Asante De Levis. Tunahitaji wadau walete humu pia simulizi ya "The Cuban Missile Crisis 1962"
Cuban Missile Crisis ilikuwa ni pamoja na mgogoro ambao Fidel Castrol aliuanzisha baada ya Marekani kukataa kununua sukari ilozalishwa Cuba.
Hapo kabla Marekani ilikuwa ni mteja mkubwa wa sukari ya Cuba na walipoweka vikwazo vya kiuchumi ikiwemo kutonunua sukari, Fidel Castrol akaamua kuzungumza na Russia (zamani USSR) na wakaingia mkataba wa kununuliana na kuuziana bidhaa hiyo adimu.
Lakini sababu kubwa ya msingi kabisa ya mgogoro huu ni USSR kuamua kuweka mitambo ya nyuklia nchini Cuba baada ya Marekani kuweka mitambo hiyo kwenye pwani za Uturuki na Italia.
Mkutano wa siri kati ya kiongozi wa USSR Nikita Khrushchev na Fidel Castrol ulifanywa na makubaliano yalifikiwa kati ya USSR na Cuba ambapo kiongozi wa USSR Khrushchev akamuomba Fidel Castrol aweke mitambo ya Nyuklia nchini Cuba ili kuweka uwiano wa nguvu kati ya USSR na Marekani, ulikuwa ni mpango wa siri mno.
Lakini pia Fidel Castrol alikuwa kwa muda mrefu akiiomba USSR kuweka mitambo hiyo nchi kwake ili kujilinda na uvamizi wa Marekani ambao Castrol aliwaona ni maadui wake.
Na hii ilichangiwa sana na kushindwa kwa jaribio la waasi wa Cuba wakisaidiwa na CIA waliposhambulia pwani ya nguruwe au "Bay of Pigs" mwezi April mwaka 1961 na kushindwa jaribio hilo. Kuna jaribio lingine liloitwa Cuban Project Operation Mongoose lilofanywa mwezi Novemba mwaka huohuo ambalo kama jaribio la "Bay of Pigs" liliidhinishwa na raisi JF Kennedy.
Walofahamu mpango huo ni watu wa karibu kabisa na Castrol kama mdogo wake Raul, Ernesto Guevara, Dorticos na mkuu wa usalama bwana Ramoro Valdes.
Lakini Marekani kwa kutumia mitambo yake ya angani na wakagundua msafara wa meli za kivita za USSR zikielekea Cuba, na wakawa wameghadhibika na kitendo hicho Castrol akawaambia wamarkani kwamba mitambo hiyo na silaha za nyuklia zilikuwa ni kwa ajili ya kujihami tu.
Fidel Castrol akamsihi Khrushchev kwamba atumie silaha za nyuklia endapo Marekani wangeishambulia Cuba na Khrushchev hakutaka kufanya jambo hilo.
Khrushchev akiwa hataki vita na Marekani akakubaliana na Marekani kwamba angeondoa silaha na meli za kivita ambazo tayari zilikuwa katika pwani ya Cuba lakini kwa masharti kwamba Marekani iondoe meli zake za kivita katika pwani za Uturuki na Italia na pia itoe uhakika wa kutoishambulia Cuba.
Castrol akiwa amekasirishwa sana na kitendo cha Khrushchev akaweka mpango wa miaka mitano ambao alitaka Marekani wakubaliane nao kwamba kwanza ni kuondoa meli ya kivita kwenye pwani ya Guantanamo, kuachana na kuwasaidia wananchi wa Cuba walokimbilia Miami, kuacha kuingia bila ruhusa katika anga la Cuba na eneo la bahari ya nchi hiyo na pia kuondoa vikwazo vya silaha kwa nchi hiyo.