Masikini wanaishi maisha ghali kuliko matajiri

Masikini wanaishi maisha ghali kuliko matajiri

Nifafanue tena!
Sawa yaani wakati maskini mimi napanda gari mfano Mbagala kwenda makumbusho natoa nauli bei gani ?
Na wakati huo huo Tajiri anatoka Mbagala mpaka makumbusho kwa gari yake anatumia mafuta ya bei gani?
Ili tuthibitishe kauli yako kuwa sisi masikini tunaishi ghali kuliko matajiri..
Umefikiria pia kuhusu ghara ya muda na hizo inconveniences za kupumuliana, kuibiwa nk
 
Sidhani kama kuna mtu anabisha, let's look on this example; Masikini coz hana hela itambidi badala ya kununua mchele kwa bei ya jumla ya sh. 2,100 itampasa anunue kwa rejareja kwa sh. 2,500.

Badala ya kununua gesi mtungi wa kila 15 kwa 56,000 italazimu anunue mtungi wa gesi wa kilo 5kwa sh.22,000.
Mfano mwingine: Kwa kuwa masikini Hana uwezo wa kununua gesi anaamua kununua mkaa, atajikuta anatumia mkaa wa 2000-3000 kwa siku,ukiweka kwa mwezi ni 60k, ukiweka na dhamani ya muda inaweza fika 80k badala ya 56k

Leta mifano mingine.
Umetumia uzoefu wako binafsi au dhaania kaka??
 
Unajua kuna vitu ni vya kijinga kuanzia mwanzo. Wewe unajua expanses za mtu tajiri?
Nazijua...angalia percentage wise kwenye kipato chake au angalia gharama anazoingia ukilinganisha na masikini
 
Nashukuru kwa kunielewa...mwalimu akikopa anawekewa riba ya 35% wakati Bakhresa anapaswa mkopo wa riba ya .2% tena kwa kubembelezwa
Bakresa hakopi milioni bali mabilioni.
In figure rate ya mkopo Mwalimu ipo juu
 
Hapana kaka sikupingi nimekuuliza una experience kama tajiri au masikini!!!Maana mimi ni tajiri nataka nikupe experience yangu kwa siku naweza tumia hata 200k!!!Ndio maana nikakuuliza wewe ni tajiri au masikini
Mimi masikini...kutumia 200k kwako inaweza kuwa ni sehemu ndogo sana kwenye kipato chako...ukitaka huduma unaweza zipata kwa bei rahisi kuliko masikini
 
Back
Top Bottom