Tatizo la watu hawajakuelewa wako wanajua hutaki kabisa kujenga!Nachomaanisha masikini kama unaona kabisa huna kipato cha kuanzisha ujenzi basi hicho kidogo peleka kwenye msosi, mavazi na mengine huku ukiendelea kuimarisha vyanzo vya pesa. Vyanzo vikiruhusu Jenga.
Ukiwa na kipato cha uhakika utajenga bila kuyumbisha mfumo wako wa maisha!
Ndo maana maisha ukae kwenu,upange au ujenge gharama za maisha ziko pale pale!
Kwa wale wenye kipato cha uhakika wajenge tu hakuna shida!
Ila kama unajitafuta unapata 20,000 kwa siku unataka ujenge familia ile hapo lazima uchemke!
Kwa nini usiwekeze kwenye kitu uanchofanya huku ukifanya saving na kuwekeza kidogo kidogo na baadae itapanda na kufikia hata 50,000 kwa siku na hapo unaweza kuanza kujenga pole pole bila kuvuruga mtaji!
Ila kuanza kujenga tu bila kutazama uchumi wako vizuri lazima kwa mbeleni uje uteteleke na waliopanga watakuzidi ubora wa maisha!