Mashtaka dhidi ya Kampuni za Mawasiliano yanawezekana

Mashtaka dhidi ya Kampuni za Mawasiliano yanawezekana

Tutamlipa alaf baada ya kumlipa tunamfungulia na yeye kesi ya wizi wa kuaminiwa
 
Kwani si inabidi idhihirike kama hiyo kazi ingempa 200M

Sijajua ni kazi gani, tuseme mfano ni ajira ya muda mrefu ambayo akiipata ndo mshahara wa utumishi wake ndo ungeleta hiyo 200M hadi kustaafu!
 
Labda kama kwa rushwa au kwa kushirikiana na mawakili wa Tigo, in which case, lolote linawezekana popote pale. Ila kwa court proceedings zilizonyooka, hakuna connection ya yeye kukosa kazi na hilo la kukatwa pesa, maana huwezi kuacha kazi ya milioni 200 kisa unaogopa riba ya shs.100/=, it defies logic! Hakuna jaji ambae hajala rushwa na mwenye akili timamu, atakupa ushindi

Mie nna shauri langu la simu kuhusu vifurushi Kuna mjinga mmoja alikuja humu tukampa moyo hadi kumuahidi sapoti ya chochote ili kesi ashinde sababu zilikuwa wazi cha ajabu jamaa sijui alifikia wap japo ukiwa na akili unajua

Mkuu hizi kampuni na mamlaka zinazowasimamia kuna magape mengi sana wanayaacha yan ukiwa na akili unapiga pesa ya maana kuanzia kwa mtoa huduma na msimamizi wa huduma believe anzia kwenye usafiri, makazi, mpka mawasiliano.
 
Sijajua ni kazi gani, tuseme mfano ni ajira ya muda mrefu ambayo akiipata ndo mshahara wa utumishi wake ndo ungeleta hiyo 200M hadi kustaafu!
Angekufa je? Au termination? Hiyo 200M ingepatikana?
 
Wakiwepo wabishi kama hao lazima heshima iwepo

Ova
Miaka fulani niliwahi kushitaki Baraza la mitihani Tanzania Kwa kunikosesha kufanya mtihani kama private candidate ili Hali walipokea malipo yangu na listi nilikuwa nayo, Bassi Tu Kwa vile serikali ni serikali wakanizingua kabla ya hukumu mwaka uliofuata Necta wakarejesha jina langu, hukumu ikayumbishwa eti mdaiwa alishanifidia Kwa kukubali kosa na kunipatia nafasi ya kufanya mtihani.
Ila Kwa kuwa ni serikali na mara nyingi kesi kama hizo mahakama uegemea upande wa mwajiri wao basi nikaicha kesi.
Ila hata Mimi na ubush lawyer wangu huwa nacheza Sana na opportunity, ukijichanganya sikuachi hapo naamini mushikaji alishatengeneza mazingira ya kuonyesha alisababishiwa kushindwa. Yawezekana huyu mwamba ni mwanasheria au aliitwa kwenye interview na akawa na mchongo mwingine, hivo ni rahisi Sana kujustify kuwa alishindwa kuwasiliana mteja wake.
 
Unaona sasa mzee unapoyumba? Kukopa ni lazima?

Achana na suala la kukopa. Mimi nataka utoe hukumu kwa case scenario niliyokupa hapo juu.
Kukopa si lazima kwa nani? Kwa mhusika kama kweli aliitaka hiyo kazi ya 200mil. basi alikuwa na ulazima wa kukopa, ila kwakuwa hakuitaka hiyo pesa, akaacha kukopa, huwezi kuwashataki Dawasco kwa mifugo kufa kiu kisa walikata maji, ilihali kuna bwawa la maji la kulipia lilikuwepo pemebeni na anakopesha, huo ni uzembe wako mwenyewe
 
Bro you lack objectively. Kukopa sio lazima. Na cha msingi kabisa ni kuwa hakutaka kukopa na ndio maana akawa na salio kwenye simu yake ila wakamwibia.
 
Labda kama kwa rushwa au kwa kushirikiana na mawakili wa Tigo, in which case, lolote linawezekana popote pale. Ila kwa court proceedings zilizonyooka, hakuna connection ya yeye kukosa kazi na hilo la kukatwa pesa, maana huwezi kuacha kazi ya milioni 200 kisa unaogopa riba ya shs.100/=, it defies logic! Hakuna jaji ambae hajala rushwa na mwenye akili timamu, atakupa ushindi
Kama ni muislamu safi je Riba si haramu kwao
 
Ni ngumu kupprove connection ya yeye kukosa kazi na hiyo deduction ya kimakosa, maana angeweza kuomba tena mkopo wa airtime na akawasiliana na mteja
Sio lazima kukopa wala kulazimisha mambo.Tunataka Milioni hizo sisi.Ili wawe na adabu.
 
Miaka fulani niliwahi kushitaki Baraza la mitihani Tanzania Kwa kunikosesha kufanya mtihani kama private candidate ili Hali walipokea malipo yangu na listi nilikuwa nayo, Bassi Tu Kwa vile serikali ni serikali wakanizingua kabla ya hukumu mwaka uliofuata Necta wakarejesha jina langu, hukumu ikayumbishwa eti mdaiwa alishanifidia Kwa kukubali kosa na kunipatia nafasi ya kufanya mtihani.
Ila Kwa kuwa ni serikali na mara nyingi kesi kama hizo mahakama uegemea upande wa mwajiri wao basi nikaicha kesi.
Ila hata Mimi na ubush lawyer wangu huwa nacheza Sana na opportunity, ukijichanganya sikuachi hapo naamini mushikaji alishatengeneza mazingira ya kuonyesha alisababishiwa kushindwa. Yawezekana huyu kwamba ni mwanasheria au aliitwa kwenye interview na akawa na mchongo mwingine, hivo ni rahisi Sana kujustify kuwa alishindwa kuwasiliana mteja wake.
Kabisa mkuu hatutakiwi kuwa watu wa kupelekeshwa

Ova
 
Angekufa je? Au termination? Hiyo 200M ingepatikana?

Kwenye mkataba huwa hakuna kipengere cha endapo utakufa au kufukuzwa. Tukiacha hayo, basi angalau sema ikiwa angeikosa hata hiyo kazi yenyewe…. lakini hayo yote huwezi kuyajengea hoja.

Wewe ndo umemkwamisha haijalishi jamaa angefeli usaili au vyovyote.
 
Hakuna logic ya kumlazimisha mtu kukopa wakati tayari umechukua mali yake. Kumbuka mkopo una riba hivyo kwake ilikuwa ni hasara nyingine.
Sio kwamba na hukumu, its logic, na mahakamani wanabase kwenye logic and common sense huku wakizingatia msimamo wa sheria unasemaje
 
Kwenye mkataba huwa hakuna kipengere cha endapo utakufa au kufukuzwa. Tukiacha hayo, basi angalau sema ikiwa angeikosa hata hiyo kazi yenyewe…. lakini hayo yote huwezi kuyajengea hoja.

Wewe ndo umemkwamisha haijalishi jamaa angefeli usaili au vyovyote.
Yaweza isijengewe hoja ila inatosha kufikirisha. Alijihakikishiaje kwamba ni lazima atapata 200M
 
Back
Top Bottom