Pre GE2025 Mashekhe wafanya ibada na kuomba majini yasaidie Rais Samia kushinda kwenye uchaguzi ujao

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kabsa Mkuu! Sisi tunaomba ulinzi wa Mwenyezi Mungu! Shughuli ya Malaika Mikaeli wataisoma namba
Majini huwa yana-vibrate at a very low frequency.
Frequency ya malaika mkuu Mikaeli iki-vibrate itawatembezea kichapo majini yote ya Tanganyika na Zanzibar mpaka majini mengine yatakimbia kwenda oman kuwasimulia waarabu kichapo walichopata wenzao.
 
Mashekhe waliokutana chini ya Shekhe Mkuu Mufti Abbakari, kwenye msikiti wa kwa Mtoro, jijini Dar es Salaam wamefanya ibada maalum ya kumwombea Rais Samia ashinde kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Shekhe mkuu akiwa kwenye ibada hiyo ameagiza kuwa mashekhe wa mikoa yote, wilaya hadi kwenye kata, wafanye ibada ya kumwombea Samia ashinde kwenye uchaguzi ujao.

Shekhe mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam amesema kuwa anayaagiza majini yote yahakikishe Rais Samia anashinda kwenye uchaguzi wa urais mwaka huu.

SWALI:
Tukiyaamini maneno ya mashekhe hawa, ina maana uchaguzi wa safari hii utakuwa ni ushindani kati ya wanadamu na majini? Kama majini yakishinda, huyu Rais atakuwa wa wanadamu wa Tanzania au atakuwa Rais wa majini?

Wananchi wanapomchagua kiongozi wao, matarajio yao ni kuwa huyo wanayemchagua atawaongoza katika jitihada zao za kuyafikia maendeleo, sasa kama majini yatamchagua mgombea kuwa Rais, hayo majini yanatarajia kunufaika vipi na huyo yaliyempigania?

Wataalam wa majini tunaomba litoleeni ufafanuzi hili la mashekhe kuomba majini yamsaidie Rais Samia, inamaanisha nini katika tafsiri pana?
Ila JF kuna wana akili ajabu😂🙌🏽
 
Shekhe mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam amesema kuwa anayaagiza majini yote yahakikishe Rais Samia anashinda kwenye uchaguzi wa urais mwaka huu.
Kwa ufahamu wangu najini ni viumbe visivyopokea amri za kibinafamu.. In short wamemtapeli
Mshana Jr ninakuunga mkono!.
Ila yule aliyetoa maneno hayo ya kipumbavu ya kuwaagiza malaika na majini sio sheikh wa mkoa wa DSM.
Anaitwa Hamid Jongo ni imamu wa msikiti wa Manyema.
Kama mnakumbuka kwenye mkutano wa bunge la katiba alilia bungeni kwa kile alichodai kuwa waasisi wa Taifa (Nyerere na Karume ) wanatukanwa!.
Sheikh wa mkoa wa DSM ( bakwata ) anaitwa Walid Alhadi aliyeteuliwa kumrithi Alhadi Musa Salum aliyevuliwa usheikh wa mkoa na kubaki huko kwenye kamati ya amani na maridhiano ya wanaoitwa viongozi wa dini.
Tukiachana na hilo Mimi ni muislamu ambaye dini nimeisoma na ninakuunga mkono kwamba MALAIKA NA MAJINI HAWAPOKEI AMRI WALA MAELEKEZO YOYOTE TOKA KWA WANAADAMU.

Ila Kuna majini waovu ( mashetani ) ambao hupokea amri na maelekezo maalumu toka kwa binadamu waovu
( Wachawi na makuhani kama huyo sheikh anayedai kuchimja mbuzi na kusoma Albadiri ) chini ya mikataba na maelewano maalumu ya kumkufuru na kumuasi Mola muumba wa ulimwengu.
Shekhe mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam amesema kuwa anayaagiza majini yote yahakikishe Rais Samia anashinda kwenye uchaguzi wa urais mwaka huu.
Kwa ufahamu wangu najini ni viumbe visivyopokea amri za kibinafamu.. In short wamemtapeli
Shekhe mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam amesema kuwa anayaagiza majini yote yahakikishe Rais Samia anashinda kwenye uchaguzi wa urais mwaka huu.
Kwa ufahamu wangu najini ni viumbe visivyopokea amri za kibinafamu.. In short wamemtapeli
 
