Masikini kuwaza kujenga nyumba ya kuishi ni umasikini pia

Masikini kuwaza kujenga nyumba ya kuishi ni umasikini pia

Ni muhimu sana kujenga.

Me nakumbuka msoto tulioupitia baada ya Mzee kufariki hivyo kutakiwa kuondoka kwenye kota za Serikali tulizokuwa tukiishi.

Bi mkubwa alichanganyikiwa sana maana familia ilikuwa kubwa na Mzee hakuwa amejenga hadi anapatwa na umauti
 
Utaona umuhimu kupitia waliokutangulia kufa.

Kuna msiba nimehudhuria juzi, mke wa marehemu analia kuachwa na watoto 3 alafu Marehemu alikuwa hajajenga, walikuwa wanaishi kota za Serikali.

Maana anajua baada ya mazishi ya mumewe atatakiwa yeye na watoto watoke kwenye hizo kota na wakaanze maisha ya kupanga.

Kama utapata nafuu jenga mapema kuepusha usumbufu kwa wategemezi wetu

Kwa maana familia nyingi tunaonza kufa huwa ni Sisi akina Baba [emoji22]

Unachokisema ni sawa na mtu kusema unaweza kuacha nyumba na mali zingine ili ziwasaidie lakini wakauza na kuanza maisha ya kupanga.
 
Mleta mada 0 - 7 Waliojenga & Wanaojenga.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
Shida analeta mambo ya ki bongo movie kwenye maisha halisi ,hakuna mtu anayejielewa hata hao anaowasema wafanya biashara wanarelax kwenye nyumba za watu hasa mji kama dar es salaam

Ni ndoto ya kila mwanaume na mwanamke mwenye akili timamu kuwaza kujenga akipata hela mkononi ya kufanya hivyo

Huyuu kasoma vitabu vya Robert kiyosaki ndio maana kuhamisha akili zake mazima bila kuchuja kwa mazingira yake kama ina make sense kwa kila kitu
 
Mawazo ya kimaskini kabisa haya, hizo nyumba zinapigwa bei ili watoto wapate mitaji wafanye mambo yao.
Hiyo umechukulia kwenye upande mmoja.

Fikiria hujajenga na umekufa na kuacha familia kwenye nyumba ya kupanga.

Ndiyo maana tunahimizana kukumbuka kujenga tukiwa hai.

Bila kusahau kujiwekeza hata kwa biashara na kilimo/ufugaji
 
Mtu unajibana wee Ili ujenge nyumba ya kuishi, ukimaliza unaanza kuishi kwenye hiyo nyumba kwa tabu nyingi. Ingekuwa na maana kama kungekuwa na maisha bila kifo, umasikini uliouchochea kwa kujenga ungepambana nao kwa kuwa muda upo tu. Kama we masikini pambana uweze kipato cha uhakika ambacho ndio kitawezesha mengine ikiwamo ujenzi.
Huu ni mtazamo hasi tena wa kimasikini.
 
Kujenga muhimu yaani pesa yako unaona kabisa ilivyotumika .

Biashara hata kuweka pesa bank ni kubet mule mule ,siku moja unaweza kulia na kupoteza pesa zote..

Ukipata pesa jenga hata nyumba ya million 300 kama ipo ndani ya uwezo wako ,nyumba ni heshima na muhimu sana ... Biashara hizi ni maisha ya kubahatisha na kuweka rehani roho yako..

Hata wanyama na ndege wanajiwekea sehemu ya kuishi mapema .
 
Ni muhimu sana kujenga.

Me nakumbuka msoto tulioupitia baada ya Mzee kufariki hivyo kutakiwa kuondoka kwenye kota za Serikali tulizokuwa tukiishi.

Bi mkubwa alichanganyikiwa sana maana familia ilikuwa kubwa na Mzee hakuwa amejenga hadi anapatwa na umauti
Na ndio maana kwa watumishi wengi wanaona bora ukope ujenge ilii majanga kama haya yakitokea wategemezi wasidhalilike sio hivyo tu kuna kufukuzwa kazi ,kuumwa mda mrefu n.k ukiwa kwenye upangaji ni mateso mkubwa
 
Unachokisema ni sawa na mtu kusema unaweza kuacha nyumba na mali zingine ili ziwasaidie lakini wakauza na kuanza maisha ya kupanga.
Hata kama itatokea wakauza hizo nyumba lakini watabakiza za wao kuishi.

