Masheikh mliosoma dini na kupata nyadhifa katika jamii acheni tabia ya kuchanganya dini na uganga/uchawi

Kama umeona nimetetea ushirikina sawa mkuu, ila mie nilikuwa nakuuliza tu.
 
Majini na uisilam ni kama samaki na maji. Huwezi kutenganisha
Kwanini mkuu wakati majini si ndio walikuwepo kabla ya kuja uislamu sasa inakuaje hawawezi kutenganishwa na uislamu? Wazee wetu wa kiafrika si walikuwa wanaabudu mizimu ambayo ndio hao majini, sasa mbona majini wanahusishwa na uislamu pekee tu?
 
Kama unakubali majini, utaacha kutafuta uganga wa kienyeji
 
Mara shekhe sharif majini, Shekhe manyaunyau yan mashkhe na uganga ni pete na kidole
 
Ishu sio mganga bali maandiko ya biblia yanaweza kutumika kwenye ushirikina na mtu yeyote yule, na nimetoa mfano Zaburi hutumika sana tu kwa mambo kama hayo tena ninacho kitabu kinaeleza jinsi unavyoweza kutumia Zaburi kwa shida mbalimbali.
unafikiri kwanini waganga wengi wanatumia Quran,hasa kutoka pwani yote hii na sio zaburi kama ambayo wewe unatumia???
 
unafikiri kwanini waganga wengi wanatumia Quran,hasa kutoka pwani yote hii na sio zaburi kama ambayo wewe unatumia???
Kwanza kuna aina tofauti za uganga hivyo kama unaona inatumika sana Qur'an basi huo unaitwa uganga wa kitabu ndio utakuwa umeenea sana eneo hilo, lakini pia kuna aina zengine za uganga kama kutumia majini au mitishamba. Mimi sio mganga ila napenda kusoma kujifunza, kwahiyo kuhusu matumizi ya Zaburi hata hao waganga wengi hawajui ila kwa wenzetu wazungu hutumia sana tu huko hakuna waganga wa kutumia Qur'an.

Kuna mdada mmoja yupo Youtube ni mkristo, anafundisha jinsi ya kutumia mitishamba na maandiko ya biblia kwa shida mbalimbali za kiroho. Na anatoa huduma ya kusoma Novena yani ukiwa na shida yako hata kumuangamiza adui yako basi unamlipa anakufanyia hayo maombi.

Kwa kifupi ni mganga wa kikristo ni mtanzania kabisa, kwahiyo mkuu haya mambo sio ya kufuata kihisia hisia na kukariri.
 
Wewe ndiyo ujitambui Mungu wa Uislamu ni IBILISI NA MALAIKA WA UISLAMU NI MAJINI NA UGANGA WA KIENYEJI NI MAJINI ...HIVYO HAO MASHEKH WAOO SAHIHI KABISA KUFANYA UGANGA
Wachungaji wenu ndivyo wanavyo wakaririsha hamna mjualo zaidi ya propaganda na hampo tayari kuelimishwa
 
Kwa kweli masheikh wanaboa, mtu kiongozi wa dini unajishughulishaje na uchawi? Karibu ya wachawi wote wakubwa ni masheikh, si hajabu hii? Waislam wanajiangusha wenyewe kwa kweli.
Kuipata pepo sio kitu kidogo wengi wa waumini huendekeza tamaa za kidunia wameshapata kazi ya kupiga pesa kupitia shirki adhabu ya Mwenyezi Mungu inawangoja
 
Huwezi kutenganisha islam na hizo mbanga...

Ndio dini inanoga
Utofauti upo tena mkubwa sana ila katika kupiga vita uislam propaganda ni nyingi wale wasiojihusisha na hayo na kuhakikisha dini inafuatwa huitwa extremist au magaidi japo haipunguzi ukweli kuwa wao ndio wafuata dini ilivyo sahihi
 
Huo uganga wa kitabu ni shirki ndugu yangu kama unajifunza ili kuwa miongoni mwao acha Mara moja utaingia hasarani siku ya kiyama

Huo uganga wa miti shamba unaruhusiwa ila usihusishwe na maombezi ya kishirikina uwe ni kama dawa za hospital tu kama wale wanaouza dawa za asili

Kuna wengine hutumia Adhana kuagua hizi zote ni shirki tujiepushe nazo
 
Sasa kama dini yenu mna hadi waumini ambao ni majini yaani mnasali nayo misikitini unadhani kuna nini hapo.
Hivi yule sharifu majini bado yupo..?
 
Wazungu wa wapi,taja eneo specific.
Novena hii ni sala isiyohusisha mitishamba,zaidi ya kuisoma na kufunga tu ukiombea jambo.
na huyu dada mmoja hawezi kufanya ukafikia tamati kwamba biblia ni nyenzo ktk field hiyo.
Kwa kifupi ni mganga wa kikristo ni mtanzania kabisa, kwahiyo mkuu haya mambo sio ya kufuata kihisia hisia na kukariri.
Wala sijakariri nakwambia kitu ninachokijua,soma sana uwe mganga mzuri kama dr sure au sharif majini.
Dini yenu ni nzuri sana imekamilika.
 
Sasa kama dini yenu mna hadi waumini ambao ni majini yaani mnasali nayo misikitini unadhani kuna nini hapo.
Hivi yule sharifu majini bado yupo..?
Majini ni viumbe kama viumbe wengine aliyoumba Mwenyezi Mungu na pia wameamrishwa kumuabudu Mungu pekee bila kumshirikisha, Surat jinn Aya ya pili

72:2 - Inaongoza kwenye uwongofu, kwa hivyo tumeiamini, wala hatutamshirikisha yeyote na Mola wetu Mlezi.

Mwenyezi Mungu kakataza kushirikishwa na kiumbe yoyote aliyemuumba na huo ndio ushirikina

Surah An-Nisa (4:36)
"Na muabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote..."

2. Surah Luqman (31:13)
"Na Luqman alipomwambia mwanawe, naye anamwusia: Ewe mwanangu! Usimshirikishe Mwenyezi Mungu. Hakika shirki ni dhulma kubwa."

Katika uislam ushirikina umekatazwa na ni dhambi kubwa hao unaowaita Sharif majini ndio mada yangu imewalenga waache hiyo dhambi watubie kwa Mola wao la si hivyo itakuwa khasara kwao siku ya kiyama
 
Nachukia ushirikina yani mimi siupendi mtu anaoufanya namchukia
Ni dhambi kubwa sana kumshirikisha Mwenyezi Mungu

4. Surah Az-Zumar (39:65)
"...Kwa hakika itakapokufikia habari, ikiwa utashirikisha, hakika vitendo vyako vitabatilika, nawe utakuwa miongoni mwa wenye hasara."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…