Majini huwa yana-vibrate at a very low frequency.
Frequency ya malaika mkuu Mikaeli iki-vibrate itawatembezea kichapo majini yote ya Tanganyika na Zanzibar mpaka majini mengine yatakimbia kwenda oman kuwasimulia waarabu kichapo walichopata wenzao.
Kama tu Baba yao alinyoosha mikono hawa watoto je!? Frequency ya Malaika Mikaeli ni moto mwingine
 
Mmewaona ndugu wa Damu wa majini. Uislamu bila majini haiwezekani
Kitu unacho takiwa kujiuliza ni kwa namna gani kitu kisicho onekana wala kusikika kinaweza kutumiwa kuna nguvu gani.. basi ujue yale maneno sio ya kawaida na sio ya binadamu wa kawaida..

Hata wanao jiita mashekh wanajua wazi kuwa kujihusisha na majini ni dhambi na imekatazwa.. aliye wakataza anaelewa maneno yake yana nguvu hata ya kumfanya mtu kichaa..

Au ni uchawi? 😀 kila mtu aabudu kwa imani yake sisi tuna dini yetu na nyinyi mna dini yenu na wala hatuta abudu mnacho kiabudu..

Kwishney
 
Mashekhe waliokutana chini ya Shekhe Mkuu Mufti Abbakari, kwenye msikiti wa kwa Mtoro, jijini Dar es Salaam wamefanya ibada maalum ya kumwombea Rais Samia ashinde kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Shekhe mkuu akiwa kwenye ibada hiyo ameagiza kuwa mashekhe wa mikoa yote, wilaya hadi kwenye kata, wafanye ibada ya kumwombea Samia ashinde kwenye uchaguzi ujao.

Shekhe mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam amesema kuwa anayaagiza majini yote yahakikishe Rais Samia anashinda kwenye uchaguzi wa urais mwaka huu.

SWALI:
Tukiyaamini maneno ya mashekhe hawa, ina maana uchaguzi wa safari hii utakuwa ni ushindani kati ya wanadamu na majini? Kama majini yakishinda, huyu Rais atakuwa wa wanadamu wa Tanzania au atakuwa Rais wa majini?

Wananchi wanapomchagua kiongozi wao, matarajio yao ni kuwa huyo wanayemchagua atawaongoza katika jitihada zao za kuyafikia maendeleo, sasa kama majini yatamchagua mgombea kuwa Rais, hayo majini yanatarajia kunufaika vipi na huyo yaliyempigania?

Wataalam wa majini tunaomba litoleeni ufafanuzi hili la mashekhe kuomba majini yamsaidie Rais Samia, inamaanisha nini katika tafsiri pana?
Hakuna mashehe hapo. Hao ni matapeli tu kwa mgongo wa dini. Ni wa kupuuzwa.
 
Nategemea waislamu mtaandamana Hawa masheikh kuhusisha uislamu na shirki
Ndugu yangu ni kwamba sisi waislamu tuko katika makundi na madhehebu tafauti tafauti.
Hao mashehe wanaotangaza ushirikina hadharani kama mlivyoona kwenye video wana wafuasi wao wanaokubaliana na uchawi na ushirikina wao na wengine wamonserikalini na wapo tayari kuwatetea na kuwaunga mkono kwa hali na mali.
Pili kidini maandamano sio njia sahihi ya kuondoa maovu katika jamii.
Tunaishi katika nchi inayoamini uhuru wa kuabudu kwahiyo nchi kama hii hata waabuduo shetani Wana haki ya kumuabudu shetani wao kulingana na katiba, sheria na kanuni za nchi, sisi tunaloweza ni kusema tu kwamba vitendo hivyo ni kinyume na uislamu sahihi aliofundisha mtume Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم.
 
Mashekhe waliokutana chini ya Shekhe Mkuu Mufti Abbakari, kwenye msikiti wa kwa Mtoro, jijini Dar es Salaam wamefanya ibada maalum ya kumwombea Rais Samia ashinde kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Shekhe mkuu akiwa kwenye ibada hiyo ameagiza kuwa mashekhe wa mikoa yote, wilaya hadi kwenye kata, wafanye ibada ya kumwombea Samia ashinde kwenye uchaguzi ujao.

Shekhe mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam amesema kuwa anayaagiza majini yote yahakikishe Rais Samia anashinda kwenye uchaguzi wa urais mwaka huu.

