Masheikh mliosoma dini na kupata nyadhifa katika jamii acheni tabia ya kuchanganya dini na uganga/uchawi

Tunguli ni nini, mitishamba!?..kama ni mitishamba,kuna tofauti gani kutibu mafua kwa viks kingo na kutibu tumbo kwa majani ya mpera!?
aliyesema kuhusu tunguli anajua zaidi..tumsubiri
 
Naomba ushahidi wa kimaandiko kuwa majini ni malaika walioasi? kutoka katika biblia au quran, chagua wewe.
 

Kuna mambo ambayo nakubaliana na wewe. Mfano, Mungu anaweza kuruhu/kuachia wachawi wakupige kipapai au azuie.
Swali dogo, Je kuna majini mazuri?? Kama ni mazuri, mazuri kwa nani?
 
Kwenye uganga unakuta mtu anaweza kujua kiarabu kidogo cha kujua kusoma na akaweza kusoma Qur'an basi hahitaji kusoma mambo mengine zaidi wala kuwa mjuzi sana wa Qur'an, sasa mtu kama huyo ndio utasema kasoma sana dini? Sasa sijui wewe uliposema kusoma sana ulitumia vigezo gani.

Mkuu naona unashindwa kuelewa unadhani uchawi unafanywa na wale wenye kuwaanga tu usiku au tiba ya uchawi ya uchawi hufanywa na waganga tu, sio lazima hadi uwe mchawi ndio uwezome kumroga mtu au kwamba huwezi kutibu uchawi mpaka uwe mganga.

Sasa sijui kama umesoma hicho nilichokuwekea maana kama ungesoma ungeona inaelezwa ukitaka kufanya nini utumie zaburi mstari gani na uitumie vp sasa nashangaa tena unakuja kuuliza zaburi gani mara sijui wachawi wanatumiaje Zaburi.

Mimi sijasema kwamba biblia imeelekeza kutumia zaburi katika uchawi au kuagua, ila nimekujuza kwamba watu hutumia hata maandiko ya biblia kwenye uchawi au kuagua na nimesema uchawi ni maneno hivyo haijalishi watahusisha maneno kutoka kwenye biblia au quran.

Sasa ukikazana kusema biblia haijaelekeza hivyo mimi hata sipingani na wewe kuhusu hilo.
 
Kuna mambo ambayo nakubaliana na wewe. Mfano, Mungu anaweza kuruhu/kuachia wachawi wakupige kipapai au azuie.
Swali dogo, Je kuna majini mazuri?? Kama ni mazuri, mazuri kwa nani?
Wako majini wazuri na wako wabaya exactly kama binadamu. Mimi na jua wako watu walitajirika kwa kufuga majini na walipo kufa watoto wao hawakujua masharti ya hayo majini yakawafilisi. Kwa ujumla mimi huwa siamini chochote zaidi ya Allah basi.
 
Naomba ushahidi wa kimaandiko kuwa majini ni malaika walioasi? kutoka katika biblia au quran, chagua wewe.

Majini ni mashetani. na mashetani ni malaika walioasi. Ufunuo 12 : 7 - 9
 
Mkuu wakati wewe una staajabu kuwepo majini wazuri na waislamu wanastaaju kuwepo malaika ambao wanamuasi Mungu, kwa maana wakati wewe unaona haiwezekani miongoni miongoni mwa kundi la malaika waliyoasi kuwepo wazuri na waislamu wanaona haiwezekani malaika kuweza kumuasi Mungu.
Shida ya kwanza inaanzia hapo.

Jambo lengine kwenye uislamu majini ni kama binaadamu tu kwa maana kuna muda hufanya mema na kuna wakati hukosea ni tofauti na sifa za malaika, kwahiyo inawezekana ukawapata wenye kufanya mema na ambao hutenda maovu maana ni kama binaadamu.
 
Wako majini wazuri na wako wabaya exactly kama binadamu. Mimi na jua wako watu walitajirika kwa kufuga majini na walipo kufa watoto wao hawakujua masharti ya hayo majini yakawafilisi. Kwa ujumla mimi huwa siamini chochote zaidi ya Allah basi.

Okay naweza kukuelewa sasa, kwa hiyo jini akikusaidia jambo lako liende sawa, basi huyo jini ni mzuri (kwako). Lakini mwingine akitumia jini kumdhuru mwingine kwa faida yake, basi aliyetumia jini atakuwa anamuhesabia jini wake kama jini mzuri na yule aliyedhuriwa anamuona jini mbaya, ndivyo ilivyo?
 