Binafsi sitapenda Watoto wangu wasumbuke nyumba ya kuishi ama chakula wakati nina nafasi ya kuwajengea nikiwa hai.

Hela ya kula watapata kwenye kodi kwenye nyumba ya wapangaji.
 
Na ndio maana kwa watumishi wengi wanaona bora ukope ujenge ilii majanga kama haya yakitokea wategemezi wasidhalilike sio hivyo tu kuna kufukuzwa kazi ,kuumwa mda mrefu n.k ukiwa kwenye upangaji ni mateso mkubwa
Sahihi Mkuu

Kupitia tukio lile nimejifunza kujenga na kuwekeza kwaajili ya kesho ya watoto wangu.

Hata kama itatokea Mama yao akaja kuolewa tena baada ya Kifo changu lakini watoto wangu wasiteseke, maana huwa ni ngumu Mwanaume akampenda Mke mwenye Watoto 3 na zaidi alafu akawa anawahudumia kama wanae wa kuwazaa
 
Ukumuelewa nilivyo muelewa nikwamba bora kuimalisha uchumi kwanza kisha mengine yatafuata tena kwa wepesi,mfano mama rishi au muuza nyaya au mbeba mizigo anajibana kwa ajili ya kujenga nyumba badala ajibane kupanua wigo wa kazi yake mfano mama rishe kutwa anaungua moto bora ajibane abadilishe kazi kisha atajenga kuliko kujenga na kuhamia huku ukiendela kubeba mizigo mabibo
Ni sahihi Mkuu lakini biashara hufirisika na kuisha wakati nyumba ni asset inaweza kuja kuwatunza wakati biashara zimeshindwa kuzalisha faida
 
Hii kauli dah[emoji3][emoji3]
Sasa nikishakufa nitawaonaje tena hao watoto
Tunajifunza kupitia mifano.

Hujawahi kuona watu wanaopitia hiyo hali, wengine watakaokuwa hai wanaweza kujifunza kwako ukiwa kama mfano.

Wanaume tunawahi kufa mapema kabla ya wake zetu.

Kwenye kila familia 10 unaweza kuta 3 ndiyo Baba za familia wapo hai ila 7 walishatangulia mbele ya haki
 
Hata kama itatokea wakauza hizo nyumba lakini watabakiza za wao kuishi.

Binafsi sitapenda Watoto wangu wasumbuke nyumba ya kuishi ama chakula wakati nina nafasi ya kuwajengea nikiwa hai.

Hela ya kula watapata kwenye kodi kwenye nyumba ya wapangaji.
Wewe kumbe unazungumzia nyumba ya biashara! Hapo sawa!
 
Ni sahihi Mkuu lakini biashara hufirisika na kuisha wakati nyumba ni asset inaweza kuja kuwatunza wakati biashara zimeshindwa kuzalisha faida
Nyumba ya kuishi sio asset kaka! Nyumba ya biashara ndo asset! Sasa kama maisha yakikushinda utauza nyumba yako unayokaa hapo tayari ushafeli!
 
Wewe kumbe unazungumzia nyumba ya biashara! Hapo sawa!
Zote muhimu, ya kuishi familia then ya biashara.

Hata kama utakufa ukiwaacha watoto wako Secondary wanaweza kusoma bila changamoto
 
Nyumba ya kuishi sio asset kaka! Nyumba ya biashara ndo asset! Sasa kama maisha yakikushinda utauza nyumba yako unayokaa hapo tayari ushafeli!
Sio asset kivipi Mkuu?

Imagine hauna hata hiyo ya kukaa vipi zile kodi unazotakiwa kulipia kila mwaka?
 
Afuu nilichojifunza kwenye kujenga ni kama addiction fulani kama vile ulevi ,uvutaji sigara ,umalaya au punyeto tu ukianza kujenga nyumba moja ndio ufunguo wa kujenga nyumba nyingine zaidi za biashara au za makazi ndio maana yule fisadi alikuwa na nyumba 75 kila mkoa
 
Ukitaka kuona Umuhimu wa Kujenga, Kufa alafu uache watoto wako 3 ama 4 kwenye nyumba ya Kupanga.

Hata kama unadhani ni umasikini kuanza kujenga lakini ni muhimu sana Kaka. Tafakari kwenye hilo

Hakuna Baba mwenye gari ila kuna Baba mwenye nyumba.
Asipoelewa hii comment huyo atakua mtu wa ajabu mno
 
Back
Top Bottom