Hata wale magaidi wanakuwa watu aina yenu! Yaani wanapewa kipande cha Aya ya Quran, nao bila kutafakari, wanatumika kupitia vipande hivyp!! Ndo kama wewe sasa!!!
Umeokoteza screenshot sijui kutoka wapi ndo tayari ushaona unaijua Quran ambayo watu wanaisoma miaka nenda rudi! Neither Quran nor Gospel inayoweza kusomwa kwa staili hiyo kwa sababu ukifanya hivyo, ndipo unaweza kukutana na aya kama hii:- Luka 19: 24-27
24 Ndipo akawaambia wale waliokuwa wamesimama karibu , ‘Mnyang’anyeni fungu lake la fedha mkampe yule mwenye kumi.’ 25 Wakamwambia, ‘Bwana, mbona tayari anayo mafungu kumi’? 26 Akajibu, ‘Nawahakikishieni kwamba, kila aliye na kitu, Mungu atamwongezea; na yule asiyetumia alicho nacho, atanyang’anywa hata hicho alicho nacho. 27 Sasa nileteeni wale maadui zangu ambao hawakutaka mimi niwe mfalme wao; waleteni hapa muwaue mbele yangu.”
Je, kwa hiyo staili yenu mtu hajaenda kuwalisha watu matango pori kwamba Bible inasema "mwenye kingi huongezewa na asiye nacho atanyang'anywa?" Na kwamba Bwana anauhusu maadui kuuawa?
Kinyume chake, ukiisoma aya hizo kwa makini unakuta aliyesema hayo kumbe sio "Bwana yule" anayefahamika na wengi kama Yesu!! Kumbe ni nukuu ya maneno yaliyosemwa na mwanadamu!!
Unless kama umeamua kupotosha kwa makusudi kama ambavyo mtu angeweza kusoma "Bwana aliagiza maadui wauawe" lakini ukweli kuhusu aya uliyoiweka mwanzoni kabisa kama 2:191 huwezi kuuelewa bila kusoma aya ya 2:190 na zingine zinazofuatia:
Ukisoma aya hizo mbili zinazofuatana utagundua kwamba kilichopo hapo ni kuji-defend! Kwamba, watu mmevamiwa, mmepigwa, na pengine wengine wameuawa na kutekwa makazi yao!!
Na ndo maana 2:190 inasema "Piganeni nao wale WALIOKUPIGENI na wala msizidishe"
Na HUWEZI kufahamu kwanini hizo aya zilikuja kwa mtindo huo bila kufahamu historia ya Muhamad na Wafuasi wake ambayo iliwafanya waikimbie hadi Mecca na kutorokea Madina baada ya kuwa kila wakati wanashambuliwa na kuuawa na hao infidels'
Now tell me: Huko mnakofundishwa upendo huwa mnafanya nini mnaposhambuliwa na kupigwa?! Huwa mnageuza shavu la kushoto kama bible inavyosema au mnapigana kama Quran inavyosema?
And remember, unapoambiwa "fight in the way of Allah" hiyo sio like any other war!!! Hiyo ni kama Wakristo mmekusanyika pale Taifa mnaanza kuhubiriana neno halafu linakuja kundi la watu na kuanza kuwatembezea kichapo! Sio kichapo cha mara moja bali hali yenyewe ndo inakuwa hivyo, inyeshe mvua, liwake jua!!!
Unataka kusema hapo Bible inawaambia "geuza shavu la kushoto?
Na kama ndivyo, vile Vita vya Msalaba vilitokea wapi?! NI Unbelievers (from Christianity PoV) wale?
Halafu haya mengine, yapunguzeni hata kwa kusoma bible yenu wenyewe!! Hebu angalia hiyo Quran 3:28 uliyoiweka hapo kisha fananisha na 2 Wakorintho 6:14 ambayo inasema:-
Hapo juu ni 2 Wakorinto 6:14. Mnaambiwaje hapo?! Au hufahamu infidel ndo hao unbelievers?! Au unataka version ya Kiswahili? Hii hapa chini:-
2 Yohana 1:9-11 nae anawaambia:-
9Mtu yeyote asiyedumu katika mafundisho ya Kristo, bali akayaacha, yeye hana Mungu. Yeyote anayedumu katika mafundisho ana Baba na Mwana pia. 10Msimpokee mtu yeyote anayewajia ambaye hawaletei mafundisho haya, wala msimkaribishe nyumbani mwenu. 11Yeyote amkaribishaye mtu wa namna hiyo anashiriki katika matendo maovu ya mtu huyo.
Tuache huu unafiki, ukweli mchungu ni kwamba, ukifuatilia maandiko ya dini zote, ni taabu tupu.