Pre GE2025 Mashekhe wafanya ibada na kuomba majini yasaidie Rais Samia kushinda kwenye uchaguzi ujao

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwa hapa waislam tumefeli na wakristo wakitusena wanakuwa kwenye haki kabisa

Viongozi wa BAKWATA ni wachumia tumbo tu hamna cha usheikh hapo

Kwanza picha linaanza huyo mufti ni Mganga na viongozi wengi wa BAKWATA ni waganga wa kienyeji


BAKWATA= CCM
 
Hali ni tete sana...
Shetani sasa anajidhihirisha namna alivyoitawala nchi hii kupitia CCM
Hawa nawaona kama makahaba wakiume wanaojipendekeza kwa mama Samia ili warambishwe asali.
Jambo ambalo mnatakiwa kujua ni kwamba viongozi wengi wa kisiasa kwa Tanzania bara ukimuondoa Mzee Mwinyi na Aboud Jumbe ( ambao ni wazanzibar ) hawakusoma elimu ya dini kabisa!. Mama Samia pamoja na kwamba ni mzanzibar lakini kwenye elimu ya dini ni mweupe!.
Sasa watu wa aina hii wanapokutana na masheikh wanaoendekeza NJAA huzidi kupelekwa gizani na viongozi hawa kwa sababu hawakupata fursa ya kusoma dini hushindwa kuelewa kuwa wanazidi kupelekwa motoni kwa dua za kumuomba shetani badala ya Allaah.
Nachotaka muelewe hapa ni kwamba wanachokifanya hawa wapuuzi wanaojifanya wasemaji na viongozi wa waislamu sio msimamo wa CCM!.
CCM ni chama cha kijamaa na HAKINA dini wala dhehebu na ndani ya CCM kuna waislamu, wakristo na hata wapagani wamo kama akina Kingunge! Kwahiyo huu uhuni uliofanywa na hao viongozi wa bakwata na huyo ibilisi anayejiita Maalim kingu isiwe sababu ya kusema CCM ni chama cha mashetani kwasababu hao hawawakilishi chama cha siasa.
Mama Samia anaweza kuwaunga mkono kutokana na unafiki wa kisiasa kama ambavyo hata walokole wakitangaza kumuombea kwa Yesu na maria wamsaidie ashinde uchaguzi pia atawakubalia kutokana na unafiki wa kisiasa.
Mabaniani wanaoabudu ng'ombe na masanamu mengine ya akina Krishna na mengine pia wakitangaza kuiomba miungu yao imuwezeshe mama ashinde uchaguzi pia mama atawashukuru.
Hizi siasa mtu akishaingia hupenda kuyaridhisha makundi yote yanayoonyesha kumuunga mkono ndiyo maana utamkuta mwanasiasa bila kujali dini yake siku ya idi atakuwa msikitini na siku ya pasaka atakuwa kanisani.
Nakumbuka Wiliamu Ruto na Rigathi Gachagua mwezi wa Ramadhani iliyopita waliingia msikitini na kusali na waislamu swala ya magharibi kisha nadhani kupata futari na waislamu na wakati huo alikuwa yupo kwenye kampeni za uchaguzi wa Kenya uliopita.
HIVYO NDIVYO WANASIASA WALIVYO.
 
Shekhe mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam amesema kuwa anayaagiza majini yote yahakikishe Rais Samia anashinda kwenye uchaguzi wa urais mwaka huu.
Kwa ufahamu wangu najini ni viumbe visivyopokea amri za kibinafamu.. In short wamemtapeli
Mkuu hao ni waganga hao

Wanamiliki mashetani maana sio majibu

Japo pia hawana uwezo huo wanaousema

Ni utapeli tu
 
Kwa hiyo kwa sasa kirefu cha CCM ni Chama Cha Majini!!
Jamani kumbukeni ndani ya CCM kuna watu wa dini tofauti tofauti pamoja na wasiokuwa na dini (wapagani )
CCM ni chama cha kijamaa ila wafuasi wao Wana dini zao.
Kesho au keshokutwa linaweza tokea kanisa linaloongozwa na askofu au mchungaji mwenye njaa zake akamuombea Mama Samia kwa iina la Yesu na maria wamsaidie ashinde uchaguzi.
Hilo likitokea haitamaanisha kwamba CCM ni chama cha kikristo.
Huu ni mwaka wa uchaguzi kwahiyo jiandaeni kushuhudia visa na vituko mbalimbali!.
Hilo walilolifanya hata kama nyinyi hamfurahii kuna wakristo wenzenu waliomo ndani ya CCM kama akina Dr Nchimbi na Paul Makonda ambao hawaoni kuwa hao masheikh wamefanya kosa lolote.
HIVYO NI MOJA YA VISA NA VITUKO VYA MWAKA WA UCHAGUZI!
 
Hapana! Kusema Bakwata ni CCM na CCM ni bakwata sio sawa!
Ndani ya CCM kuna watu wa dini na madhehebu tafauti tafauti.
Ndani ya CCM kuna waislamu kama mama Samia, Kikwete nk.
Ndani ya CCM kuna wakristo wakatoliki kama akina Dk Nchimbi, Paul Makonda nk.
Ndani ya CCM kuna wakristo wa Madhehebu mengine kama akina askofu Gwajima nk.
Kwahiyo maneno ya kihuni yaliyosemwa na hao masheikh siyo msimamo wa CCM japo CCM hawawezi kuwakataa kutokana na unafiki wa kisiasa wa kutokuwa na upande wowote na kumuunga mkono kila anayekuunga mkono.
 
Kuna kazi kubwa ya kurudisha utaifa wa taifa hili huko tuendako ...
 


Hizo sala zitafanya kazi tu kama kuna reform bila hivyo wanaombea wizi mwema😂
 
..tujiepushe kukosoa viongozi.

..mara nyingi mkiwakosoa viongozi wa dini, waumini wa dini husika huhisi mmeivunjia heshima dini yao.

..kiongozi wa dini akikosea kwa kutokujua, au kwa makusudi, ni vizuri kupotezea tu kwani watu wana akili za kujua jambo sahihi, na lisilo sahihi.
 
Masheikh tena na majini ya vitabu.....hii ni laana kwa taifa. Imagine taifa linaongozwa na majini.
 
Sijui ni kwa namna gani lakini nashawishika kukubaliana na hili usemalo
 
Kama naona Tanzania inaanza kuwa nchi iliyo chini ya majini wa vitabu
 
Ndio dini inataka hivyo.. uhuru wa kuabudu tuheshimu.
Hiyo ndio ya HAKI.
 
Jini ni kiumbe tu kama ulivyo wewe , jini na binadamu wanapomkosea Allah wanakuwa mashetani
 
CCM ndiyo Chanzo Cha Matatizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…