Masikini kuwaza kujenga nyumba ya kuishi ni umasikini pia

Masikini kuwaza kujenga nyumba ya kuishi ni umasikini pia

Wewe kapuku upanue vyanzo vya kipato chako ili uwe taita pia,siyo kwenda kuzika pesa.
Wewe ulizaliwa kwenye Meli sio.
Kwangu mimi ni Nyumba kwanza.
Napambana narudi Nyumbani kwangu.
Mambo ya kukumbushana kodi kodi za Nyumba sio kipaumbele changu.

Nyumba ya mtu ni utumwa tu. Upo Nyumba ya kupanga umestarehe zako na familia yako mala Mwenye nyuma kaleta notisi ya uhame anataka kujenga Godown hapo.
Au kaiuza ukaonane tena na mmiliki mpya ambaye hataki kupangisha tena.

Unaanza kuhangaika na Madalali.

Jenga dogo pesa inatafutwa wakati wote.
Nyumba ni heshima kwa tunao jitambua. Familia inatulia sehemu nzuri uliyoichagua na kula maisha bila ya Bughudha za mama Mwenye Nyumba.

Kupanga ni fedheha kwa sisi watu wenye heshima zetu.
 
Mimi nina mifano mingi sana!
Bila kuwa na biashara au shughuli ya kukufanya uwe na mzunguko wa pesa haijarishi umejenga lazima maisha yakupige!
Kikubwa kuliko vyote tufanye mambo kwa uwiano!
Tusijenge kuonekana tunajenga tu mda mwingine hata ubora wa nyumba ni mdogo!
Tujenge kwa kujua kesho kuna maisha pia na nyumba haitaingiza fedha ni Liability kwa hiyo lazima tujue gharama ziko pale pale na haziepukiki!
Hata watu wanaostaafu na kupata changamoto ya kiafya baada ya uchumi kupungua sio kwamba huwa hawana nyumba ila huwa hawana fedha ndo maana yanawatokea madhira ya kiafya na kufa mapema!
Mkuu kila mtu ana kipaumbele chake anacho ona kinampa furaha maishani mwake,sio razima kila mtu awaze kama ww unavyo waza ,alafu kingine si kila mtu anaweza fanya biashara, biashara ni kipaji.

Ww unavyo yachukulia maisha sio anavyo yachukulia mwingine na ndio maana kuna baadhi ya watu wakipata hela hawawazi hata kujenga wala kufanya biashara bali anaenda kuzinywa pombe na kuhonga malaya kwa sababu anaamini kuwa hicho ndo kinacho mpa furaha.
 
Hapa tunajadili na vijana wanaojifanya wachumi kwa kusoma theory za Robert kiyosaki anayehubili kujenga ni kuzika pesa na wao bila kufikiria wanajiona wajanja na washauri wa kibiashara huku wakijua kabisa mifumo yetu ya kibiashara sio sawa na ya ulaya

Hata kiyosaki mwenyewe alikuwa akinunua nyumba na kuziuza baadaye akijua thamani ya ardhi hupanda bei

Jidanganye kukuza mtaji na huna kiwanja ukifikiria bei inakungoja wewe mtakavyokuja jenga kipindi cement mfuko laki moja ndio akili itakuwa sawaaa
Arafu sio kwamba anayeanza kujenga ni fala kuwa hawezi kuja fanya biashara
 
Kama hujaoa huwezi kuelewa mkuu
Em oa af ubanane na familia yako na familia zingine kwenye nyumba za watu
Sio kila unachosoma kutoka kwa motiveshno spika wa kizungu kina apply the same here in Africa!Big NO
 
Unaponda walio jenga wakati huo unaishi kwenye nyumba iliyo jengwa na wanaume wenzio hivi una akili kweli?

Kama kujenga hakuna maana mbona hujaenda kuishi juu ya mti?
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Nimesoma post yako nimegundua wewe bado ni mtoto mdogo, yani kula kulala.

Hata me kipindi naishi kwa dingi niliamini kama hivyo uaminivyo, ila nilipo kua, kuoa na kubarikiwa watoto, mawazo hayo sina tena.

Dogo hakuna kitu cha kinyonge kama kudaiwa kodi

Na unapokua na Nyumba yako, hatakama unakula ugali na mchicha kila siku, lakini unakua huna pressure za hapa na pale.

Kua kwanza ujitegemee utayajua haya.
Point
 
"SIZITAKI MBICHI HIZI"

Niliwahi kukutana na dogo mmoja ambaye alikuwa anamsema baba yake kuwa amezika pesa kwa kujenga ile nyumba yao ya kuishi (ni ya ghorofa). Wakati akimsema hivyo mzee wake, yeye mwenyewe anaishi kwenye hiyohiyo nyumba. Tangu amalize digrii yake ya biashara, yupo tu nyumbani. Kazi yake kubeba vyuma (kupiga nondo).

Mleta mada, ukikua, utaelewa tu. Subiri majukumu yaanze. Sasa hivi endelea kusoma vitabu vya motivational speakers.
 
