Mashujaa 0-1 Simba SC | NBC Premier League | Lake Tanganyika | 1 November, 2024

Incident gani ambayo refa wa kati ameiamua au ameiacha kuamua ambayo imeenda kuipa faida Simba ya kunufaika na kupata bao?
 
We foko kweli kalilie chooni na mwiko wako huko nyuma
Bado mechi mbili tuwalipe kubebwa na refa
 
Reactions: BRN
Mkuu, umeona ubao lakini au unatype tu bila kuchungulia? πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
Mkuu hebu soma tena nimesema "LEO HATUTOSIKIA"

Yaani sababu mmeshinda ila mngefungwa au ku draw basi tungesikia hayo
 
πŸ˜…mkizubaa ile nafasi ya 3 itakua yenu
 
Incident gani ambayo refa wa kati ameiamua au ameiacha kuamua ambayo imeenda kuipa faida Simba ya kunufaika na kupata bao?
Kwanza alifunika Tuta bahati mbaya mshika kibendera Ali mpotezea maana tukio alikua ana kimbia nalo mpaka kwenye kibendera Cha Kona na presha ya wachezaji wa Mashujaa aka potezea.
Pili muda ulio simama mpira haukufika dk 6 lakini kwakua ni refa wa mfukoni akaweka dk 6.

Tatu kwenye muda wa nyongeza uwezi ukaweka nyongeza wakati mpira haukusimama.

Refa Mdoe ana tabia zote za refa wa zamani wa Mchongo Abdalah Kama mbuzi.
 
Muda uliosimama mpira wewe unaupimaje?

Ulikuwa una stopwatch pembeni pale mpira ambapo unakuwa umesimama wewe huko kwako ukawa unai stop?

Hukuona matukio ya balls boys kuacha kurusha mipira ndani ili kuchelewesha muda?

Hukuona matukio ya Kocha wa Simba akiokota mipira na kuwapa Mashujaa warushe na wao wakiwa wanajivuta kwenda kupokea mpira kwake?

Hukuona mpaka Kocha akajikuta anakasirika na kuanza kuwafokea hao wachezaji wa Mashujaa kwa ushamba waliokuwa wanamfanyia?

Hukuona kuna time hadi wachezaji wa Simba iliwabidi waende kuokota mipira wenyewe kuwapa Mashujaa ili kuokoa muda?

Hukuona mipira ya kurushwa kuelekea Simba kulikuwa na ucheleweshwaji wa kimakusudi wa muda?

Sometimes unaona mchezaji wa mashujaa anatoka eneo la mbali kwenda kurusha mpira huku akitembea taratibu na akishaufikia mpira anaunyanyua ishara ya kurusha lakini baadae anauweka chini anakuja mwingine kurusha, halafu huyu anayerusha ni mtu ambaye alikuwa karibu?
 
Mtani katoboa kwa mateso sana duh!πŸ˜‡πŸ˜‡
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…