanawake wangapi?
 
Back
Top Bottom