Asante kwa kunipa elimu mpya.

Kulingana na Biblia, malaika walioasi walifukuzwa pamoja na kiongozi wao. Hivyo mbinguni hakuna uasi tena.
Naomba kwa ufupi unijibu hili kulingana na imani.kitabu chako, Je shetani alikuwa muovu tangu kuumbwa kwake?
 
Nitajie mganga mmoja ambaye una uhakika haijui Quran kiwango cha kuitwa msomi wa Quran.
Mimi naamini wote ni wasomi wazuri kabisa.
Mkuu naona unashindwa kuelewa unadhani uchawi unafanywa na wale wenye kuwaanga tu usiku au tiba ya uchawi ya uchawi hufanywa na waganga tu, sio lazima hadi uwe mchawi ndio uwezome kumroga mtu au kwamba huwezi kutibu uchawi mpaka uwe mganga.
mtaje mtu asiye mchawi anayeroga,kuhusu kuagua sina shida,ndio maana nikasema wanakuwa waganga sio wachawi,yeyote anayetibu anakuwa mganga.
Sasa sijui kama umesoma hicho nilichokuwekea maana kama ungesoma ungeona inaelezwa ukitaka kufanya nini utumie zaburi mstari gani na uitumie vp sasa nashangaa tena unakuja kuuliza zaburi gani mara sijui wachawi wanatumiaje Zaburi.
bahati mbaya hujui wala huwezi kuhisi unajadili na mkristo wa aina gani,unafikiri ugumu wa kusali novena ungezingatiwa ikiwa kuna verse moja au mbili za kusoma ktk zaburi ili umshtakie mtu kwa Mungu???
ndio maana yake,ukisikia mtu anakwambia nazi inatumika kwenye maandalizi ya chai unajua tu huyu aliona maziwa akadhani ni nazi,matumizi ya kitu sehemu yanatokana na uhitaji wake sio maamuzi tu.
Sasa ukikazana kusema biblia haijaelekeza hivyo mimi hata sipingani na wewe kuhusu hilo.
Biblia haijaagiza,hata anayefanya anajua anacheza mluzi anaopiga mwenyewe,lakini Quran inaagiza kabisa,kwanini wanaoisoma wasiwe wataalamu wa field hiyo??
 
Hapana jini mzuri hakudhuru kama binadamu mzuri hakudhuru, kuhusu yule mzee aliye fuga majini alitajirika na alipo fariki walifilisika si sababu wale majini walikuwa wabaya kuna masharti wale watoto hawakujua ndio wakafilisika. Baba yao alikuwa akichinja mara kwa mara wale watoto walikuwa hawachinji navyo sikia majini wanataka na wao msosi au wanywe damu hapo sijui Allahu ya Alam mimi sina experience na hayo nimesikia tu.
 

Interesting story.
 
Asante kwa kunipa elimu mpya.

Kulingana na Biblia, malaika walioasi walifukuzwa pamoja na kiongozi wao. Hivyo mbinguni hakuna uasi tena.
Naomba kwa ufupi unijibu hili kulingana na imani.kitabu chako, Je shetani alikuwa muovu tangu kuumbwa kwake?
Unamkusudia Ibilisi ambaye kwa mafundisho ya kiislamu alikuwa jini, na hakuwa muovu alipoumbwa ila baada ya kuasi ndipo akaitwa shetani.
 
Majini ni mashetani. na mashetani ni malaika walioasi. Ufunuo 12 : 7 - 9
ufunuo 12: 7-9 Hii hapo chini sijaona sehemu imetaja majini ni malaika walioasi nisaidie ku-highlight kama ipo.

7 Kisha kukazuka vita mbinguni: Mikaeli na malaika wake wakipigana na hilo joka. Joka nalo pamoja na malaika wake likapigana nao.
8 Lakini joka na malaika wake wakashindwa, na hapakuwa tena na nafasi kwa ajili yao mbinguni.
9 Basi joka hilo kuu likatupwa nje, yule nyoka wa kale aitwaye Ibilisi na Shetani, adanganyaye watu wote ulimwenguni. Alitupwa chini ardhini, yeye pamoja na malaika wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…