Ukitaka kuona Umuhimu wa Kujenga, Kufa alafu uache watoto wako 3 ama 4 kwenye nyumba ya Kupanga.

Hata kama unadhani ni umasikini kuanza kujenga lakini ni muhimu sana Kaka. Tafakari kwenye hilo

Hakuna Baba mwenye gari ila kuna Baba mwenye nyumba.

Sasa utaonaje umuhimu wakati umeshakufa.
 
Nimezunguka sana nyumba za kupanga faida niliyoipata ni kukosa furaha na amani ndani ya nyumba hizo..

Sasa nipo kwangu wanangu wanazunguka ndani ya fensi Kwa furaha mtambuka...

Kupanga ni kuchagua. Over

Kujenga muhimu
 
Mtu unajibana wee Ili ujenge nyumba ya kuishi, ukimaliza unaanza kuishi kwenye hiyo nyumba kwa tabu nyingi. Ingekuwa na maana kama kungekuwa na maisha bila kifo, umasikini uliouchochea kwa kujenga ungepambana nao kwa kuwa muda upo tu. Kama we masikini pambana uweze kipato cha uhakika ambacho ndio kitawezesha mengine ikiwamo ujenzi.
Kijana mshkuru shemeji yako kwa kuwastiri wewe na dada yako, Umekalisha kende kwenye sofa la shemeji na umepata ujasiri wa kuwatusi watu wanaojibana ili kupata makazi ya familia zao.
 
Ukiwa na uchumi imara utaweza kujenga nyumba ya ndoto yako na kwa muda mfupi sana. Nyumba ni muhimu sana sana lakini jengeni uchumi imara kwanza, ili usije kupata mateso ya kujenga nyumba kwa miaka kumi plus
 
Hii ndo hoja.
 
Generational Poverty haiwezi kuisha kwa mentality kama hizi za kwenye comments nilizo pitia.
 
Kujenga siku hizi ndo habari yenyewe, wanaokataa, kujenga ingali anafamilia na anawatoto, heri kuchuguzwa kihakili, eithar kaathiriwa na nini hapa duniani. Kujenga sawa na kupata uhuru rasmi.
 
Wewe ulizaliwa kwenye Meli sio.
Kwangu mimi ni Nyumba kwanza.
Napambana narudi Nyumbani kwangu.
Mambo ya kukumbushana kodi kodi za Nyumba sio kipaumbele changu.

Nyumba ya mtu ni utumwa tu. Upo Nyumba ya kupanga umestarehe zako na familia yako mala Mwenye nyuma kaleta notisi ya uhame anataka kujenga Godown hapo.
Au kaiuza ukaonane tena na mmiliki mpya ambaye hataki kupangisha tena.

Unaanza kuhangaika na Madalali.

Jenga dogo pesa inatafutwa wakati wote.
Nyumba ni heshima kwa tunao jitambua. Familia inatulia sehemu nzuri uliyoichagua na kula maisha bila ya Bughudha za mama Mwenye Nyumba.

Kupanga ni fedheha kwa sisi watu wenye heshima zetu.
Huyu dogo mwenyewe tunamuelewesha hapa kapanga hosteli pale ARU
 
Hapa tunajadili na vijana wanaojifanya wachumi kwa kusoma theory za Robert kiyosaki anayehubili kujenga ni kuzika pesa na wao bila kufikiria wanajiona wajanja na washauri wa kibiashara huku wakijua kabisa mifumo yetu ya kibiashara sio sawa na ya ulaya

Hata kiyosaki mwenyewe alikuwa akinunua nyumba na kuziuza baadaye akijua thamani ya ardhi hupanda bei

Jidanganye kukuza mtaji na huna kiwanja ukifikiria bei inakungoja wewe mtakavyokuja jenga kipindi cement mfuko laki moja ndio akili itakuwa sawaaa
Arafu sio kwamba anayeanza kujenga ni fala kuwa hawezi kuja fanya biashara
Huyu Bado kijana mdogo. Haoni utofauti wa nadharia na maisha halisi.

Tulivyokuwa chuo 1+1= 2 intact. Mtaani 1+2 unapata jibu lolote likiwemo 0. Huwez kugarantee biashara na kuacha kujenga. Kuna Leo na kesho. Huyu dogo karithi hela na mawazo ya wenye hizo hela. Muacheni
 
Sasa utaonaje umuhimu wakati umeshakufa.
Utaona umuhimu kupitia waliokutangulia kufa.

Kuna msiba nimehudhuria juzi, mke wa marehemu analia kuachwa na watoto 3 alafu Marehemu alikuwa hajajenga, walikuwa wanaishi kota za Serikali.

Maana anajua baada ya mazishi ya mumewe atatakiwa yeye na watoto watoke kwenye hizo kota na wakaanze maisha ya kupanga.

Kama utapata nafuu jenga mapema kuepusha usumbufu kwa wategemezi wetu

Kwa maana familia nyingi tunaonza kufa huwa ni Sisi akina Baba 😢
 
Back
Top Bottom