Pamoja na kazi nzuri wanayofanya vijana wetu, niliwahi kupendekeza hapa kuwa....
Kwa kuwa kitengo cha kurusha mabomu ni muhimu sana kwenye VITA
Kwa kuboresha, wasisahau pia kuchukua vijana waliosoma Physics kidato cha sita (A-Level) kwani hao wakipikwa vizuri kijeshi, wanaweza kufanya kazi nzuri sana na ya kitaalam kwani topic ya hesabu za projectile nk wanakuwa tayari wameshasoma vizuri huko shuleni.
Kwa kufanya hivyo vita inaweza kupigwa kwa gharama nafuu na madhara kidogo kwani usahihi (accuracy) ya kurusha mabomu itaongezeka sana...... Mfano; mahala wengine wamerusha mabomu ishirini, mtaalam anaweza kurusha pengine matano tu na yawe na ufanisi zaidi ya hayo ishirini....
Na ndio sababu unaweza kusikia baadhi ya Nchi zilizoendelea zinajisifia kuwa, zina Jeshi dogo ila mahiri kwa kila idara...