Mashambulizi ni makali mno nchini Congo kati ya Jeshi la wananchi wa Tanzania eneo la goma

Magical power

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2022
Posts
2,158
Reaction score
5,626
Mashambulizi ni makali mno nchini Congo kati ya Jeshi la wananchi wa Tanzania eneo la goma jeshi la wananchi JWTZ limepoteza Askari wawili huku M23 wakishindwa kusonga mbele kutokana na mashambulizi mazito ya JWTZ yakiendelea idadi ya Askar wa M23 waliofaliki katika mashambulizi hayo imewekwa kapuni na msemaji wa jeshi la waasi M23.
 
Tatizo M23 wanajificha nyuma ya kivuli cha raia kwa vile wanajua mission ya JWTZ ni ya kulinda raia, sio kushambulia raia.

Itolewe amri ya raia wote kutoka hapo Goma kwa muda wa week 2 alafu wabaki wanaume kwa wanaume uone M23 watavyoomba poo kabla ya week kuisha.
 
Wanashambulianaje hapo wakati mimi naona wamesimama tu huku mmoja akionekana kama anapita kuwapa mikono wenzake?
 
Yaliyopatikana baada ya JWTZ kuwachakaza vibaya M23. Ilikuwa hatari eneo la Sake nchini DRC, picha za maiti na vifaa vya M23.

Congo ipo katika vita endelevu dhidi ya maharamia wa M23 ambao wanatishia kuuteka mji wa Goma. Jeshi la Kongo FARDC likishirikiana na Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ kwa anuani ya SADC, walishambulia eneo la vilimani katika mji wa Sake ambapo M23 walikuwa wakijificha kwa kujibu mashambulizi.
 
Pamoja na kazi nzuri wanayofanya vijana wetu, niliwahi kupendekeza hapa kuwa....
Kwa kuwa kitengo cha kurusha mabomu ni muhimu sana kwenye VITA
Kwa kuboresha, wasisahau pia kuchukua vijana waliosoma Physics kidato cha sita (A-Level) kwani hao wakipikwa vizuri kijeshi, wanaweza kufanya kazi nzuri sana na ya kitaalam kwani topic ya hesabu za projectile nk wanakuwa tayari wameshasoma vizuri huko shuleni.

Kwa kufanya hivyo vita inaweza kupigwa kwa gharama nafuu na madhara kidogo kwani usahihi (accuracy) ya kurusha mabomu itaongezeka sana...... Mfano; mahala wengine wamerusha mabomu ishirini, mtaalam anaweza kurusha pengine matano tu na yawe na ufanisi zaidi ya hayo ishirini....
Na ndio sababu unaweza kusikia baadhi ya Nchi zilizoendelea zinajisifia kuwa, zina Jeshi dogo ila mahiri kwa kila idara...
 
Loh, naona silaha nzito hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…