SWALI:
Tukiyaamini maneno ya mashekhe hawa, ina maana uchaguzi wa safari hii utakuwa ni ushindani kati ya wanadamu na majini? Kama majini yakishinda, huyu Rais atakuwa wa wanadamu wa Tanzania au atakuwa Rais wa majini?

Wananchi wanapomchagua kiongozi wao, matarajio yao ni kuwa huyo wanayemchagua atawaongoza katika jitihada zao za kuyafikia maendeleo, sasa kama majini yatamchagua mgombea kuwa Rais, hayo majini yanatarajia kunufaika vipi na huyo yaliyempigania?

Wataalam wa majini tunaomba litoleeni ufafanuzi hili la mashekhe kuomba majini yamsaidie Rais Samia, inamaanisha nini katika tafsiri pana?
Hali ni tete sana...
Shetani sasa anajidhihirisha namna alivyoitawala nchi hii kupitia CCM
 
Ndugu yangu ni kwamba sisi waislamu tuko katika makundi na madhehebu tafauti tafauti.
Hao mashehe wanaotangaza ushirikina hadharani kama mlivyoona kwenye video wana wafuasi wao wanaokubaliana na uchawi na ushirikina wao na wengine wamonserikalini na wapo tayari kuwatetea na kuwaunga mkono kwa hali na mali.
Pili kidini maandamano sio njia sahihi ya kuondoa maovu katika jamii.
Tunaishi katika nchi inayoamini uhuru wa kuabudu kwahiyo nchi kama hii hata waabuduo shetani Wana haki ya kumuabudu shetani wao kulingana na katiba, sheria na kanuni za nchi, sisi tunaloweza ni kusema tu kwamba vitendo hivyo ni kinyume na uislamu sahihi aliofundisha mtume Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم.
Nimekuelewa, lakini hili lingesemwa na mwngine pasingekalika.
 
Hili haliwezi kufanya waislamu wakamuwajibisha huyp sheikh jongo?? Angeweza kumpigia kampeni Samia bila kuhusisha majini na uislamu

Nategemea waislamu mtaandamana kwa hili la huyu sheikh kudhalilisha dini
Kwa desturi ya nchi yetu ni ngumu sana,watu wa namna hii wapo tayari hata kukufanyia ubaya wowote ili kulinda maslahi yake binafsi kwa sababu hata huo Uimamu wa hapo Manyema ana zaidi ya miaka 30 kwenye nafasi hiyo na hakai huko kariakoo anakaa tandika huko hapo Manyema amepafanya ndiyo kazini kwake.
Hao watu hatari sana.
 
Hii dini hii, kiongozi mkubwa wa dini anathubutu kuyashirikisha majini kwenye maamuzi ya hatima ya wanadamu, huu ni ushirikina wa wazi wazi na kufuru kubwa kweli kweli.
 
Mwenye kufahamu jina la huyu Sheikh.
View attachment 3222765
Huyu ni mpumbavu mmoja anajiuta Dr sule.
Anachozungumza siyo sahihi.
Mitume wa Allaah wamepewa miujiza ya kuweza kuongea na kuviamrisha viumbe ambavyo havisikii wala kuongea katika hali ya kawaida.
Baadhi ya mitume waliweza kuviamrisha hata miti na mawe na viumbe hivyo vikawasikiliza mitume na kufuata amri zao.
Nabii Suleiman aliwezeahwa kuzungumza na wanyama wote na alifundishwa lugha za ndege sisimizi na wanyama wengine ikiwa pamoja na mashetani na majini pia aliwezeahwa kuuamrisha hata upepo ufanye anavyotaka na upepo ulifanya.
Mtume صلى الله عليه وآله وسلم hakufuga majini ila kwa uwezo wa Allaah aliweza kuongea nao na kuwadhibiti baadhi ya majini waovu wasifanye kama kupita mbele yake akiwa anaswali na kitendo hiki ni katika miujiza aliyopewa kithibitisha utume na unabii wake na haimaanishi kwamba alifuga majini.
Tukisoma biblia hata Yesu aliyaamrisha mashetani yameache mgonjwa na yahamie kwenye kundi la nguruwe na kitendo kama hicho ni katika miujiza ya kuthibitisha utume na unabii wake na kila mtume na Nabii hupewa miujiza kulingana na hali , mazingira na watu aliotumwa kwao .
 
Back
Top Bottom