Mashushushu wa Fidel Castro walikuwa na hisia ya sita(Sixth Sense)

Ni kweli Castro alikuwa anatembea na mwanamke mpya kila siku na harudii tena! Yasemekana alitimiza takribani wanawake elfu 30.

Anayejua atujuze juu ya hili.
 
Mmmh kwa kweli ni ushujaa ulioje!! RIP Fidel Castro.[emoji16][emoji23]
 
Umetupa habari nyeti ambayo hatukuijua ,huyu Fidel alikuwa jasusi la kimataifa hizi njama za kumuuwa zilifanywa kwa ustadi mkubwa lakini watu wake walimsaidia yeye kuwa salama.
 
Simulizi nyingine ambaye msiache kuileta humu ni ile ya ushindi mkubwa ambao Castro aliupata dhidi ya wavamizi Katika Pwani ya Nguruwe ama Bay of the Pigs mwaka 1961.
 
 
N
Kama Mungu anakujaalia Mtoto wa kiume, italeta raha kumuita majina kama Fidel au Castro. Sio Juma.


Ni kweli mkuu, Mimi mwanangu wakiume nimemuita Sankara.

Nimempa jina hilo kwasababu nilivutiwa Sana na harakati za aliyewahi kua Rais wa Burkina Faso hayati Thomas Sankara.
 
Duh...kumbe Marehemu Che Guavara alishakaa hadi Dar! Shikamoo Mkuu.
Mkuu GENTAMYCINE na habari zako za Makumbusho kweli hizi habari hukuwa unafahamu?

Che Gueavara alikaa Tz kati ya mwaka 1964-65,aliingia kwa siri japo Serikali ya Tz ilijua ujio wake.Alikaa Ubalozi wa Cuba pale Upanga akipanga safari ya kwenda Zaire kuwasaidia kina Kabila kumuondoa Mobutu.

Safari yake kwenda Zaire(DRC) ilikuwa kwa njia ya gari,alisafiri siku kadhaa mpaka Kigoma na baadae kuvuka kwa mtumbwi ziwa Tanganyika kwa kuvushwa na wavuvi bila wao kumfahamu.

Aliishi ktk kijiji cha Kibamba kilichopo mwambao mwa ziwa Tanganyika.Na alitumia jina bandia "code name" la Kiswahili,aliitwa "Tatu".

Baadae aliamua kuachana na Kabila baaada ya kukuta askari wa Kabila hawana nidhamu,kazi yao wakiteka vijiji na kuuwa watu wasio na hatia na kubaka kina mama.Walikuwa walevi hata nyakati za mapambano na wapenda ngono sana.Che akawaambia hawawezi kushinda vita kama "chakula" chao itakuwa ni pombe na wanawake.

Akaamua kuondoka,akaja Dsm,akanywa kahawa,akakaa siku kadhaa,na inasemwa alikuwa anakula chakula mara kadhaa kwenye mgahawa fulani pale Kkoo.

Aliporudi kwao,akaongoza mapinduzi ya Bolivia.Na mwisho utabiri wake wa pombe na wanawake kwa askari wa Kabila ukatimia,kwani Kabila hakumshinda Mobutu toka msituni,bali alifanikisha baada ya Mobutu kuzeeka na kukosa ushawishi.Huyu ndio Che rafiki wa Ruz Fidel Castro Le Commandet
 
fuatilia 'the magic bullet' aliyopgwa kenedy,kenedy hakupgwa risasi moja na wala oswald hahusiki
 
Umetupa habari nyeti ambayo hatukuijua ,huyu Fidel alikuwa jasusi la kimataifa hizi njama za kumuuwa zilifanywa kwa ustadi mkubwa lakini watu wake walimsaidia yeye kuwa salama.
KGB itakua walikua wakimpga tafu,kumbuka ussr walikuwa na makombora cuba kwa ajili ya kukata ngebe za marekani
 
Mwanangu wa kwanza nimempa jina fidel Castro.
Mwanangu wa pili nimempa jina Ghadafi.

Mwanangu wa tatu nimempa jina Thomas sankara.
Mwanamapinduzi halisi. Waambie wawasome hao, ili wajue kwa nini wanaitwa majina hayo.
 
Tatizo ndani ya CIA kumejazana mashushushu kibao wa Castro ambao hata kulipwa hawalipi lakini ni waumini sana wa ideology ya Castro na Cuba. Wazee na sasa wajukuuu. Hii ni problem kubwa sana Langley
 
nimejifunza mengi sanaaaaaa huu uzi ila nin SWALI
kuna movie yeyote imeshawahi tungengenezwa juu ya maisha ya fidel au che guevera?

nitarudi kuchek jibu naona mb zinakata broooo
 
Huyu mtu nampenda kuliko navyojipenda mwenyewe. Huwa nikikaa kumsoma mpaka machozi yananitoka. Kwangu mimi ni mtu ambaye ataishi daima kwenye fikra zangu siku zote za maisha yangu.
umemsoma kwenye kitabu gani mkuu na sisi tumegee kidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…